Monday, 23 October 2017

KONGA MANO LA ROHO MT karismatic katoliki

Tags

Sunday, 22 October 2017

HIVI NDIVYO BIBLIA INAVYO MTAMBULISHA MUNGU (SOMO LA 2) kisimachabaraka.blogspot.com

Tags



BIBLIA  INAVYO MTAMBULISHA MUNGU  (SOMO LA 2 )- Kisimachabaraka.blogspot.com.

Mpendwa huu ni mwendelezo wa kipengele tulicho anzanacho tuliweza kuona baadhi ya mistari inayo mtambulisha Mungu na ina husunini lakini leo Mungu ametupa tena neema ya kuitazama mistari hii michache endelea kupitia katika Biblia yako ili umjue zaidi Mungu kwa maana mistari kama hii inaonesha sura halisi ya Mungu ,na pia baada ya kumjua vema utaweza kuwa imara pasipo kutegemea zaidi imani ya mtu mwingine kwa maana uwepo wa Mungu aliye hai utakuandama .endelea kupitia nitakuletea mistari mingine iliyo sheheni namna Biblia inavyo mtambulisha Mungu lakini katika Agano Jipya pekee yake kwani hapa niliichanganya ,hapo utapata sifa nyingine nyingi ambayo hujaziona hapa wala katika kipengele kilicho pita.lakini usisahau kushare na mwenzio mambo kama haya  ,iwe ni kwa watsApp Facebook nk,karibu nami nina kutakia upitiaji mwema na Mungu aliye hai kupitia jina la Yesu akubarikii.Amen

Baba wa watu                              ( Ebr 2;11-13)  (Isaya 66;13)

 Mungu ni aliye jaa neema         ( Yn 1;14  )  (Omb 3;21-34)

Mungu ni asiye badirika            ( Isa 46  )    (Yn 8;58  )   ( Ebr 13 ;8)

Mungu ni mwaminifu                (Rum 8;35-39) 

 Mungu ni upendo                    ( Yn 15;13)

Mungu ni mhukumu wa watu wote               2 ( Tm4;8)

Mungu ni  nuru /mwangaza                             (Dan 2;22) (Yn 8;120)

Mungu ndiye  Bwana  wa  utukufu                (Lk 9;26-36)

Mungu ni mwenye hasira kuhusu uovu        ( Mk 3;5) ( kum 29;19-29)

Mungu ni Mungu aliye mahali popote        ( 1Fl 8;27)   (Mt 18;20 )   ( Efe 4;10 -55)

 Tutaendelea ,endelea kupitia lika siku upate vitu vipya  

                      limetolewa na  E.mkinga

NB;share kwa marafiki zako  kwa kupitia account zao za 

           WatsApp  Facebook  Twitter  Instagram  nk

                                 KISIMA CHA    BARAKA 
                          kisimachabaraka.blogspot.com

Saturday, 21 October 2017

TAARIFA MUHIMU KWAKO

Tags



KARIBU TUNATOA HUDUMA YA KUINGIZA TAARIFA MBALIMBALI YOU TUBE KAMA VILE NJIMBO ZA INJILI KWA MWIMBAJI YEYOTE ANAYE HITAJI HUDUMA HI I UNAKARIBISHWA ,AU KITUCHOCHOTE UNACHO HITAJI KIWAFIKIE  WATU KIURAHISI .TUMA ujumbe kwa watsApp,tuta utaingizwa kwenye group na wasiliana humo vizuri ,na hii itakusaidia kupata taarifa za matukio mbalimbali kwa wakati na utajua yanayo endelea kwenye blog hii ya kisima cha baraka.mpe na mwenzako taarifa hii barikiwa 

                  
                             



                       

Thursday, 19 October 2017

HIVI NDIVYO SHETANI ANAVYO FANYA KAZI

Tags

 

    NAMNA SHETANI ANAVYO FANYA KAZI 
            

 Hapa tuta kuletea siri nyingi za namna shatani anavyo fanya kazi akifikiri nisiri kumbe ziko wazi,nakutakia utembeleaji mwema wa ukurasa huu.

                                                     
  
    Shetani kazi yake ni kuiba na kuharibu kuua nk ,yeye hana uhalali wa kumiliki chochote lakini Mungu pekee ndiye mmiliki wa vyote,shetani ni mwizi   ni muharibifu ,Mungu aliumbe  shetani akanuia kuchafua kazi ya Mungu,
Uharibifu mmoja wapo anao ufanya ni kuharibu watoto wa Mungu akiwataka wamfuate yeye kwa lazima ,ili kwamba siku ya kuhukumiwa kwake asiwe pekeyake .Njia nzuri kwake anayo itumia ili kuwapata watu wa Mungu ni kuwatengenezea mitego ya kumkosea Mungu wao ili wafarakane na Mungu wao aliye mtakatifu na muumba (dhambi )kisha hupata nafasi ya kuwachukua kirahisi kabisa nakuwapeleka mbali sana kwasababu ya uovu wao,chaajabu wakitambua na kutubu shetani huwaachilia nao hurudishwa  na kuketi na Mungu wao kwa raha musharehe na kinacjo mfanya awaachlilie ni maamuzi ya mtu aliye tekwa anapo hitaji msaada wa Mungu kwakumaanisha ndiposa damu ya Yesu kristo msalabani inapo chukua nafasi kwa nguvu zaajabu na kuwaokoa ( he we we umempaYesu maisha yako? ) chukua hatua maana muda umekwisha yadunia yanapia,bado kitambo kidogo mwana wa adamu atashuka mawinguni kama tulivyo mwona akienda zake ,ndipo kila mtu atakapo hukumiwa sawasawa na matendo yake.                                                                  
    NAKIBOKO CHAKE NI SADAKA  YA YESU KRISTO MSALABANI.   
          Kwa kupigwa kwake sisi tumepona
                                  

                      
                                   Inakuja 
                                      

MAJINA YA MUNGU NA MAANA ZAKE

Tags

MAJINA YA MUNGU NA MAANA ZAKE 

                                   


Hapa tuta jifunza chanzo cha majina hayo ili ikusaidie kujua vema ukuu wa Mung wetu aliye                                                                                  
         endelea tu kupitia ukurasa kila siku

HAWA NDIO MATAPELI WANAO ZUNGUKA DUNIA NZIMA KILA SIKU USIKU NA MCHANA

Tags
             

  HAWA NDIO MATAPELI WANAO ZUNGUKA DUNIA NZIMA  KILA SIKU USIKU NA MCHANA .

Hawa ni baadhi tuu lakini kupitia hawa basi ujifunze kitu na ikiwa ni wewe mmoja wapo basi acha maramoja tabia hiyo maana huu ni muda wa kuyatenda yaliyo mema Najua utasema mengi kutokana na makundi haya nakukaribisha kutoa comment zako kwani kusifiwa na kusemwa ni sehemu ya maisha ya binadamu na sio kila kitu kinaweza kukubalika kwa watu wote hata Yesu hakukubalika kwa watu wote mpaka leo,lakini watake wasitake Yesu atabakikuwa Bwana wa mabwana,na mkombozi wa ulimwengu
      
                                                          HAYA NI BAADHI  YA MAKUNDI YA MATAPELI
  • Manabii wa uwongo, wana tabia ya kuwaaminisha watu kitu ambacho Mungu haja watuma waseme kwa watu ,lakini pongezi ziwafikie manabii wa kweli.

  • Wahubiri wanao hubiri pesa badala ya kumuhubiri Yesu kristo aliye hai ili wanadamu waokolewe

  • Watoza ushuru wanao toza zaidi ya kiwango kilicho pangwa,

  • Walimu wanao watongoza wanafunzi ili waweze kufanya nao mapenzi (watoto wao ),acha kuwapeteza watoto wako

  • Wanawake wanao wahitaji kuolewa kwa wanaume wenye pesa (huu sio  mpango wa Mungu )ni utapeli ulio jificha

  • Waganga wa kipepo.wanaacha kumwacha Yesu kristo aponye wao wanajifanya wanaponya (acheni utapeli kwajina la Yesu kristo )

  • Wafanya biashara wanaotumia nguvu za giza.watu wakifika kwenye maduka yao wanaona maduka yame jaa bidhaa halali na wana nunua humo  ,kumbe kwenye ulimwengu wa Roho sio bidhaa kama zinavyoonekana   bali ni  viungo  vyawatu na vitu vingine vichafu (huo ni uchawi mchana  kweupe) acha maramoja kwajina la Yesu maana huhumu yako ungefanikiwa kuiona usingeendelea,kufanya utapeli huo kwaajili ya kupate mali zisizo halisi unaamua mpaka kufanya uuaji.

  • Watu wanao hubiri dini badala ya kumuhubiri Yesu kristo iliwatu waokolewa waende mbinguni (acha mara moja )anza leo kumuhubiri kristo Yesu ili dunia ijawe na nguvu za Mungu kupitia mwanaye Yesu kristona sio kujawa na nguvu ya dini

  • Wanaume wanao tumia pesa au utajiri kuwatapeli wanawake ,acha maramoja tumia utajiri wako kutapeli bali tumia kwaajili ya sifa na utukufu kwa Bwana ,watu wote uliowapoteza utajibia

  • Wanajeshi wanao furahia kuwapiga watu virungu  bila sababu za msingi  na kuwajengea watu hofu ya kuwaogopa ,badala ya  kujenga nao urafiki mzuri maana ndio walinzi wawatu wote (Mlinzi wako akikutaka umuogope maana yake nini?na ukimuogopa kuna siku ataweza kukufanyia nini?.jibu unalo mwenyewe.

  • Watu wanao hubiri zaidi habari za mafanikio ya mwilini badala ya kuhubiri habari za toba ili watu watubu na kuingia mbingun                                NB; kuwa makini usitapeliwe  mfanye Bwana Yesu kristo kuwa kiongozi wako katika Roho mtakatifu                                                                                              E.mkinga


NB;share kwawenzako nao wapate ujumbe

                                                                               WatsApp   Twitter   Facebook   Instagram  
                                    
        KISIMA CHA BARAKA

                                  Kisimachabaraka.blogspot.com

MASWALI MBALI MBALI YAHUSUYO IMANI HALISI YA KIKRISTO

Tags
   

 MASWALIO YA KIIMANI YATOKANAYO NA BIBLIA




                                                  

1.   Kwanini Mungu ali mruhusu Ibrahimu kumtoa mwanaye wapekee kama sadaka ya kuteketezwa ?
Jibu;   Kwasababu Mungu alitaka aijaribu imani ya  Ibrahimu  juu ya Mungu aliye hai kama nithabiti nndio maana akahesabiwa haki kwa imani yake kuwa thabiti  (Mwanzo 22;16) (Ebrania 11;8-9)

2.    Kwanini Mungu aliamua kugairi Isaka asitolewe sadaka ya kuteketenzwa nabadala yake  akamtwaa mnyamaa katika kichaka kwaajili ya sadaka ?

Jibu;  Kwasababu Isaka alikuwa mtoto wa agano kati ya Ibrahimu na Mungu  ya kwamba kupitia Isaka Ibrahimju atakuwa na watoto wengi kama mchanga wa Baharini na kama Nyota wa angani na Mungu hawezi kuvunja agano lake (Mwanzo 22;17)

3.   Kwanini Mungu hakuamua kufanya sadaka ya Isaka kuteketezwa kuwa kama fidia ya dhambi za wanadamu dunia nzima ?

Jibu; Kwasababu Isaka hakuamua mwenyewe kuwa sadaka kwa ulimwengu na kufa kwaajili ya watu,kwakuwa sadaka ya ukombozi wa ulimwengu haikuhitaji mtu kuteseka tuu  bali ilihitaji mtu aliye amua kwa dhati kujitoa kwaajili ya kuteseka kwaajili ya watu  hivyo ilihitaji mtu aliye na shahuku  na aliye amua kujitoa sadaka bila manung’uniko  ndio maana baada ya kuona hakuna mwanadamu anaye weza Mungu akaamua kushuka mwenyewe kwa njia ya kujifanya kama mwanadamu wakawaida (Yesu kristo)

4.   Je inatupasa kumuheshimu ibrahimu?

Jibu ;   Ndiyo  Kwasababu yeye ni Baba wa imani aliye tufundisha juu ya imani thabiti ya Mungu halisi .Pia pia  kwasababu ni wazao wake kama alivyo ahidiwa kuwa atakuwa na watoto wengi kama mchanga wa baharini na  Nyota za angani(yeye ni Baba yetu wa imani)ingawa hapaswi kuheshimiwa zaidi ya Mungu   (Mwanzo 22;16) (Ebrania 11;8-9).

    Yataendelea; endelea kupitia tu kila siku

                                               E.mkinga



NB;share na wenzako nao wapate ujumbe.


                
             WatsApp  Twitter   Facebook   Instagram  
                                     

                                     KISIMA CHA BARAKA
                                  Kisimachabaraka.blogspot.com


Wednesday, 18 October 2017

MAAJABU YA UUMBAJI WA MUNGU

Tags



Jifunze kutafakari namna Mungu alivyo waajabu na mkuu kupitia uumbaji wake
        
                            

Tafakari kwa njia ya picha hizi nanyingine zitaingizwa zinazo kupa kutafakari juu ya uumbaji
                                                








Tuesday, 17 October 2017

HAKUNA KITU KIZURI NA KIBAYA KAMA NDOA,

Tags
        

    HAKUNA KITU KIZURI NA KIBAYA KAMA NDOA,
                        
                     (huu ni muhutasari tu)
                                                  




Najua unazo tafsiri zako juu ya ndoa lakini,dhana yangu na Maelezo haya machache yatajikita kuzungumzia zaidi maisha ya ndoa( maisha ya ndoa)kwasababu maisha yake ndiyo yanayo zaa mjadala.na sio tafsiri kama wengine wanavyo tafsiri

Ndoa, ni aina ya maisha yanayohusu jinsia mbili tofauti  ,kwa kibali au idhini ya kanisa au serikali.watu hao wawili wanapo kubaliana kwaidhini hiyo wanakuwa na uhalali wa kuishi pamoja kama mume na mke wakizaa watoto na kwenda mbinguni,

Mpendwa wangu,moja kwa moja nianze kukuonesha vitu vichache juu ya mtazamo wa kichwa cha hapo juu maarufu kama  HAKUNA KITU KIZURI NA KIBAYA KAMA NDOA ,hii ni kutokana na watu wengi kuona na kusema kuwa ndoa ni mbaya na wengine wakisema kuwa ndoa ni nzuri lakini leo nataka nikupe suruhisho la mjadala huu.kwa kuorodhesha tu baadhi ya uzuri na ubaya wa ndoa kisha nitasuruhisha,mwishoni

                                  FAIDA ZA NDOA

Humwezesha mwanandoa kuishi maisha ya amani  na yaliyo jaa ushindi mkuu dhidi ya dhambi ya uzinzi.hii ni kwasababu maandiko matakatifu yana idhinisha kuoa kuliko kuwakwa tama mpendwa, kimsingi ikiwa huja oa ina maana utawatamani wale ambao sio wakezako bali ni wake za watu au wajane au wasio olewa  au wanaume za watu  ,kwasababu kutamani mwanamkeau mume  asiyo wako ni kosa (1petro 2;14) ,(1Kor 6;9)

Ndoa inasaidia kusudi la Mungu kutimia,lengo  mojawapo laMungu kumuumba mwanadamu lilikuwa ni kuitunza nchi ambayo imeumbwa na ndio maana mwanadamu aliambiwa akailime na kuitunza hiyo nchi na kitendo cha kuruhusu kuzaliana ni kutokana na ukubwa wa dunia na rasilimali zilizopo juu ya  kazi ya kutunza uumbaji inavyo hitaji watu wa kutosha   Mwanzo 9;7) ,(Mwanzo 1;27),wakaambiwa zaeni mkaongezeke  mkaijaze nchi na kuitiisha,soma hizo aya utaona mambo ya siri sana ambayo Mungu alikusudia

Ndoa ina weza kusaidia kukuza kipato cha familia ,hii ni kutokana na mshikanano na kusaidiana katika mawazo bunifu ya kimaendeleo baina ya wanandoa wenyewe .

                                HASARA ZA NDOA

          Simaanishi haifai au usifikiri kuwa nakukatisha tamaa ya kuoa au kuolewa  hapana bali nataka ujue unapo taka kuoa au kolewa uwe umejindaa vizuri ili kuepuka maneno machafu yanayo chafua kituchema kilicho andaliwa na Mungu (ndoa)

  • Ina weza kumsababisha mtu akawa na majuto na stress nyingi,hii hutokana na migogoro katika ndoa hiyo ,ingawa migogoro hii inawezekana kabisa kuisha na wanandoa wakaishi kama  paradiso

  • Inaweza kumkatisha mtu tama ya maisha

  • Ina weza kumtengenezea mtu maumivu ndani ya nafsi yake

  • Inaweza kumpotezea mtu muda mwingi wakufanya mambo mengine kama kumtafuta Mungu nk,hii ni pale ndoa inapokuwa na migogoro isiyo eleweka ambayo ina mpamtu ulazima wa kuyafikiri hayo kuliko mengine ya   msingi zaidi

NB;Kwa asili ndoa ni njema ni nzuri kabisa lakini chanzo kinacho sababisha ndoa ionekane kuwa mbaya na wanadamu wenyewe andiko hili linadhihirisha kuwa ndoa ninjema ,kwasababu Mungu anapo umba kitu huwa hakosea vyote anaviumba kwa nia njema lakini watumiaji hutumia bilakujua utaratibunamna wa kukitumia kituhicho sawasawa na mapenzi ya Mungu (Mwanzo 1;31)

    MAMBO YA KUZINGATIA UKIWA NDANI YA NDOA        (MWANANDOA),AU KABLA YA KUOA AU KUOLEWA


Hapa ninachanganya zote lakini zitakufaa zote

  • Jiulize huyo unaye taka kuoana naye ,umempendea nii ,hii inasadia kudumisha uimara wa ndoa ,mfano ukimpendea uzuri wa rangi yake tu inamaana sikumoja akipata tatizo litakalo sababisha sura yake kuharibika itakuwa vigumu kumpenda au ukimpendea utajiri inamaana kuwa akifirisika basi na ndoa lazima ita firisika (kuvunjika),lakini ukimpenda kwa jinsi alivuo na atakavyo kuwa ndoa itadumu kwani ikiwa unampendwa jinsi alivyo upendo wako unanguvu ya kumbadirisha iwapo utajua kuutumia upendo kwa mabaririko na uimara wa ndoa yako

  • Mwombe Mungu akuoneshe chaguo sahihi, (kwa wasio oa au kuolewa ),mpendwa suala la kumwomba Mungu watu wengi huwa wanalipiga wanasema inatakiwa utumie akilizako kuchagua mke au mume sasa nikuachie wewe swali ,je,unataka kutumia akili zako katika kumtafuta mwenzi wako kwaajili ya ndoa kwani wewendiye uliye anzisha ndoa?utajijibu mwenyewe watu wengi wanaishia kwenye uchumba kwasababu hawamuulizi mwanzilishi wa ndoa kuwa ninani anafaa kuwa na mimi,kumbuka Adamu aliletewa mke sasa wewe unataka umchukue mke .unauhakika hapounapochukua ndio penyewe panapopatikana mwenzi wako,angalia usije ukachukua kiumbe kingine ,uliza kwanza wakwako mahali alipowekwa kazi yako nikwenda kumchukua sio kumtafuta unamtafuta kwani amepotea? haina shida ukitaka kuchukua wewe chukua tu utakacho kipata baadaye usinipigie simu,ikiwa unakubaliana na wazo hili kumbuka kuandika ndio hapo chini

  • Andaa akili zako na moyo wako kukubaliana na misukosuko au changamoto au utofauti utakao jitokeza wakati wa ndoa ,hii ni kwasababu hata kama lilikuwa ni kusudi la Mungu kuoana na mtu huyo lakini kumbuka yeye ni mwanadamu ana mapungufu yake kwahiyo jiandae

  • Uwe mvumilivu na msikivu juu ya ushauri anao utoa mwenzako

  • Usi mwone mwenzako kama chanzo cha matatizo bali chanzo cha baraka ,bali onya neni kwa upole na upendo wa agape

  • Unyenyekevu kwa mwanamke nijambo muhimu sana na ndilo linalo wateka wanaume wengi kuwapenda zaidi na kuwajali wake zao (Mithali 9;13)na (Mithali 31;11-12)

  • Mwana ume tambua kuwa huyo ni mwanamke usitake kumshurutisha mithili ya mwanaume kwasababu atabaki kuwa mwanamke akiwa na homin zake za kike na ndizo zinazo mfanya hatakama amesoma sana lakini kuna mambo atayafanya kama mwanamke ,na ndio maana wengi wao lazima wainuliwe kwasababu uwezo wa kujiinua nimdogo wanawake msiishangae hoja hii lakini usipojali utauona ukweli ndaniyake ukikosea hapo lazima mtagombana

  • Mwanamke mheshimu mumeo hatakama ni mdogo kwa umbile kwako au hana uwezo mkubwa wa kutafuta kipato mweshimu au hana  elimu kaqma wewe mweshimu ,wanawake wengi wakigundua wakojuu wanaanza dharau ,huu ni ushauri wa bure kwani maumivu ya nafsi utawapata wewe sio wanao kuonya ,kupitia heshima yako ndio dawa ya kumfanya awe mtu mzuri kwako,ukijifanya wewe kuwa bamsa huwezi kuolewa kirahisi na kamaumeolewa lazima mtagombana sana

  • Kuweni makini kwakutunza siri zenu za ndani hii ni kwasababu kuna baadhi ya mambo mkiyatoa nje yanaporudi ndani yanarudi yakiwa yamebeba maumivu misumali miba nk

  • Kila mmoja na awe mtii kwamwenzake (1Kor 7;4-5)

NB;Kuishi vizuri inawezekana ikiwa kila mmoja amesimama kwenye nafasi yake kwa upendo mkuu (2kor 2;14)

  • Kijana au vijana kuweni waangarifu msivutwe na mambo ya dunia,kwasababu yanapelekea mtu anapotaka kuoa au kuolewa anakuwa anavitu ambavyo vinawahusu wanandoa wakati yeye bado sio mwana ndoa mfano ;kuwa na mimba kabla ya ndoa ,kuzaa kabla ya ndoa hatakama utaolewa lakini umesha sababisha doa au mtu akipata magonjwa ya zinaa wakati sio mwana ndoa yaani anabeba mzigo usio muhusu,acha kuwabebea watu vifurushi usivyojua kikichomondani yake.

NB;ukikurupuka wakati wa kuoa au kuolewa unaweza kujutia wakati wa ndoa

  • Pia ikiwa umepanga kuishi bila kuoa au kuolewa ,ni marufuku kuingia kwenye uzinzi (usiwakwe tama maana kutamani mke  au mume asiye  wako ni kosa, (Mathayo 5:27-28) neno la Mungu linasema “mmesikia kwamba imenenwa,usizini,lakini mimi nawaambia kila mtuatazamaye mwanamke kwa kumtamani amekwisha kuzini naye moyoni mwake,pia soma  (1kor 6;8-9) na (1Kor 7;1-3).je umeifurahia makala hii na imekusaidia,na ina manufaa kwako?
NB;ubaya wa ndoa unakuja pale wanandoa wanapo gombana na kutokupata suruhisho,hapo ndipo wengi wanapoona kuwa ndoa ni mbaya kwasababu ya makosa yao kwani muda mwingine kunapotokea tatizo niwepesi kuomba msaada kwa washauri wakati dawa halisi wanayo wao wenyewe wakikaa pamoja kwa upendo na hekima ili kujadiri juu ya utofauti ulio jitokeza,hii ni muhimu kwani chanzo halisi cha migiogoro ya ndoa wanandoa wenyewe wanaijua,kwnai umewahi kusikia Ibrahimu na Sara waliwai kwenda kuomba ushauri wa ndoa yao ,au ndoa ya Yusuph na Mariam,uliwai sikia wamegombana na wakaenda kuomba ushauri nyie mnatatizo gani?
                
                               Imeandaliwa na  E.mkinga.

                                                  kisimachabaraka.blospot.com

                  kumbuka ku sharea  katika makundi mbalimbali ya watsapp/facebook twitter kila unacho kisoma kutoka blog hii , 

Monday, 16 October 2017

JIFUNZE KUSALI ROZALI TAKATIFU

Tags


                                       NAMNA YA KUSALI ROZALI TAKATIFU

 

                                                                        KUMBUKA


                                                  Share,watsapp
                                                          Share Facebook
                                                                  Share instagram
                                                                             Share twitter
                                                                                         Share uwezavyo

IJUE NGUVU KUU ILIYO JIFICHA KATIKA MSALABA WA YESU KRISTO MWANA WA MUNGU ALIYE HAI

Tags



    IJUE NGUVU YA MAAJABU ILIYOJIFICHA KATIKA MSALABA WA YESU KRISTO MWANA WA MUNGU ALIYE HAI.

      Be blessed in the name of the Father the son and the Holy spirity.Amen


                      
                 
  AHSANTE KWA KUENDELEA KUPITIA NA KUSUBIRI SOMO LIMESHA WEKWA WAALIKE NA WENGINE  NA UNARUHUSIWA KUTOA COMMENT HAPO CHINI AU KUSHUHUDIA JUU YA ULIVYO PATA MSAADA KUPITIA SOMO HILI ILI NIENDELEE KUKUOMBEA NA MUNGU AKUBARIKI ENDELEA KULISOMA TARATIBU KATIKA ROHO MTAKATIFU AMEN





             TAMBUA NGUVU YA MSALABA WA YESU

               ( soma katika Roho kwa kuhitaji msaada  ) 

Mpendwa hii ndiyo mada niliyo kuahidi kwamba nitakuletea  yenye maelezo machache yenye nguvu juu ya nguvu iliyo jificha kataka msalaba wa Yesu kristo.karibu twende pamoja.katika Roho mtakatifu

Muda huu nataka tuweza jifunza na kujua nguvu inayopatikana msalabani kwa Bwana yesu,.kimsingi neno msalaba lilianza kusikika sana baada ya kifo na ufufuko wa yesu ndipo siri ya msalaba ilipoanza kufichuka kwa kasi ,ingawa nguvu ya utendaji wa msalaba wa yesu kimsingi ulikuwako tangu kuwekwa misingi ya dunia lakini kutokana na nyakati na majira ya utendaji wa Mungu nguvu hii ya msalaba ilidhihirika zaidi wakatiwake maalum ulupofika wa kuzaliwa kufa na kufufuka kwa Bwana wetu yesu kristo .
            ( endelea kusoma katika Roho kwa kuhitaji msaada  ) 

Mpendwa kabla ya ujio wa yesu kwa njia ya kuzaliwa kupitia mwanadamu tunaona kuwa Yesu alikuwepolakini staili ya kuja duniani Mungu akaona niafadhari aonekane kama mwana damu iliwasiogope hata kutembea naye  na  aliendelea kutenda kazi lakini wanadamu hawakujua ya kuwa ndio yesu mwenyewe maana wakati wa udhihirisho wake ulikuwa bado lakini utendaji kazi wake ulisha kuwepo utendaji huu tuna uthibitisha kwenye kitabu cha {hesabu 21-4-9 } maandiko yanasema “wakasafiri kutoka mlima wa Hori kwa njia ya bahariya shamu ilikuizunguka nchi ya Edom watu wakafa moyo kwasababu ya ile njia 5 watu wakamnung’unikia Mungu na Musa ,mbona mmetupandisha huku?kutoka nchi ya misri ,ilitufe jangwani? Maana hapana chakula wala hapana maji na roho zetu zina kinai chakula hiki dhaifu 6 Bwana akatuma nyoka za moto kati ya watu ,wakawauma watu wakafa7 watu wakamwendea musa wakasema tumafanya dhambi kwasababu tume mnung’unikia mungu na wewe utuombee kwa Bwana atuondolee nyoka hawa .basi musa akawaombea watu .8 Bwana akamwambia musa ,jifanyie nyoka wa shaba ukaiweke juu ya mti na itakuwa kila mtu aliye umwa aitazamapo ataishi .9 Musa akafanya nyoka wa shaba ,akaiweka juu ya mti hataikiwa nyoka amemwuma mtu alipoitazama ile nyoka wa shaba akaishi . Mpendwa haya ni mambo ya rohoni ambayo kwakawaida unaweza jiuliza maswali mengi lakini ndio hivyo ya kuwa Yule nyoka wa shaba alikuwa ni Yesu mwenyewe alikuwapo akitenda kazi lakini kwa kiashiria cha majina mengini kwakuwa muda wa uthihirisho wake kama ilivyo nenwa na manabii ulikuwa bado .
             (Roho mtakatifu kuna kitu anataka ukujue)
Hata ile safina wakati wa nuhu alikuwa ni Yesu mwenyewe na fimbo ya musa hizi zote ni product za miti ambazo zinasimama badala ya msalaba wa Bwana Yesu .alionekana akitenda kazi kwa nguvu sana lakini wengi hawakutambua ya kuwa ni Yesu au ni mwana wa Mungu mwenye uweza wa kifalme aliye tabiriwa (Isaya 9;2-7 ).hili lina thibitishwa pia pale ambapo wale walio msulibisha Bwana Yesu hawakumtambua pia yakuwa ndiye, mpaka pale walipoona nguvu yaajabu siku ya kifo chake juu ya msalaba na hapo ndipo dunia iliposhuhudia nguvu hii ya msalaba wa yesu baada ya kuangikwa na kufa pale msalabani (Mathayo 27;45 – 54) .Ndipo nguvu ya msalaba wa Bwana Yesu ilipo anza kuonekana ikitenda kazi za ajabu .
                                   (usikate tamaa endelea )
Lakini kabla sija kupeleka mbali nataka ujue kitu kimoja kwamba kwadesturi za kiyahudi mtu kufa au kutundikwa msalabani lilikuwa nitendo la laana ,yaani msalabani wali mtundika mtu aliye fanya maasi kama wale wamyang’anyi wawili kumaanisha kuwa huyu mtu amelaaniwa na alifia hapo kifo cha msalabani na ndio maana utaona Yesu siku alipo tundikwa msalabani kuna watu pia ambao nao walionekana ni waharifu kama yeye alivyo onekana kama muharifi walikuwa wametundikwa .lakini chaajabu ambacho napenda ukijue ni hiki Yesu alikuwa hana kosa lolote lakini alitundikwa msalabani sasa swali la kujiuliza kwanini atundikwe wakati hana dhambi au kosa?(2 kor 5;21) yeye asiye jua dhambi alimfanya kuwa dhambi kwaajili yetu ili sisi tupate kuwa haki mbele ya Mungu katika yeye. Pia soma ( waefeso 2;8-9 ) na (warumi 10;9), kuna mambo ya ajabu Mungu anakuambia kwahiyo maandiko yanapo sema alimfanya kuwa dhambi na wakati tuna juana maandiko yametuthibitishia kuwa  hakuwa na dhambi maana yake  pale msalabani ilitakiwa mimi na wewe ndio tutundikwe pale kwasababu ya makosa yetu sasa Yesu akaamua ajifanye kana kwamba yeye ndiye aliye tenda kwalengo la kutuokoa mimi na wewe ingawa ukitaka akuokoe lazima  unyenyekee kama Yule myang’anyi mwingine alivyoonesha unyenyekevu yaani ukubali na kukiri kwa  kinywa chako sawasawa na (warumi 10;9).

Msalaba maana yake mzigo na ndio maana Yesu ana sema atakaye taka kumfuata kwanza aikane nafisi yake  ajitwike msalaba wake na kisha anifiatea ,huo mzigo ndio msalaba maana yake yeye aliamua abebe mzigo kwaajili yetu. Je, wewe una weza kukubali kufugwa Gerezani miaka 30 kwaajili ya mtu  fulani aliye ua ?kama huwezi basi kuna mtu aliye kusaidia sana  kuipunguza na wenda kuiondoa kabisa adhabu uliyo takiwa uipate kwa halali kabisa ingawa hata hautaki kumshukuru na kumfuata,na adhabu aliyo ipata ina maana ilitupasa kabisa kwa kipimo kilekile tuichukue kila mmoja kwa mateso yaleyale mpaka kufa na ndio maana yeye aliamua afe lili kwamba kile kifo kilicho kuwa halali kwa wanadamu akiondoe kwa kufufuka kwake lakini kwakweli upendo wa Mungu katika kristo una nguvu (siku ya mwisho utajibia kwanini hutaki kumuheshimu umekazana na udini na umemwacha Yesu )

 Hebu nasi leo tushuhudie mathayo anaanza kwa kusema Basi tangu saa sita palikuwa na giza juu ya nchi yote hata saa tisa na kama saa tisa yesu akapaza sauti kwa nguvu akisema ,Eloi,Eloi lama sabakthani? Yaani Mungu wangu Mungu wangu mbona umeniacha?maeneo hayo utaono wengi walimdhihaki na kila mtu alisema  lake pasipokujua  ndiposa ukianzia mathayo mstari wa (Math 50 ). hapo biblia inasema,"naye yesu akiisha kupaza sauti tena tena kwa nguvu akaitoa roho yake".ina maana sio kwa kulazimishwa ,lilikuwa nitendo la automatic nguvu kubwa ikatoka pale msalabani na kusambaa dunia nzima ikaanza kuvuja na kuharibu kila utaratibu na vizuizi vilivyo zuia uhuru wetu sisi wanadamu katika kumshuhudia Mungu wetu (Math 51 )inasema.Natazama pazia la hekalu likapasuka vipande viwili toka juu hata chini ingawa watu hawakujua pia maana ya kupasuka lile pazia hata sasa baadhiya watu hawajui labda wanapo soma somo hili ndio wana funguka sasa na mungu awasaidie kujua zaidi ;hili ni pazia ambalo lilikuwa linatenganisha kati ya kuhani na watuwake ambapo aliyepaswa kuingia ndani ni kuhani pekee ili kupeleka shida za watu kwa Mungu kwa hivi watu walitoa shida zao kwa kuhani mkuu ndiposa kuhani pekee alipaswa kuzipeleka kwa Mungu hali ameingia chumba cha ndani kinacho tenganishwa na lile pazia  yaani patakatifu papatakatifu ,kwahivi baada ya kifo cha Bwana Yesu pale msalabani lile pazia likapasuka katikati kumaanisha kua sasa niruksa kwa kila mwanadamu kumwendea Mungu wetu na kuzungumza naye na kujibiwa .

Jambo la pili lililo dhihirika na nchi ikatetemeka;miamba ikapasuka .hii miamba katika ulimwengu wa kiroho ilikuwa ni vizuizi vinavyo rudisha nyuma maisha ya wanadamu lakini kupitia  hii nguvu ya msalaba ndiyo iliyo pasua miamba yote na kuitetemesha nchi vizuizi vika ondoka na ndicho kinacho fanyika hata leo kwa nguvu hii ya msalaba mtakatifui wa Bwana wetu Yesu kristo magonjwa hupona wafu hufufuliwa wachawi wana salenda chini ja nguvu hii ya msalaba kwa maana ndiyo kiboko yao.

 (Math 52) makaburi yakafunuka ikainuka miili mingi ya watakatifu waliolala 53 nao wakiisha kutoka makaburini mwao baada ya kufufuka kwake wakaingia mji mtakatifu wakawatokea wengi, KIUKWELI MSALABA UNA NGUVU NDIYO MAANA UKISOMA (1Kor 1;18 ). INASEMA KWASABA NENOLA MSALABA KWAO WANAOPOTEA NI UPUUZI, BALI KWETUSISI TUNAOOKOLEWA NINGUVU YA MUNGU.
Kupitia nguvu ya msalaba wafu wakafufuka kwaufupi hii ilikuwa ni automatic action katika uso wa dunia sasa swali je,! kutokana na mambo haya machache tu kati ya mengi wale makuhani walinzi na wote walio mdhihaki walifanyanini? (Math 54) mwandishi anaendelea kwa kusema Basi Yule Akida na hao waliokuwa pamoja naye wakimlinda Yesu walipoliona tetemeko la nchi na mambo yaliyo fanyika wakaogopa sana wakisema , Hakika huyu alikuwa mwana wa mungu .

     (  Nguvu ya msalaba na damu ya  Yesu ipo kazini hata sasa )
KUPITIA MANENO HAYA TUNA JIFUNZA IKIWA WALE WALIO MTESA WAKIWA NA MIOYO MIGUMU YA KUAMINI YAKUWA NDIYE KRISTO WANAKUJA KUSHITUKA BAADAYE WAKATI MAMBO YAMESHA HARIBIKA YAANI WAME MPIGA NA KUMDHARIRISHA VYA KUTOSHA YAANI NISAWA NA WEWE UKAMPIGA MZAZI WAKO BILA KUJUA YEYE ANA KUAMBIA MIMI NI MZAZI WAKO LAKINI WEWE UNA MWAMBIA KELELE HALAFU UNAENDELEA HALAFU UKISHA MUUA NDIO UNAKUJA KUSHITUKA KUWA HA! KUMBE ALIKUWA NI MZAZI ,MPENDWA INATUPASA NASI KUTAMBUA MAPEMA KUTUBU NA KUISHI MAISHA YA WOKOVU MAANA TUSIJE PUUZIA HALAFU SIKUIKIFIKA NDIO TUNA TAMBUA MWISHONI KAMAWALE WALINZI TUNAPASWA KUWA MAKINI MAANA MAANDIKO YANASEMA SAA YA WOKOVU NI SASA NA SAA ILIYO KUBALIKA NI SASA WEWE UNAYE SEMA WAKATIWAKO BADO SI KWELI NEEMA YA MUNGU ILISHA MWANGWA KWA NJIA YA MSALABA SUALA NI MAAMUZI TU YA MTU MWENYEWE

NB;kumbuka hata kabla ya kifo chake yesu alipokuwa angalipale msalabani aliweza kutoa hukumu ya haki iliyotokana na kuwepo pale msalabani kwakuwa lengo kuu la kifo chake pale msalabani ilikuwa kuondoa uadui kati ya Mungu na wanadamu uadui ulio dumu kwa muda mrefu ingawa Yesu alikuwepo tangu mwanzo akitenda makuu na ule uadui ulio anza pale bustanii Edeni ilionekana hakuna kipatanishi sahihi cha mwanadamu na dhambi zake kwa Mungu ndiposa kifo cha Yesu msalabani kikatoafidia {kuwaweka huru na kuna huru kweli kweli pia ukisoma (Waefeso 2;16)akawapatanisha wote wawili na Mungu katika mwili mmoja kwa njia ya msalaba akiisha kuufisha ule uadui kwa huo msalaba akaja akahubiri amani kwenu ninyi mliokuwa mbali ,na amani kwao wale walio kuwa karibu kwa maana kwa yeye sisisote tumepata njia ya kumkaribia Baba kwa Roho mmoja. basi tangu sasa ninyi sio wageni wala wapitaji bali ninyi ni wenyeji pamoja na watakatifu ,watu wa nyumbani mwake Mungu mmejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii naye kristo Yesu mwenyewe ni jiwe kuu la pembeni
                 (msalaba wa Yesu una nguvu)
.Mpendwa kifo cha Bwana yesu kimeleta mabadiriko makubwa sana na mengi sana hata amani uliyo nayo nikutokana na nguvu ya msalaba lakini wewe hata kumshukuru mungu unapuuzia iliwa umeelewa vema somo hili fuatisha maneno haya usifuatishe ikiwa bado huja itafakari vizuri nguvu ya msalaba,kama hujaelewa vizuri rudia kusima taratibu inawezekana hujaelewa kwasababu shetani yupo kazini hataki uelewe basi rudia tena kusoma katika roho kama kunakitu umekipata katika somo hili fuatisha maneno haya kwa hali ya utulivu katika roho na usikose kuandika ushuhuda hapo chini kwenye comment ,ili niendelee kukuombea zaidi.Mpendwa kupitia nguvu ya msalaba hatashida zako leo zinaweza kosa nafasi kabisa ndani yako ikiwa umeiaminiu nguvu hiyo ya msalaba fuatisha maneno haya ikiwa umeamini na unahitaji msaada wa nguvu ya msalaba wa Yesu kristo mwana wa Mungu aliye hai haya anza ; BABA MUNGU KAPITIA JINA LA MWANAO YESU KRISTO ALIYE KUFA MSALABANI ILI NGUVU HIYO YA MSALABA ITUPATANISHE NA WEWE MUNGU WETU,NIME SIKIA NENO HILI NAMI NINA KUJA KWAKO MUNGU NI,NATUBU DHAMBI ZANGU ZOTE NAKUOMBA MUNGU WANGU UNISAMEHE KWA DAMU YA YESU KRISTO ILIYO MWAGIKA PALE MSALABANI NGUVU YA MSALABA KUPITIA DAMU YA YESU INITAKASE , E MUNGU WANGU NAKUSIHI KWA ROHO YANGU ULIFUTE JINA LANGU LILILO ANDIKWA KWENYE KITABU CHA HUKUMU NA ULIANDIKE SASA KWENYE KITABU CHA UZIMA CHA WATU WAENDAO MBINGUNI {MJIMTAKATIFU }E BWANA YESU NGUVU YA MSALABA WAKO INIOKOE KAMA ULIVYO YAFUNUA MAKABURI YA WAFU KWANGUVU YA MSALABA WAKO ILIYO TOKA PALE MSALABANI NA KUSAMBAA DUNIA NZIMA NA KUFUFUA WAFU  NA MARA HIYO WAKAINGIA MJI MTAKATIFU NAMI UNIFUFUE ROHO YANGU NA KUNIPA KIBALI CHA KUURITHI UFALME WAKO MBINGUNI ASANTE BWANA YESU KWA KUNISAMEHE NAKUKUBALI KULIANDIKA JINA LANGU KATIKA KITABU CHA UZIMA KUPITIA NGUVU YA MSALABA WAKO BWANA YESU NA DAMU YAKO,PIA NAKUOMBA UHARIBU KILA KIZUIZI KINACHO NIZUIA NISISONGE MBELE KATIKA MAJUKUMU YANGU YAKUPENDEZAYO KILA KIZUIZI KIPASUKE NA KUYEYUKA KWA NGUVU YA MSALABA WAKO BWANA WANGU YESU KRISTO NA NIKALINDWE KWANGUVU YA MSALABA WAKO YESU MAANA SINA MWINGINE ILA NI WEWE TU BWANA NIPE UVUMILIVU UKANIPE HATAYALE NISIYO YAOMBA PIA UMSAIDIE KILA MWENYE SHIDA E BWANA DHIHIRIKA KWAO WAKUTAFUTAO NA WASIO KUJUA NA KUKUTAFUTA WAFUNULIE NURU YA USO WAKO KUPITIA NGUVU YA MSALABA WAKO ASANTE MUNGU KATIKA JINA LA YESU KRISTO ALIYE NIFILIA MSALABANI AMEN .SOMO HILI LITAENDELE LAKINI WEWE ANZA KULIFANYIA KAZI HAUTA KUWA HIVYO KAMA ULIVYO NGUVU YA MSALABA ITAENDELEA KUDHIHIRIKA KWAKO 
NGUVU YA MSALABA
Linaweza kuendelea muda wowote maana Mungu ni mwaminifu.lakini endelea tu kupitia blog hii utakutana na mengikama vile shuhuda mbalimbali nk                        
                                 Limeandaliwa  na E.mkinga

                        KISIMA CHA BARAKA


             Kisimachabaraka.blogspots.com