Tuesday, 17 October 2017

HAKUNA KITU KIZURI NA KIBAYA KAMA NDOA,

Tags

        

    HAKUNA KITU KIZURI NA KIBAYA KAMA NDOA,
                        
                     (huu ni muhutasari tu)
                                                  




Najua unazo tafsiri zako juu ya ndoa lakini,dhana yangu na Maelezo haya machache yatajikita kuzungumzia zaidi maisha ya ndoa( maisha ya ndoa)kwasababu maisha yake ndiyo yanayo zaa mjadala.na sio tafsiri kama wengine wanavyo tafsiri

Ndoa, ni aina ya maisha yanayohusu jinsia mbili tofauti  ,kwa kibali au idhini ya kanisa au serikali.watu hao wawili wanapo kubaliana kwaidhini hiyo wanakuwa na uhalali wa kuishi pamoja kama mume na mke wakizaa watoto na kwenda mbinguni,

Mpendwa wangu,moja kwa moja nianze kukuonesha vitu vichache juu ya mtazamo wa kichwa cha hapo juu maarufu kama  HAKUNA KITU KIZURI NA KIBAYA KAMA NDOA ,hii ni kutokana na watu wengi kuona na kusema kuwa ndoa ni mbaya na wengine wakisema kuwa ndoa ni nzuri lakini leo nataka nikupe suruhisho la mjadala huu.kwa kuorodhesha tu baadhi ya uzuri na ubaya wa ndoa kisha nitasuruhisha,mwishoni

                                  FAIDA ZA NDOA

Humwezesha mwanandoa kuishi maisha ya amani  na yaliyo jaa ushindi mkuu dhidi ya dhambi ya uzinzi.hii ni kwasababu maandiko matakatifu yana idhinisha kuoa kuliko kuwakwa tama mpendwa, kimsingi ikiwa huja oa ina maana utawatamani wale ambao sio wakezako bali ni wake za watu au wajane au wasio olewa  au wanaume za watu  ,kwasababu kutamani mwanamkeau mume  asiyo wako ni kosa (1petro 2;14) ,(1Kor 6;9)

Ndoa inasaidia kusudi la Mungu kutimia,lengo  mojawapo laMungu kumuumba mwanadamu lilikuwa ni kuitunza nchi ambayo imeumbwa na ndio maana mwanadamu aliambiwa akailime na kuitunza hiyo nchi na kitendo cha kuruhusu kuzaliana ni kutokana na ukubwa wa dunia na rasilimali zilizopo juu ya  kazi ya kutunza uumbaji inavyo hitaji watu wa kutosha   Mwanzo 9;7) ,(Mwanzo 1;27),wakaambiwa zaeni mkaongezeke  mkaijaze nchi na kuitiisha,soma hizo aya utaona mambo ya siri sana ambayo Mungu alikusudia

Ndoa ina weza kusaidia kukuza kipato cha familia ,hii ni kutokana na mshikanano na kusaidiana katika mawazo bunifu ya kimaendeleo baina ya wanandoa wenyewe .

                                HASARA ZA NDOA

          Simaanishi haifai au usifikiri kuwa nakukatisha tamaa ya kuoa au kuolewa  hapana bali nataka ujue unapo taka kuoa au kolewa uwe umejindaa vizuri ili kuepuka maneno machafu yanayo chafua kituchema kilicho andaliwa na Mungu (ndoa)

  • Ina weza kumsababisha mtu akawa na majuto na stress nyingi,hii hutokana na migogoro katika ndoa hiyo ,ingawa migogoro hii inawezekana kabisa kuisha na wanandoa wakaishi kama  paradiso

  • Inaweza kumkatisha mtu tama ya maisha

  • Ina weza kumtengenezea mtu maumivu ndani ya nafsi yake

  • Inaweza kumpotezea mtu muda mwingi wakufanya mambo mengine kama kumtafuta Mungu nk,hii ni pale ndoa inapokuwa na migogoro isiyo eleweka ambayo ina mpamtu ulazima wa kuyafikiri hayo kuliko mengine ya   msingi zaidi

NB;Kwa asili ndoa ni njema ni nzuri kabisa lakini chanzo kinacho sababisha ndoa ionekane kuwa mbaya na wanadamu wenyewe andiko hili linadhihirisha kuwa ndoa ninjema ,kwasababu Mungu anapo umba kitu huwa hakosea vyote anaviumba kwa nia njema lakini watumiaji hutumia bilakujua utaratibunamna wa kukitumia kituhicho sawasawa na mapenzi ya Mungu (Mwanzo 1;31)

    MAMBO YA KUZINGATIA UKIWA NDANI YA NDOA        (MWANANDOA),AU KABLA YA KUOA AU KUOLEWA


Hapa ninachanganya zote lakini zitakufaa zote

  • Jiulize huyo unaye taka kuoana naye ,umempendea nii ,hii inasadia kudumisha uimara wa ndoa ,mfano ukimpendea uzuri wa rangi yake tu inamaana sikumoja akipata tatizo litakalo sababisha sura yake kuharibika itakuwa vigumu kumpenda au ukimpendea utajiri inamaana kuwa akifirisika basi na ndoa lazima ita firisika (kuvunjika),lakini ukimpenda kwa jinsi alivuo na atakavyo kuwa ndoa itadumu kwani ikiwa unampendwa jinsi alivyo upendo wako unanguvu ya kumbadirisha iwapo utajua kuutumia upendo kwa mabaririko na uimara wa ndoa yako

  • Mwombe Mungu akuoneshe chaguo sahihi, (kwa wasio oa au kuolewa ),mpendwa suala la kumwomba Mungu watu wengi huwa wanalipiga wanasema inatakiwa utumie akilizako kuchagua mke au mume sasa nikuachie wewe swali ,je,unataka kutumia akili zako katika kumtafuta mwenzi wako kwaajili ya ndoa kwani wewendiye uliye anzisha ndoa?utajijibu mwenyewe watu wengi wanaishia kwenye uchumba kwasababu hawamuulizi mwanzilishi wa ndoa kuwa ninani anafaa kuwa na mimi,kumbuka Adamu aliletewa mke sasa wewe unataka umchukue mke .unauhakika hapounapochukua ndio penyewe panapopatikana mwenzi wako,angalia usije ukachukua kiumbe kingine ,uliza kwanza wakwako mahali alipowekwa kazi yako nikwenda kumchukua sio kumtafuta unamtafuta kwani amepotea? haina shida ukitaka kuchukua wewe chukua tu utakacho kipata baadaye usinipigie simu,ikiwa unakubaliana na wazo hili kumbuka kuandika ndio hapo chini

  • Andaa akili zako na moyo wako kukubaliana na misukosuko au changamoto au utofauti utakao jitokeza wakati wa ndoa ,hii ni kwasababu hata kama lilikuwa ni kusudi la Mungu kuoana na mtu huyo lakini kumbuka yeye ni mwanadamu ana mapungufu yake kwahiyo jiandae

  • Uwe mvumilivu na msikivu juu ya ushauri anao utoa mwenzako

  • Usi mwone mwenzako kama chanzo cha matatizo bali chanzo cha baraka ,bali onya neni kwa upole na upendo wa agape

  • Unyenyekevu kwa mwanamke nijambo muhimu sana na ndilo linalo wateka wanaume wengi kuwapenda zaidi na kuwajali wake zao (Mithali 9;13)na (Mithali 31;11-12)

  • Mwana ume tambua kuwa huyo ni mwanamke usitake kumshurutisha mithili ya mwanaume kwasababu atabaki kuwa mwanamke akiwa na homin zake za kike na ndizo zinazo mfanya hatakama amesoma sana lakini kuna mambo atayafanya kama mwanamke ,na ndio maana wengi wao lazima wainuliwe kwasababu uwezo wa kujiinua nimdogo wanawake msiishangae hoja hii lakini usipojali utauona ukweli ndaniyake ukikosea hapo lazima mtagombana

  • Mwanamke mheshimu mumeo hatakama ni mdogo kwa umbile kwako au hana uwezo mkubwa wa kutafuta kipato mweshimu au hana  elimu kaqma wewe mweshimu ,wanawake wengi wakigundua wakojuu wanaanza dharau ,huu ni ushauri wa bure kwani maumivu ya nafsi utawapata wewe sio wanao kuonya ,kupitia heshima yako ndio dawa ya kumfanya awe mtu mzuri kwako,ukijifanya wewe kuwa bamsa huwezi kuolewa kirahisi na kamaumeolewa lazima mtagombana sana

  • Kuweni makini kwakutunza siri zenu za ndani hii ni kwasababu kuna baadhi ya mambo mkiyatoa nje yanaporudi ndani yanarudi yakiwa yamebeba maumivu misumali miba nk

  • Kila mmoja na awe mtii kwamwenzake (1Kor 7;4-5)

NB;Kuishi vizuri inawezekana ikiwa kila mmoja amesimama kwenye nafasi yake kwa upendo mkuu (2kor 2;14)

  • Kijana au vijana kuweni waangarifu msivutwe na mambo ya dunia,kwasababu yanapelekea mtu anapotaka kuoa au kuolewa anakuwa anavitu ambavyo vinawahusu wanandoa wakati yeye bado sio mwana ndoa mfano ;kuwa na mimba kabla ya ndoa ,kuzaa kabla ya ndoa hatakama utaolewa lakini umesha sababisha doa au mtu akipata magonjwa ya zinaa wakati sio mwana ndoa yaani anabeba mzigo usio muhusu,acha kuwabebea watu vifurushi usivyojua kikichomondani yake.

NB;ukikurupuka wakati wa kuoa au kuolewa unaweza kujutia wakati wa ndoa

  • Pia ikiwa umepanga kuishi bila kuoa au kuolewa ,ni marufuku kuingia kwenye uzinzi (usiwakwe tama maana kutamani mke  au mume asiye  wako ni kosa, (Mathayo 5:27-28) neno la Mungu linasema “mmesikia kwamba imenenwa,usizini,lakini mimi nawaambia kila mtuatazamaye mwanamke kwa kumtamani amekwisha kuzini naye moyoni mwake,pia soma  (1kor 6;8-9) na (1Kor 7;1-3).je umeifurahia makala hii na imekusaidia,na ina manufaa kwako?
NB;ubaya wa ndoa unakuja pale wanandoa wanapo gombana na kutokupata suruhisho,hapo ndipo wengi wanapoona kuwa ndoa ni mbaya kwasababu ya makosa yao kwani muda mwingine kunapotokea tatizo niwepesi kuomba msaada kwa washauri wakati dawa halisi wanayo wao wenyewe wakikaa pamoja kwa upendo na hekima ili kujadiri juu ya utofauti ulio jitokeza,hii ni muhimu kwani chanzo halisi cha migiogoro ya ndoa wanandoa wenyewe wanaijua,kwnai umewahi kusikia Ibrahimu na Sara waliwai kwenda kuomba ushauri wa ndoa yao ,au ndoa ya Yusuph na Mariam,uliwai sikia wamegombana na wakaenda kuomba ushauri nyie mnatatizo gani?
                
                               Imeandaliwa na  E.mkinga.

                                                  kisimachabaraka.blospot.com

                  kumbuka ku sharea  katika makundi mbalimbali ya watsapp/facebook twitter kila unacho kisoma kutoka blog hii , 


EmoticonEmoticon