Thursday, 19 October 2017

MASWALI MBALI MBALI YAHUSUYO IMANI HALISI YA KIKRISTO

Tags

   

 MASWALIO YA KIIMANI YATOKANAYO NA BIBLIA




                                                  

1.   Kwanini Mungu ali mruhusu Ibrahimu kumtoa mwanaye wapekee kama sadaka ya kuteketezwa ?
Jibu;   Kwasababu Mungu alitaka aijaribu imani ya  Ibrahimu  juu ya Mungu aliye hai kama nithabiti nndio maana akahesabiwa haki kwa imani yake kuwa thabiti  (Mwanzo 22;16) (Ebrania 11;8-9)

2.    Kwanini Mungu aliamua kugairi Isaka asitolewe sadaka ya kuteketenzwa nabadala yake  akamtwaa mnyamaa katika kichaka kwaajili ya sadaka ?

Jibu;  Kwasababu Isaka alikuwa mtoto wa agano kati ya Ibrahimu na Mungu  ya kwamba kupitia Isaka Ibrahimju atakuwa na watoto wengi kama mchanga wa Baharini na kama Nyota wa angani na Mungu hawezi kuvunja agano lake (Mwanzo 22;17)

3.   Kwanini Mungu hakuamua kufanya sadaka ya Isaka kuteketezwa kuwa kama fidia ya dhambi za wanadamu dunia nzima ?

Jibu; Kwasababu Isaka hakuamua mwenyewe kuwa sadaka kwa ulimwengu na kufa kwaajili ya watu,kwakuwa sadaka ya ukombozi wa ulimwengu haikuhitaji mtu kuteseka tuu  bali ilihitaji mtu aliye amua kwa dhati kujitoa kwaajili ya kuteseka kwaajili ya watu  hivyo ilihitaji mtu aliye na shahuku  na aliye amua kujitoa sadaka bila manung’uniko  ndio maana baada ya kuona hakuna mwanadamu anaye weza Mungu akaamua kushuka mwenyewe kwa njia ya kujifanya kama mwanadamu wakawaida (Yesu kristo)

4.   Je inatupasa kumuheshimu ibrahimu?

Jibu ;   Ndiyo  Kwasababu yeye ni Baba wa imani aliye tufundisha juu ya imani thabiti ya Mungu halisi .Pia pia  kwasababu ni wazao wake kama alivyo ahidiwa kuwa atakuwa na watoto wengi kama mchanga wa baharini na  Nyota za angani(yeye ni Baba yetu wa imani)ingawa hapaswi kuheshimiwa zaidi ya Mungu   (Mwanzo 22;16) (Ebrania 11;8-9).

    Yataendelea; endelea kupitia tu kila siku

                                               E.mkinga



NB;share na wenzako nao wapate ujumbe.


                
             WatsApp  Twitter   Facebook   Instagram  
                                     

                                     KISIMA CHA BARAKA
                                  Kisimachabaraka.blogspot.com



EmoticonEmoticon