IJUE NGUVU YA MAAJABU ILIYOJIFICHA KATIKA MSALABA WA YESU KRISTO MWANA WA MUNGU ALIYE HAI.
Be blessed in the name of the Father the son and the Holy spirity.Amen
AHSANTE KWA KUENDELEA KUPITIA NA KUSUBIRI SOMO LIMESHA WEKWA WAALIKE NA WENGINE NA UNARUHUSIWA KUTOA COMMENT HAPO CHINI AU KUSHUHUDIA JUU YA ULIVYO PATA MSAADA KUPITIA SOMO HILI ILI NIENDELEE KUKUOMBEA NA MUNGU AKUBARIKI ENDELEA KULISOMA TARATIBU KATIKA ROHO MTAKATIFU AMEN
TAMBUA NGUVU YA MSALABA WA YESU
( soma katika Roho kwa kuhitaji msaada )
Mpendwa hii ndiyo mada niliyo kuahidi kwamba
nitakuletea yenye maelezo machache yenye
nguvu juu ya nguvu iliyo jificha kataka msalaba wa Yesu kristo.karibu twende
pamoja.katika Roho mtakatifu
Muda huu nataka tuweza jifunza na kujua nguvu inayopatikana msalabani kwa Bwana yesu,.kimsingi neno msalaba lilianza kusikika sana baada ya kifo na ufufuko wa yesu ndipo siri ya msalaba ilipoanza kufichuka kwa kasi ,ingawa nguvu ya utendaji wa msalaba wa yesu kimsingi ulikuwako tangu kuwekwa misingi ya dunia lakini kutokana na nyakati na majira ya utendaji wa Mungu nguvu hii ya msalaba ilidhihirika zaidi wakatiwake maalum ulupofika wa kuzaliwa kufa na kufufuka kwa Bwana wetu yesu kristo .
( endelea kusoma katika Roho kwa kuhitaji msaada )
Mpendwa kabla ya ujio wa yesu kwa njia ya kuzaliwa kupitia
mwanadamu tunaona kuwa Yesu alikuwepolakini staili ya kuja duniani Mungu akaona
niafadhari aonekane kama mwana damu iliwasiogope hata kutembea naye na aliendelea
kutenda kazi lakini wanadamu hawakujua ya kuwa ndio yesu mwenyewe maana wakati
wa udhihirisho wake ulikuwa bado lakini utendaji kazi wake ulisha kuwepo utendaji
huu tuna uthibitisha kwenye kitabu cha {hesabu 21-4-9 } maandiko yanasema “wakasafiri kutoka mlima wa Hori kwa njia
ya bahariya shamu ilikuizunguka nchi ya Edom watu wakafa moyo kwasababu ya ile
njia 5 watu wakamnung’unikia Mungu na Musa ,mbona mmetupandisha huku?kutoka
nchi ya misri ,ilitufe jangwani? Maana hapana chakula wala hapana maji na roho
zetu zina kinai chakula hiki dhaifu 6 Bwana akatuma nyoka za moto kati ya watu
,wakawauma watu wakafa7 watu wakamwendea musa wakasema tumafanya dhambi
kwasababu tume mnung’unikia mungu na wewe utuombee kwa Bwana atuondolee nyoka
hawa .basi musa akawaombea watu .8 Bwana akamwambia musa ,jifanyie nyoka wa
shaba ukaiweke juu ya mti na itakuwa kila mtu aliye umwa aitazamapo ataishi .9
Musa akafanya nyoka wa shaba ,akaiweka juu ya mti hataikiwa nyoka amemwuma mtu
alipoitazama ile nyoka wa shaba akaishi . Mpendwa haya ni mambo ya rohoni
ambayo kwakawaida unaweza jiuliza maswali mengi lakini ndio hivyo ya kuwa Yule
nyoka wa shaba alikuwa ni Yesu mwenyewe alikuwapo akitenda kazi lakini kwa
kiashiria cha majina mengini kwakuwa muda wa uthihirisho wake kama ilivyo nenwa
na manabii ulikuwa bado .
(Roho mtakatifu kuna kitu anataka ukujue)
Hata ile safina wakati wa nuhu alikuwa ni Yesu mwenyewe na
fimbo ya musa hizi zote ni product za miti ambazo zinasimama badala ya msalaba
wa Bwana Yesu .alionekana akitenda kazi kwa nguvu sana lakini wengi hawakutambua
ya kuwa ni Yesu au ni mwana wa Mungu mwenye uweza wa kifalme aliye tabiriwa (Isaya
9;2-7 ).hili lina thibitishwa pia pale ambapo wale walio msulibisha Bwana Yesu
hawakumtambua pia yakuwa ndiye, mpaka pale walipoona nguvu yaajabu siku ya kifo
chake juu ya msalaba na hapo ndipo dunia iliposhuhudia nguvu hii ya msalaba wa
yesu baada ya kuangikwa na kufa pale msalabani (Mathayo 27;45 – 54) .Ndipo nguvu
ya msalaba wa Bwana Yesu ilipo anza kuonekana ikitenda kazi za ajabu .
(usikate tamaa endelea )
Lakini kabla sija kupeleka mbali nataka ujue kitu kimoja
kwamba kwadesturi za kiyahudi mtu kufa au kutundikwa msalabani lilikuwa nitendo
la laana ,yaani msalabani wali mtundika mtu aliye fanya maasi kama wale wamyang’anyi
wawili kumaanisha kuwa huyu mtu amelaaniwa na alifia hapo kifo cha msalabani na
ndio maana utaona Yesu siku alipo tundikwa msalabani kuna watu pia ambao nao
walionekana ni waharifu kama yeye alivyo onekana kama muharifi walikuwa
wametundikwa .lakini chaajabu ambacho napenda ukijue ni hiki Yesu alikuwa hana
kosa lolote lakini alitundikwa msalabani sasa swali la kujiuliza kwanini
atundikwe wakati hana dhambi au kosa?(2 kor 5;21) yeye asiye jua dhambi alimfanya kuwa dhambi kwaajili yetu ili sisi
tupate kuwa haki mbele ya Mungu katika yeye. Pia soma ( waefeso 2;8-9 ) na (warumi
10;9), kuna mambo ya ajabu Mungu anakuambia kwahiyo maandiko yanapo sema
alimfanya kuwa dhambi na wakati tuna juana maandiko yametuthibitishia kuwa hakuwa na dhambi maana yake pale msalabani ilitakiwa mimi na wewe ndio
tutundikwe pale kwasababu ya makosa yetu sasa Yesu akaamua ajifanye kana kwamba
yeye ndiye aliye tenda kwalengo la kutuokoa mimi na wewe ingawa ukitaka akuokoe
lazima unyenyekee kama Yule myang’anyi
mwingine alivyoonesha unyenyekevu yaani ukubali na kukiri kwa kinywa chako sawasawa na (warumi 10;9).
Msalaba maana yake mzigo na ndio maana Yesu ana sema atakaye
taka kumfuata kwanza aikane nafisi yake
ajitwike msalaba wake na kisha anifiatea ,huo mzigo ndio msalaba maana
yake yeye aliamua abebe mzigo kwaajili yetu. Je, wewe una weza kukubali kufugwa
Gerezani miaka 30 kwaajili ya mtu fulani
aliye ua ?kama huwezi basi kuna mtu aliye kusaidia sana kuipunguza na wenda kuiondoa kabisa adhabu
uliyo takiwa uipate kwa halali kabisa ingawa hata hautaki kumshukuru na
kumfuata,na adhabu aliyo ipata ina maana ilitupasa kabisa kwa kipimo kilekile
tuichukue kila mmoja kwa mateso yaleyale mpaka kufa na ndio maana yeye aliamua
afe lili kwamba kile kifo kilicho kuwa halali kwa wanadamu akiondoe kwa
kufufuka kwake lakini kwakweli upendo wa Mungu katika kristo una nguvu (siku ya
mwisho utajibia kwanini hutaki kumuheshimu umekazana na udini na umemwacha Yesu
)
Hebu nasi leo
tushuhudie mathayo anaanza kwa kusema Basi tangu saa sita palikuwa na giza juu
ya nchi yote hata saa tisa na kama saa tisa yesu akapaza sauti kwa nguvu
akisema ,Eloi,Eloi lama sabakthani?
Yaani Mungu wangu Mungu wangu mbona umeniacha?maeneo hayo utaono wengi
walimdhihaki na kila mtu alisema lake
pasipokujua ndiposa ukianzia mathayo
mstari wa (Math 50 ). hapo biblia inasema,"naye
yesu akiisha kupaza sauti tena tena kwa nguvu akaitoa roho yake".ina maana
sio kwa kulazimishwa ,lilikuwa nitendo la automatic nguvu kubwa ikatoka pale
msalabani na kusambaa dunia nzima ikaanza kuvuja na kuharibu kila utaratibu na
vizuizi vilivyo zuia uhuru wetu sisi wanadamu katika kumshuhudia Mungu wetu (Math
51 )inasema.Natazama pazia la hekalu
likapasuka vipande viwili toka juu hata chini ingawa watu hawakujua pia
maana ya kupasuka lile pazia hata sasa baadhiya watu hawajui labda wanapo soma
somo hili ndio wana funguka sasa na mungu awasaidie kujua zaidi ;hili ni pazia
ambalo lilikuwa linatenganisha kati ya kuhani na watuwake ambapo aliyepaswa
kuingia ndani ni kuhani pekee ili kupeleka shida za watu kwa Mungu kwa hivi
watu walitoa shida zao kwa kuhani mkuu ndiposa kuhani pekee alipaswa kuzipeleka
kwa Mungu hali ameingia chumba cha ndani kinacho tenganishwa na lile pazia yaani patakatifu papatakatifu ,kwahivi baada
ya kifo cha Bwana Yesu pale msalabani lile pazia likapasuka katikati kumaanisha
kua sasa niruksa kwa kila mwanadamu kumwendea Mungu wetu na kuzungumza naye na
kujibiwa .
Jambo la pili lililo dhihirika na nchi ikatetemeka;miamba ikapasuka .hii miamba katika ulimwengu
wa kiroho ilikuwa ni vizuizi vinavyo rudisha nyuma maisha ya wanadamu lakini
kupitia hii nguvu ya msalaba ndiyo iliyo
pasua miamba yote na kuitetemesha nchi vizuizi vika ondoka na ndicho kinacho
fanyika hata leo kwa nguvu hii ya msalaba mtakatifui wa Bwana wetu Yesu kristo magonjwa
hupona wafu hufufuliwa wachawi wana salenda chini ja nguvu hii ya msalaba kwa
maana ndiyo kiboko yao.
(Math 52) makaburi
yakafunuka ikainuka miili mingi ya watakatifu waliolala 53 nao wakiisha kutoka
makaburini mwao baada ya kufufuka kwake wakaingia mji mtakatifu wakawatokea wengi,
KIUKWELI MSALABA UNA NGUVU NDIYO MAANA UKISOMA (1Kor 1;18 ). INASEMA
KWASABA NENOLA MSALABA KWAO WANAOPOTEA NI UPUUZI, BALI KWETUSISI TUNAOOKOLEWA
NINGUVU YA MUNGU.
Kupitia
nguvu ya msalaba wafu wakafufuka kwaufupi hii ilikuwa ni automatic action katika
uso wa dunia sasa swali je,! kutokana na mambo haya machache tu kati ya mengi
wale makuhani walinzi na wote walio mdhihaki walifanyanini? (Math 54) mwandishi
anaendelea kwa kusema Basi Yule Akida na hao waliokuwa pamoja naye wakimlinda Yesu
walipoliona tetemeko la nchi na mambo yaliyo fanyika wakaogopa sana wakisema ,
Hakika huyu alikuwa mwana wa mungu .
( Nguvu ya msalaba na damu ya Yesu ipo kazini hata sasa )
KUPITIA
MANENO HAYA TUNA JIFUNZA IKIWA WALE WALIO MTESA WAKIWA NA MIOYO MIGUMU YA
KUAMINI YAKUWA NDIYE KRISTO WANAKUJA KUSHITUKA BAADAYE WAKATI MAMBO YAMESHA
HARIBIKA YAANI WAME MPIGA NA KUMDHARIRISHA VYA KUTOSHA YAANI NISAWA NA WEWE
UKAMPIGA MZAZI WAKO BILA KUJUA YEYE ANA KUAMBIA MIMI NI MZAZI WAKO LAKINI WEWE
UNA MWAMBIA KELELE HALAFU UNAENDELEA HALAFU UKISHA MUUA NDIO UNAKUJA KUSHITUKA
KUWA HA! KUMBE ALIKUWA NI MZAZI ,MPENDWA INATUPASA NASI KUTAMBUA MAPEMA KUTUBU
NA KUISHI MAISHA YA WOKOVU MAANA TUSIJE PUUZIA HALAFU SIKUIKIFIKA NDIO TUNA
TAMBUA MWISHONI KAMAWALE WALINZI TUNAPASWA KUWA MAKINI MAANA MAANDIKO YANASEMA
SAA YA WOKOVU NI SASA NA SAA ILIYO KUBALIKA NI SASA WEWE UNAYE SEMA WAKATIWAKO
BADO SI KWELI NEEMA YA MUNGU ILISHA MWANGWA KWA NJIA YA MSALABA SUALA NI
MAAMUZI TU YA MTU MWENYEWE
NB;kumbuka
hata kabla ya kifo chake yesu alipokuwa angalipale msalabani aliweza kutoa
hukumu ya haki iliyotokana na kuwepo pale msalabani kwakuwa lengo kuu la kifo
chake pale msalabani ilikuwa kuondoa uadui kati ya Mungu na wanadamu uadui ulio
dumu kwa muda mrefu ingawa Yesu alikuwepo tangu mwanzo akitenda makuu na ule
uadui ulio anza pale bustanii Edeni ilionekana hakuna kipatanishi sahihi cha
mwanadamu na dhambi zake kwa Mungu ndiposa kifo cha Yesu msalabani kikatoafidia
{kuwaweka huru na kuna huru kweli kweli pia ukisoma (Waefeso 2;16) “akawapatanisha wote wawili na Mungu katika
mwili mmoja kwa njia ya msalaba akiisha kuufisha ule uadui kwa huo msalaba
akaja akahubiri amani kwenu ninyi mliokuwa mbali ,na amani kwao wale walio kuwa
karibu kwa maana kwa yeye sisisote tumepata njia ya kumkaribia Baba kwa Roho
mmoja. basi tangu sasa ninyi sio wageni wala wapitaji bali ninyi ni wenyeji
pamoja na watakatifu ,watu wa nyumbani mwake Mungu mmejengwa juu ya msingi wa
mitume na manabii naye kristo Yesu mwenyewe ni jiwe kuu la pembeni
(msalaba wa Yesu una nguvu)
.Mpendwa
kifo cha Bwana yesu kimeleta mabadiriko makubwa sana na mengi sana hata amani
uliyo nayo nikutokana na nguvu ya msalaba lakini wewe hata kumshukuru mungu
unapuuzia iliwa umeelewa vema somo hili fuatisha maneno haya usifuatishe ikiwa
bado huja itafakari vizuri nguvu ya msalaba,kama hujaelewa vizuri rudia kusima
taratibu inawezekana hujaelewa kwasababu shetani yupo kazini hataki uelewe basi
rudia tena kusoma katika roho kama kunakitu umekipata katika somo hili fuatisha
maneno haya kwa hali ya utulivu katika roho na usikose kuandika ushuhuda hapo
chini kwenye comment ,ili niendelee kukuombea zaidi.Mpendwa kupitia nguvu ya
msalaba hatashida zako leo zinaweza kosa nafasi kabisa ndani yako ikiwa
umeiaminiu nguvu hiyo ya msalaba fuatisha maneno haya ikiwa umeamini na
unahitaji msaada wa nguvu ya msalaba wa Yesu kristo mwana wa Mungu aliye hai
haya anza ; BABA MUNGU KAPITIA JINA LA MWANAO YESU KRISTO ALIYE KUFA MSALABANI
ILI NGUVU HIYO YA MSALABA ITUPATANISHE NA WEWE MUNGU WETU,NIME SIKIA NENO HILI
NAMI NINA KUJA KWAKO MUNGU NI,NATUBU DHAMBI ZANGU ZOTE NAKUOMBA MUNGU WANGU
UNISAMEHE KWA DAMU YA YESU KRISTO ILIYO MWAGIKA PALE MSALABANI NGUVU YA MSALABA
KUPITIA DAMU YA YESU INITAKASE , E MUNGU WANGU NAKUSIHI KWA ROHO YANGU ULIFUTE
JINA LANGU LILILO ANDIKWA KWENYE KITABU CHA HUKUMU NA ULIANDIKE SASA KWENYE
KITABU CHA UZIMA CHA WATU WAENDAO MBINGUNI {MJIMTAKATIFU }E BWANA YESU NGUVU YA
MSALABA WAKO INIOKOE KAMA ULIVYO YAFUNUA MAKABURI YA WAFU KWANGUVU YA MSALABA
WAKO ILIYO TOKA PALE MSALABANI NA KUSAMBAA DUNIA NZIMA NA KUFUFUA WAFU NA MARA HIYO WAKAINGIA MJI MTAKATIFU NAMI
UNIFUFUE ROHO YANGU NA KUNIPA KIBALI CHA KUURITHI UFALME WAKO MBINGUNI ASANTE
BWANA YESU KWA KUNISAMEHE NAKUKUBALI KULIANDIKA JINA LANGU KATIKA KITABU CHA
UZIMA KUPITIA NGUVU YA MSALABA WAKO BWANA YESU NA DAMU YAKO,PIA NAKUOMBA
UHARIBU KILA KIZUIZI KINACHO NIZUIA NISISONGE MBELE KATIKA MAJUKUMU YANGU
YAKUPENDEZAYO KILA KIZUIZI KIPASUKE NA KUYEYUKA KWA NGUVU YA MSALABA WAKO BWANA
WANGU YESU KRISTO NA NIKALINDWE KWANGUVU YA MSALABA WAKO YESU MAANA SINA
MWINGINE ILA NI WEWE TU BWANA NIPE UVUMILIVU UKANIPE HATAYALE NISIYO YAOMBA PIA
UMSAIDIE KILA MWENYE SHIDA E BWANA DHIHIRIKA KWAO WAKUTAFUTAO NA WASIO KUJUA NA
KUKUTAFUTA WAFUNULIE NURU YA USO WAKO KUPITIA NGUVU YA MSALABA WAKO ASANTE
MUNGU KATIKA JINA LA YESU KRISTO ALIYE NIFILIA MSALABANI AMEN .SOMO HILI
LITAENDELE LAKINI WEWE ANZA KULIFANYIA KAZI HAUTA KUWA HIVYO KAMA ULIVYO NGUVU
YA MSALABA ITAENDELEA KUDHIHIRIKA KWAKO
NGUVU
YA MSALABA
Linaweza kuendelea muda wowote maana Mungu ni mwaminifu.lakini endelea tu kupitia blog hii utakutana na mengikama vile shuhuda mbalimbali nk
Limeandaliwa na E.mkinga
KISIMA CHA BARAKA
EmoticonEmoticon