Monday, 6 November 2017

SAA YA WOKOVU NI SASA/SIKU YA KUOKOKA NI LEO.

Tags

   
SAA YA WOKOVU NI SASA /SIKU YA KUOKOKA NI LEO.
                                            
                                                  
1.   SAA YA WOKOVU NI SASA/ SIKU YA KUOKOKA NI LEO.  
                      
 Mpendwa katika kristo Yesu, nimeamua tujifunze juu ya suala hili maana  wengi wanajiuliza kwamba. Kuokoka ni lazima? wengine wanatumia andiko la (Mt 24:13) wakisema yakuwa wokovu sio leo, bali mpaka  siku ya mwisho wanadai kuwa "hauwezi kusema upo ng’ambo ya mto wakati bado hauja vuka" (yaani wanachanganya mambo ya ki-imani na ushindi wa mwilini yaani wa kidunia. wanafikiri Mbinguni ni mji wa mwilini, kumbe ni mji wa kiroho, ulio halisi, unao onekana kwa imani na imani hiyo ndiyo inayo mpelekea mtu kuufikia ule mji), kauli hii ndiyo wengi wana itumia wakidhani wako sahihi, kumbe wanaitafsiri tofauti, hawa jui ya kuwa katika Biblia kuna maneno yanayo wahusu wale wanaotembea katika njia za Bwana (Mungu), na kuna maneno yanayo wahusu wale walio potea au ambao hawana jitihada za kuutafuta utakatifu, yaani ambao kushinda kwao ni vigumu labla mpaka mganga wakipepo atabiri au ujanja ujanja wa ibilisi utumike, sasa watu wanashindwa kuangalia ninenogani lilizungumzwa katika mazingira gani na niwatu wa aina gani walikuwa wana ambiwa (maandiko yanasema neno lina weza kuua na pia neno lina weza huhuisha ).

Mtu wa Mungu, tambua wakati fulani, kuna vifungu vingine unaweza ukavimeza huku ukifikiri vina kuhusu na kumbe havi kuhusu, kwa wakati ule, yaani wakati wake kwako bado, sasa ngoja nikupe vipande vichache ili uki puuzia yatakayo kupata mimi simo, (maana kwa kweli watu wana shangaza sijui wokovu unawa athiri kivipi), ngoja nikuulize. Je, wokovu unapinga nini na
unaruhusu nini? na wewe unapinga nini  na unaruhusu nini? Na Yesu alipinga nini na uliruhusu nini?, yaani ni mambo gani aliyo waagiza mitume wake waendele kuwaeleza mataifa?

Kwanza nianze kwa kukumbushana kwa habari za kufika mbinguni, ifahamike kuwa hizi ni habari za kiimani ambazo mwanadamu anaye hijitaji kufika huko lazima aamini ya kuwa mbinguni ni sehemu halisi tunayoiendea lakini sehemu hii ina namna yake ya kufika pale, (mbinguni).

Mtu yeyote anapo tazamia kufika mahali fulani jambo la kwanza ni lazima maandalizi ya safari ya fanyike, pia ina mpasa ajue aina ya usafiri atakao utumia, kwa mfano; Ikiwa atatumia usafiri wa ndege ni lazima awe na paspoti, na ikiwa ni kwa gari nilazima awe na tiketi, na kila sehemu ina ainayake ya tiketi (kibali) na aina ya maandalizi ya safari pia ni tofaut. Mfano; anaye toka Kenya kuelekea MwanzaTanzania maandalizi ni tofauti na Yule anaye fanya maandalizi ya safari ya kutoka MwanzaTanzania  kwenda Tabora Tanzania, je nina maana gani?, huwenzi kusema nitafika Mwanza wakati hata safari huja ianza na hata Tiketi huna je utafika Mwanza? NA NDIO MAANA NINA KWAMBIA YAKUWA SAA YA WOKOVU NI SASA.

Mwana wa Mungu, huwezi ukasema mtu akifika mbinguni ndio atakuwa ameokoka halafu nawewe ukaanza kujipa moyo na kusema nawewe utafika mbinguni wakati hauna jitihada zozote zinazo fanana na unacho ki-amini, NB; kufika mbinguni ni sehemu moja wapo ya ushindi au wokovu, lakini lazima utambue kwamba ushindi huo haujaja ghafla tu bali katika ulimwengu wa roho mtu huyo alishaokolewa hata kabla hajafika mbinguni alikuwa tayari na kibali (tiketi) yaani mtu wa Milki ya mbinguni

Pia unaposema mpaka mtu afike mbinguni wakati hakuna jitihada zozote, je utafikaje pasipo kuijua njia au kuwa na Paspoti? (kibali / kitambulisho ) kwani haujui kuwa ukiwa na kitambulisho tayari ni ishara ya kupata haki yako hata kabla ya kupewa  haki halisi? Sawa kuna wakati njia una ijua sasa utapitaje hiyo njia usipo kuwa na sifa za kupita hiyo njia?.
 Twende sambamba, kwa mfano; mtu umepewa kanuni na mbinu za kufika ng'ambo ya mto. Ukaambiwa kabla haujavuka amini kuwa umeshavuka, lakini amini huku unafanya mazoezi ya kurukaruka ili uimarishe mifupa itakayo kuwezesha kuruka mpaka ng’ambo zaidi. pia uwe unakula vyakula Vya kuongeza nguvu ili ziku saidie Siku ya kuruka. halafu wewe ukapuuzia,  je unafikiri utaweza kuruka? Siku ikifika,

Hapa ndio utakuta wengine wana jipa moyo wakisema ninaweza nika bahatisha hata kama siku fuata zile kanuni. Ndugu unamjua aliye ziweka hizo kanuni (mbinu) kwanini aliziweka, Mwana wa Mungu, acha ubishi. kawaulize?  una wakumbuka, wale wazee na vijana waliokuwa wakimcheka Nuhu wakati akijenga safina?. Walikuwa wabishi kama wewe lakini bahati nzuri walipata jibu zuri Siku ya gharika. sasa onyo kwako usisubiri siku mbaya zifike.

Mwingine anaweza kusema  mbona ninaweza kukatia tiketi nikiwa ndani ya gari,  tatizo lako unamawazo ya safari fupi ambazo hazina utaratibu maalum wa utendaji wa kazi, na ndivyo anavyo fanya shetani anakukatia tiketi ukiwa ndani, lakini Mungu
anataka kabla hujaianza safari uwe na tiketi kwa sababu safari yake sio ya magendo bali nisafari halisi ya kifalme.

Siku moja Mtu mwingine akani ambia wana wa Israeli wasingelivuka ile Bahari basi wokovu wangekuwa hawaja pata nikagundua kwamba huyu mambo ya rohoni yeye anayafikiria sana kimwili, anafikiri ni hisabati zenye majibu ya “kubeti” nika mwambia; Wana wa Israeli wokovu wao ulianzia misri kitendo cha Farao kuwapa ruhusa ya kuondoka misri, katika ulimwengu wa roho ina maanisha wokovu walisha kuwa nao toka misri na ndio maana waliachiwa huru, na kuivuka Bahari ilikuwa ni mwendelezo wa utimilifu au uthihirisho wa ushindi waliokwisha upata kutoka misri. Hii ni kwasababu hata baada ya kuvuka bahari bado safariyao ilikuwa haija timia.
Kama huja nielewa labda nikuulize swali; je, unafikiri wana wa Israeli wasingeliruhusiwa kutoka Misri kuianza safari ya kuelekea nchi ya ahadi. Pale baharini wangefika?. Hapo ndipo utakapogundua kwamba, safari ya ushindi au safari kuelekea nchi ya ahadi waliianza toka wapo Misri.

A.  JE, TUNAWEZAJE KUIJUA NJIA YA KWENDA MBINGUNI?

Bwana Yesu alikuja duniani kutuonesha njia ya kuelekea nchi ya ahadi ambayo kwa kuja kwake ali ianzisha mara moja (yohana 17-19).

MAANA YA KUOKOKA; Kuokoka ni kunusurika, kupona, kukombelowa, kutolewa katika hatari, kuwa katika hali ya usalama, salimika
WOKOVU; Hii ni hali ya kusalimika na adhabu ya mwenyezi Mungu; hali ya kuwa mbali na adhabu ya mwenyezi Mungu

NB; Unaweza kunusurika na adhabu ya Mungu ambayo ingekupata ukiwa duniani mfano laana nk au adhabu ya baada ya kufa kutupwa katika moto wa milele, hivyo wokovu ni neema inayo kuja kwa imani. (Waefeso 2;8) “kwa maana mmeokolewa  kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, nikipawa cha Mungu” nikipawa cha Mungu inamaana imani au mtu anapokuwa na uhakika juu ya kwamba yeye ni mshindi hata kabla hajafa ni kipawa kwasababu si kila mtu anaweza kuamini hivyo ndio maana kwa msaada zaidi Bwana Yesu alikuja duniani kutupa kipawahicho ili tuwe na uhakika wa safari.(Mt 1:21)inakazia kuwa Yesu alikuja kuwaokoa au kuwa kusuru wanadamu na dhambi zao, sasa swali dhambi hizi aliwanusuru mbunguni au alikuja duniani ilikuokoa kilicho potea? (Luk19:9-10)hii ni habari ya zakayo

NB; KUOKOKA SIO DINI MPYA BALI NI NEEMA ILIYO KUWAPO TANGU MWANZO, Wamisionari wali leta dini kwa staili ya wokovu lakini kadiri siku zilivyo kwenda kuna uzembe ukaanza kuingia makanisani na kuanza kuchukulia  kumtafuta Mungu  kama kitu cha kipuuzi hivyo wanadamu wakaanza kuchanganya miungu wakijua ndiye Mungu.(Falsafa ya kiafrika, Amerika, Malawi n.k visikutinge hizi ni zakidunia hivyo jifunze falsafa ya Mbinguni hili ndilo kusudi la kuja kwa Bwana Yesu duniani ili tuziache falsafa zakidunia.

Wokovu unampa mtu uhakika wa safari yake watu wengi hawana uhakika wa safari yao ya mbinguni kwa sababu ya mafundisho waliyo ya pata au walivyo ya elewa vibaya
Maandiko ya biblia katika (yohana,8:12-14) yana sema  Basi Yesu akawaambia tene akasema, mimi ndimi nuru ya ulimwengu yeye anifuataye, hata kwenda gizani kamwe, bali atakuwa na
nuru ya uzima ,Basi mafarisayo wakamwambia, wewe unaji shuhudia mwenyewe, ushuhuda wako sio kweli, Yesu akajibu akawaambia, mimi ingawa najishuhudia mwenyewe ushuhuda wangu ndio kweli; kwa sababu najua niliko toka na niendako; lakini ninyi hamjui nilikotoka wala niendako”
Nime amua kuitumia aya hii ambayo inaonesha namna BwanaYesu alivyo kuwa na uhakika wa anako kwenda, kwa sababu haku onekani kwa macho ya kawaida ambapo hata mafarisayo hawa kujua niwapi huko.
sasa ndivyo ambavyo mwanadamu anaye jua ya kuwa yupo safarini, safari ya kuelekea mji mtakatifu  ni muhimu awe na uhakika wa safari yake yaani awe na uhakika na kule aendako (ukiona wewe huna uhakika yaani unasemakuwa siwezi kuwa na uhakika kuwa mimi ni mshindi kabla sijavuka mto), basi ujueuko matatani kuelekea mbinguni, (mji wawatakatifu),najua unaogopagharama wakati Yesu alisema mzigo wake sio mzito bali ni mwepesi (Mt 11:28-30), (nirahisi kuuona ushindi huo ninao kwambia tukiwa uko upande wake),

B.  JE KUWA UPANDE WA YESU MAANA YEKE NINI?

Kuacha ,ulevi ulafi wizi ,chuki, uzinzi, uchawi, ushirikina wivu mbaya, nk ( yahana 14:23-24) ; Mfano wewe unapo kwenda kwa nganga wa kipepo halafu unapinga eti wokovu sio leo, kama sio leo unamaanisha wanadamu hawapo safarini (yohana 17;15-16) na kama wapo safarini   je, mtu aliyeianza safari hiyo anakuwaje?, yaani anakuwa na mtazamo gani au uelewa gani? ,na imani gani? ,na anajitahidi sana katika maisha yake kufanya mambo gani ?

kwa kawaida mtu aliye amini kifo cha Bwana Yesu msalabani ni lazima atajua na kusudi la kifo chaYesu. Kwa ufupi Yesu alikuja kutuonesha njia ya Kwenda kwa Baba (Mji mtakatifu au Yerusalemu mpya) ndio maana katika mafundisho yake alikuwa anasema kuwa Yeye ni njia kweli na uzima (yahana 14:6-7) , kila aaminiye hata tahayarika.   

Wokovu ni kama taa ya kuwaongoza wateule siku ya kumlaki Bwana Yesu mawinguni, kwa kawaida mwana wa Mungu aliye katika safari ya mbinguni ni lazima awe na taa yenyenguvu na sio kutegemea taa ya mwingine, maana giza litakapo ingia wasio na taa na mafuta yakutosha itawawia vigumu kumlaki Bwana Yesu mawinguni; ndugu mfano huu pia alisha tuwekea wazi Bwana Yesu kabla ya kupaa kwake (Mt 25:1-13)

Pia ngoja niweke wazi kuwa Yesu alisema alikuja ulimwenguni siyo kuu hukumu ulimwengu bali ulimwengu uokolewe katika yeye. ukiendelea kusema kuwa wokovu sio duniani swali; BwanaYesu duniani alikuja kufanya nini? mpendwa yesu alikuja kuwaelekeza
wanadamu njia sahihi na mbinu zifaazo za kufika mbinguni, kwa kuwa wanadumu walikuwa wanasikia lakini hawasikii yaani kuwafungua walio fungwa. na ingekuwa wokovu hauanzii duniani basi asingeshuka duniani, kwani angekuja kufanya nini,
inamaana angebaki mbinguni, ingelikuwa wokovu unapatikana kulekule asinge kuja ange tusubiri kule kule.

kwani mtu akitaka kuwa padre akifika kanisani tayari anakuwa padre ?, kama jibu ni hapana ina maana kuna mlolongo fulani wa maisha ya maandalizi ya kuwa padre ndivyo ilivyo katika ufamle wa Mbinguni .

Mpendwa hiki ndicho kilicholeta shida sana hata kabla Yesu hajapaa mbinguni. waandishi mafarisayo na walimu wa sheria walimpinga sana aliposema kuwa yeye ni mwana wa Mungu na
amekuja kuokoa ulimwengu, wakasema kuwa haiwezekani mbona wewe tuna kufahamu ya kuwa ni mwanadamu kama sisi, na umekuja kuokoa ulimwengu wewe kama nani na umetoka wapi, hawa kujua kwamba kuna safari na maisha mapya wanayo takiwa kuanza kuyaishi kwa nyakati hizo za ujio wake ambao ulikuwa na lengo la kuwafanya wanadamu wajitambue kuwa duniani sio kwao (wanapita kama vile yeye alivyo mpitaji). kitendo hiki cha yesu kuja duniani pia ni kati ya vigezo vinavyo ashiria kuwa wokovu una anzia duniani
na mtu akivumilia mpaka mwisho katika maisha hayo ya wokovu kutokana na yale yatakayo tokea ili kupoteza uamuzi wake wa kumfuata yesu. ndiye atakaye fikia utimilifu wa wokovu au wa safari aliyo ianzia akiwa duniani .
                 
              
C.   THAMANI YA WOKOVU DUNIANI.

Thamani ya wokovu duniani ni kumpa mtu uhakika wa safari. pia humpa mwanadamu.
·       Kukombolewa, yaani Kulipiwa deni (Kufutiwa mashitaka),(Kol.2:12-15)
·       Kuzaliwa Upya kiroho, yaani kuzaliwa mara ya pili; ili kufanyika Mwana wa Mungu na kuwa kiumbe kipya kwa imani.(Yoh.1:12,13; 2Kor. 5:17)
·       Kutumikiwa na Malaika wa Mungu; (Ebr.1:13,14) (Kut 23;20-22)
·       Kutawaliwa na nguvu za Mungu kwa njia ya imani. (1Pet. 1:3-5; Zab.34:7)
·       Kupewa ahadi ya Baba, yaani Roho Mtakatifu na Ujazo (kutawaliwa/ kuongozwa) wa Roho Mtakatifu.(Mdo.2:37-
40 )
·       Kuwa Mtakatifu ungali bado upo duniani na Kumpendeza Mungu, haiwezekani; (Zab.16:3):
·       Tunashinda na zaidi ya kushinda kwake yeye atupendaye. (Rum. 8:31-39).
·        Kuwa wanafunzi wa Kweli-Kweli wa Yesu kristo (Yoh.8:31,32)
·       Kusikilizwa na kujibiwa maombi mbele za Mungu.
·       Kuwa na mamlaka na amri juu ya nguvu za shetani, mapepo, majini, magonjwa, sumu, na nguvu zote zauharibifu (Marko 16:17-20; Luka 10:17-20).
·       Kuepushwa na moto wa milele au hukumu ya milele.(Rum. 8:1) n.k.
·       Maadui zako watakuwa maadui wa Mungu(Kut 23;20-22)
Kumbuka hata Roho mtakatifu katika matendo ya mitume hakuwashukia wakulima au mafarisayo au walimu walio kuwa mashuleni bali aliwashukia wale waliokuwa wakimngoja katika utakatifu (walio mkiri Bwana Yesu kuwa yeye ni mwokozi), Ndipo walipopata nguvu ya kuhubiri kwa nguvu neno la Mungu. na kushinda, mpendwa muulize Paulo na Sila, kilicho wafanya wafunguliwe gereza mbali na kumsifu mungu (ni nguvu gani hiyo) tatizo wengine wame zoea
kumtegemea mwanadamu ndio maana ni wabishi, endeleeni kubisha kuna siku mtasikia mwangwi wa ubishi wenu mlio ufanya miaka mingiiliyo pita.na mwangwi wa injili hii masikioni mwenu

Pia Yesu alisema kwa kupingwa kwake sisi tumepona, (Isaya 53-5), inamaanisha sio tutapona bali tumepona ina maanisha nini?, hili neno linaupana, yaani ushindi nikuanzia sasa mpaka kuurithi ufalme wa mbinguni, haleluyaaa pia neno jingine ni hili aaminiye na kubatizwa ataokoka, yeyote anaye amini kuwa Yesu alikufa kwaajili yake nilazima ataamini ya kuwa kifo chake msalabani ndicho kilicho mpa uhakika wa safari yake. na safari hii ya ushindi anaianzia duniani kwani Yesu alisha ianzisha duniani ndio maana kwenye maombi yake ya mwisho alisema “siombi uwatoe duniani bali uwakinge na yule mwovu” ,(yahana 17:15) (huu ni ushindi alio ukusudia tangu tunapokuwa duniani) kisha akasema “ili pale nitakapo kuwepo nanyi muwepo” ( yahana 14:3).

Mkristo au mwanadamu yeyote ni lazima aamini kuwa Yesu alikuja kumu andalia mwanadamu maisha ya baadaye ndio maana alisema ninakwenda kuwaandalia makao ili, pale nitakapo kuwepo nanyi muwepo, kwa sababu yeye ndio njia, utasemaje kuwa utafika mbinguni wakati hauyatendi yale aliyokuagiza. Mtu anaposema nime okoka ina maana ana uhakika na kifo cha yesu msalabani inamaana ana imani nacho kwasababu kitendo cha kufa kwake pale msalabani na ndipo wokovu ulipopatikana.

Hilo andiko katika (Mit 24;13) kwa ufupi haliwahusu wale ambao hawaja jitambua na kuianza safari ya kumfuata Bwana Yesu kwa matendo yaliyo amriwa na Yesu, ndio maana utaona kisa cha Yesu kuongea hivyo ilikuwa ni pale wale walio mkubali na kumfuata walipo muuliza kwa habari ya ishara za nyakati (mwisho wa dunia ), ndiposa akawaambia kuwa wavumilie maana kuna mambo yata kayo wapata lakini atakaye jitahidi kuvumilia mpaka mwisho ndiye atakayeokoka. Naomba nikuulize ikiwe wewe ni mzinzi au mchawi au mlafi au mwizi au una woga au muuwaji ,ukilichukuwa andiko hili na kusema lina kuhusu sasa unataka uniambie ya kuwa uvumilie uovu wako ? ndipo uingie mbinguni, hata kama ni kuvumilia changamoto mbona changamoto alizo nazo mwenye dhambi asilimia kubwa ni kuto kana na uovu wake lakini Yule aliye upande wa Mungu mara nyingi huwa changamoto zake huwa kama majaribu, SOMA (mdo;4:12). na ( luk 19:9),

D.  SOMA VIFUNGU HIVI UJUE ZAIDI JUU YA SAA YA WOKOVU (AU MUDA  WA KUOKOKA).

Kuna watu wanafikiri kuwa siku yao ya kuokoka haija fika na kisa kuna maandiko yanayosema kuwa kilajambo lina wakatiwake basi watu wanafikiri kuwa kuna siku iliyopangwa ya mtu fulani kumpokea yesu, nataka nikutoe kwenye fikra hii, mpendwa Bwana Yesu anataka wanadamu wote tumkubali yeye na kumpa maisha yetu kila mmoja leo na sio kesho na ndio maana alisema msiya sumbukie ya kesh eti mtakula nini au mtakunya nini au mta vaa nini bali utafuteni kwanza ufalme wa Mungu na haki yake, na hayo mengine mtazidishiwa, tatizo wanadamu wana poona ya kuwa wana hitaji wapate muda wa kutimiza haja za miili yao, wanaanza kujitetea wakisema wakati wao bado (najua siri hii unaweza kuipinga lakini ndio mpango halisi wa Mungu ya kuwa uokolewe leo, kitendo cha Yesu kuja duniani hakikuhitaji tena kutoa au kuongeza wakati wa mtu fulani kuokolewa bali kitendo cha kufa kwake na kufufuka ndipo wakovu mkuu ulipo anza na kutangazwa rasmi kwa kila aaminiye

Shida sio Mungu hajapanga uokolewe leo bali ni ufahamu wako ulio tekwa na ibilisi juu ya suala zima la wokovu na muda ufaao. ndio maana Yesu alisema kesheni mkiomba kwakuwa hamjui saa wala mtafuteni bwana maadamu anapatikana (Isaya55:6-7) , anaposema hatujui muda wala saa ina maana kuna jambo lazima lifanyike leo.

Yaani Mpaka hapo, siri za Mungu haziangalii elimu ya mtu yaani hata wewe msomi unashindwa kuujua ukweli wa maandiko mpaka hapo nimeamini ya kuwa maneno ya Yesu aliyo sema Aliwaficha wenye hekima na akili akawafunulia watoto wachanga nisahihi kabisa, mpendwa weka elimu yako mbali na kumtafuta Mungu vingi nevyo elimu yako ita kuponza ,usiangalie wadhifa wako Yesu ana wadhifa mzuri kuliko wewe, achamadoido, njoo kwa Yesu, hapa haijarishi wewe ni waziri Mwalimu, Raisi, Papa , Askofu , Mchungaji, Mkulima, Mchawi, Balozi, Mtoza, ushuru Farisayo au mwanasheria wote twende kwa Yesu, lakini usikurupuke. Fanya maamuzi toka moyoni na uamue kweli kumpa Yesu maisha usiigize au kufuata mkumbo ,bali amua mwenyewe. toka rohoni mwako. hakika utamwona Bwana.

E.  SOMA ZAIDI AYA HIZI CHACHE KATI YA NYINGI NA ROHO WA MUNGU ATAKUPA NEEMA
           
1kor6:1-10,Mdo28:1,Yohan5:41-47,Walawi1930-31, Isay8;16,Yoha10:19,Ebrani2:3,Yahana3:14-15,Luk.1:77, Mdo.2:47b, 1kor.10:32-33, 2kor.6:2, Kol.1:13,1tim.1:15, Rumi.8:24,Efes.2:8.

Isome na kuielewa ingawa kunamingine mingi ielezayo juu ya saa ya wokovu (usisome kiupinzani, soma kwa kutamani kupata ukweli), Amina.
                      



usisome kiupinzani soma kwa kutamani kupata ukweli) pia soma vizuri somo zima
na Mungu Roho mtakatifu atakufundisha na kukuelewesha kupitia jina la yesu
Amina,

          E.mkinga
      Share kwenye mitandao mingine


EmoticonEmoticon