Tuesday, 3 October 2017

Tags

    NAMNA YA KUISHINDA DHAMBI YA UZINZI /UASHERATI

Bwana Yesu asifiwe mpendwa katika Kristo. Leo napenda tujifunze kwa ufupi namna ya kuishinda dhambi ya uzinzi/uasherati ambayo inaonekana kuwatesa wengi kuanzia ngazi ya wachungaji ,vijana wazee ,wanandoa , wachumba na kila mwanadamu duniani .USIACHE KUPITIA ETI KWASABABU UNAHISI UNAJUA SAANA MASUALA KAMA HAYA BALI MUNGU ANA KUSUDI NA WEWE. Kwa maana yeye anajua yale yote unayokuwa unayafanya ukiwa peke yako (sirini ), hivyo nami nitapita sirini katika hiyo njia ya giza iliyokufunga na kukufanya uwe mtumwa wa uzinzi nakisha nitakuleta nuruni kwajina la Yesu kristo hata kama hutaki,maana nimegundua hii roho inakusumbua ,  (pia najua inawasumbua wengi maana nimekutana na maswali mengi juu ya suala hili,ndipo nikaamua nikupe angalau vipande vichache kama ifuatavyo)

Kwanza kabisa katika somo lililopita la dhambi tuliangalia maana ya dhambi na dawa ya dhambi lakini leo tutaangalia namna ya kushinda dhambi ya uzinzi. UZINZI NI KUSHIRIKIANA TENDO LA NDOA NA MTU PASIPO IDHINI YA MUNGU ANAYOITOA BAINA YA WATU WAWILI WA JINSIA TOFAUTI (mke na mume) KUPITIA WATUMISHI WAKE, KUIDHINISHA MAHUSIANO HAYO BAINA YA JINSIA MBILI KWALENGO LA KUISHI PAMOJA KAMA MUME NA MKE WAKIZAA WATOTO NA KWENDA MBINGUNI. LAKINI UASHERATI NI KITENDO CHA MKE AU MUME WALIO KATIKA NDOA KUSHIRIKI TENDO LA NDOA NJE YA NDOA YAO ILIYOIDHINISHWA NA MUNGU KUPITIA WATUMISHI WAKE. Sikufariji ya kuwa uzinzi ulioufanya au unaoufanya Mungu atakusamehe tu ukimwomba bali nataka ujitambue yakuwa Mungu sio wa mizaa,utani au sio wa kuhangaishwa jitahidi kuwa makini maana hiyo ni mbinu tu ya kivita ambayo shetani anatumia kukutafuna waziwazi bila wewe kujua hebu fanya maamuzi makuu upya yatende yaliyo mema mengi, chukia uzinzi kama matapishi yako mwenyewe

CHANZO CHA MTU KUTENDA DHAMBI YA UZINZI/UASHERATI

Hapa kumbuka sizungumzii asili ya dhambi kwani hiyo tulishazungumzia kwenye somo lililopita. Mara nyingi dhambi huja kwa njia ya mawazo ambayo mtu anayapa nafasi nahali mawazo hayo yakiwa si mazuri, pia kupitia kuona, macho yako unapotazama vitu mbalimbali mfano mwanaume unapomtazama wanawake, na kuipa akili nafasi ya kutafakari maungo ya mwili wake au muonekano wake unaomfanya avutike kumtazama na kisha kuanza kutafakari, ingawa kwa njia ya kuona tu anakuwa ameshafanya uzinzi, rejea (Mathayo 5:27-28) halikadhalika kwa njia ya kuzungumza,ambapo mtuanachukua hatua ya mojakwamoja kuzungunza na mtu wa jinsia tofauti juu ya uzinzi, (Mwanzo 3:6 ) inasema “mwanamke alipoona ya kuwa ule mti wafaa kwa chakula ,wapendeza macho nao ni mti wa kutamanika kwa maarifa basi alitwaa katika matunda yake akala akampa na mumewe naye akala” 
.Mpendwa hapa sizungumzii kuwa Adamu na mkewe walifanya uzinzi, hapana ,bali nataka uone kilichopelekea kula yale matunda ya mti walio katazwa, cha kwanza mawazo yalianzishwa ndani yao lakini hawakuyashughulikia wakayapa nafasi yakuendelea kuwatafakarisha juu ya uwezekano wa kula yale matunda, maana kiukweli ule mti ulikuwa ni watofauti na kilichopelekea kuendelea kutafakari ilikuwa ni roho ya kishetani ambayo ikiwadanganya, namaanisha shetani alipanda wazo ndani ya Eva na Eva akapanda wazo ndani ya Adamu kutokana na ile roho iliyo mwingia na mwishowe wakaanguka katika dhambi, (Mwanzo 3:1-4,…) utaona maandiko yanasema “ Basi nyoka alikuwa mwerevu kuliko wanyama wote wa mwituni aliowafanya Bwana Mungu ,akamwambia Mwanamke ,At! Hivi ndivyo alivyosema Mungu msile matunda ya miti yote ya bustani? Mwana mke akamwambia nyoka matunda ya miti ya bustani twazeza kula lakini matunda ya mti ulio katikati ya bustani Mungu amesema msiyale wala msiyaguse msije mkafa ,Nyoka akamwambia mwanamke .Hakika hamtakufa”. Ninachotaka hapa ujue ni kwamba shetani anapotaka utende dhambi usifikiri atatumia kitu kingine zaidi ya viungo vyako mwenyewe anaweza kutumia macho yako, masikio yako, kinywa chako, au akili yako kupandikiza wazo na kisha anaendelea kukupa maswali ya changamoto; mfano anaweza kusema; Ati! wewe unafikiri toka uokoke au tangu upadirishwe au tangu uslimishwe au tangu ubatizwe ni miaka mitatu au mitano au ishirini sasa hujafanya uzinzi hata mara moja wakati wenzako wanafanya uzinzi na bado wanamtangaza Yesu ya kuwa ni Bwana acha uzembe unafikiri ukifanya tu mara moja kwani kunashida siutatubu? Damu ya Yesu ipo kwa ajili yako fanya leo tu, huoni binti huyo utamkosa, tumia fursa hiyo, yaani wewe ni padre kabisa kweli miaka yote hii unafikiri utaweza kukaa bila kujaribu hata moja? Hebu ukaongee na mama Yule, au dada wa secrestia ukimwacha shauri yako, au anaweza kusema yaani wewe mwalimu huwaoni hawa form four na form three mbona wakubwa halafu huoni wamenawiri watamaliza shule shauri yako au shetani anaweza kusema, wewe mama fulani sikuhizi kuna vijana wengi wenye mapenzi ya kweli na wabichi kabisa, huyu mume wako ukimtoroka siku moja kwani kuna shida yoyote? Si mara moja tuu. 

Hii yote ni mifano ambayo shetani ana weza kutumia kukuanzishia wazo ndani yako ili uanze kulichanganua, pia ukisoma (Mathayo 5:27-28) neno la Mungu linasema “mmesikia kwamba imenenwa,usizini,lakini mimi nawaambia kila mtuatazamaye mwanamke kwa kumtamani amekwisha kuzini naye moyoni mwake ,jicho lako la kuume likikukosesha ling’oe ulitupe mbali nawe kwa maana yakufaa kiungo chako kimoja kipotee wala mwili wako mzima usitupwe katika jehanam” pia hapa unaona bado anaeleza ya kuwa kumbe hata macho yako shetani anaweza kuyatumia kukukosesha na ndio maana anasema amtazamaye mwanamke na kumtamani, kumbe kumtazama tu pasipo tamaa sio dhambi lakini kuna muda shetani anapotaka kukuangusha analeta tamaa za uzinzi wakati ule unapomwangalia mwanamke na kumtamani ndipo dhambi ya uzinzi inapotajwa, lakini Yesu akatoa suluhisho ya kuwa hilo jicho lililokukosesha yafaa uling’oe yaani hiyo hali ya kuwatazama wanawake au wanaume na kuwatamani kiuasherati hiyo hali mbaya yafaa uikatae ikae mbali nawe, kumbuka msaada pekee wa kufanikisha hilo ni Roho wa Mungu ambaye anapatikana kwa njia ya kumkubali Bwana Yesu kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yako na ndiposa Mungu Baba Mwana na Roho mtakatifu watakuja watafanya makao ndani yako na kukushindia, Haleluyaa!! 

Nina jua inawezekana unafanya uzinzi lakini wewe mwenyewe hupendi ingawa jitihada zako ili uepukane na uzinzi ni za kiwango cha chini, ushauri wangu sogea kwa ujasiri mbele ya kiti cha rehema cha Mungu na kuanza kuyatenda mema mengi ili uovu wako usahaulike na uamue kutoka moyoni maana inawezekana. 
Hata leo umepanga kufanya uzinzi hujui ya kuwa Mungu anakuona hatakama utajificha na unaposoma ujumbe huu kuna roho ndani yako inakwambia acha kusoma mbona anakukatisha mpango wako wa kafanya leo tu. NATAMKA KUPITIA MAMLAKA NILIYO PEWA NA BWANA YESU YAKWAMBA HIYO ROHO INAYO KUSUKUMA IKIKUDANGANYA KWAMBA UKAFANYE LEO TU NINA IAMURU KUPITIA JINA LAYESU NDANI YAKO MSOMAJI, NINAIYEYUSHA KWA DAMU YA YESU NA KWA JINA LA YESU, HILO JINI MAHABA NALIKATIKE VIPANDE VIPANDE NA KUANGUKA CHINI YA MIGUU YAYESU KRISTO, NINAKUUNGANISHA WEWE MSOMAJI NA UFALME WA MUNGU ILI MUNGU ATUME SASA UWEZA WAKE UTAKAO KUFANYA USHINDE, NA ULE MPANGO WAKO WA KWENDA KUZINI UFE KWA JINA LA YESU, AIMEN!!
(1Korintho 6: 18 ) Neno la Mungu linasema “Ikimbieni zinaa kila dhambi aitendayo mwanadamu ni nje ya mwili wake ila yeye afanyaye zinaa hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe”, mpendwa yaani mpaka ufikie kwenywe zinaa ya kuvua nguo na kulala na mtu wajinsia tofauti inamaana sio kitu cha kawaida ulimpaje ibilisi nafasi ya kumvulia nguo zako au hujui ya kuwa ikiwa unafanya zinaa katika ulimwengu wa kiroho Mungu angetaka akufungue macho uone umelala na nani najua usingerudia tena watu wengi sana wana lala na shetani mwenyewe na mapembe yake na uchafu wake lakini anazifunga fahamu za watu wasijione ya kuwa wamelala na nani ili yeye aweke lile pando litakalokuletea mauti pasipo wewe kujua kwa muda ule na ndio maana mtu akishafanya uzinzi ndio anaanza kujutia ni kwanini amefanya.

 Mpendwa mwana wa Mungu hebu rudi kwa Yesu kwa matendo mema na toba ya rohoni ya kufunga na kuomboleza juu ya uovu huo maana ukiuendekeza utakupeleka jehanam, Yesu bado anakupenda na ndio maana amekupa kuwa hai ili ufanye matengenezo mara moja kwa kuwa saa ya wokovu ni sasa.

(Waefeso 5:3) Neno la Mungu linasema, “Lakini uasherati usitajwe kwenu kamwe wala uchafu wo wote wala kutamani kama iwastahilivyo watakatifu” , (Warumi 6:12-14) “Bali dhambi isitawale ndani ya miili yenu ipatikanayo na mauti hata mkazitii tama zake wala msiendelee kuvitoa viungo vyenu kuwa silaha za dhuruma kwa dhambi bali jitoeni wenyewe kwa Mungu kama walio hai baada ya kufa na viungo vyenu kwa Mungu kuwa silaha za haki kwa maana dhambi haitawatawala ninyi kwa sababu hamuwi chini ya sheria bali chini ya neema”. ikiwa utahitaji kuishinda dhambi hiyo ya uzinzi basi lazima ukubali kuvitoa viungo vyako kwa Yesu ili vitumike kumtangaza yeye maana ukiwa chini ya neema yake (wokovu kamili) ndiposa utaweza kushinda hata kama ni mlei au mtumishi wa Mungu lazima ujitoe kweli kweli na si kuigiza ili ushinde na hakika utashinda 

(Rumi 6: 19-23) Neno la Mungu lina sema “ Nasema kwa jinsi ya kibinadamu kwa sababu ya udhahifu wa dhamili yenu kwa kuwa kama mlivyovitoa viungo vyenu vitumiwe na uchafu na uasi mpate kuasi vivyo hivyo sasa vitoeni viungo vyenu vitumiwe na haki mpate kutakaswa maana mlipo kuwa watumwa wa dhambi mlikuwa huru mbali na haki ni faida gani basi mliyo pata siku zile za mambo hayo mnayoyatahayarikia sasa? Kwa maana mwisho wa mambo hayo ni mauti lakini sasa mkiisha kuwekwa huru na kuwa mbali na dhambi na kufanywa watumwa wa Mungu mnayo faida yenu ndiyo kutakaswa na mwisho wake ni uzima wa milele kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika kristo Yesu Bwana wetu” na hii ndio maana Daudi alisema “Maneno ya kinywa changu na mawazo ya moyo wangu yapate kibali mbele zako Mungu mwamba wangu na mwokozi wangu ,” (Zaburi 19:14) alita mbua ya kuwa kumbe mawazo yake si mazuri yanampelekea kumwasi Mungu sasa sijui wewe kama umetambua ya kuwa mawazo yako unayaendekeza kwenye dhambi mpaka unaanguka ndipo ushituke?. 

(Wakolosai 3:5) Neno la Mungu linasema “Basi vifisheni viungo vyenu vilivyo katika nchi ,uasherati,uchafu tamaambaya,mawazo mabaya na kutamani ndiyo ibada ya sanamu”
(Warumi 5:19-21 ) “kwa maana kama kuasi kwake mtu mmoja watu wengi waliingizwa katika hali ya wenye dhambi , kadhalika kwa kutii kwake mmoja watu wengi wameingizwa katika hali wa wenye haki, lakini sheria iliingia ili kosa lile liwe kubwa sana na dhambi ilipo zidi neema ilikuwa nyingi zaidi ili kwamba kama vile dhambi ilivyotawala katika mauti vivyo hivyo kwa njia ya haki neema itawale hata uzima wa milele kwa Yesu Kristo Bwana wetu”. Mpendwa unaweza ukadhani kuwa kwakuwa uovu umetawala sana duniani nawe umejikuta kama hufai tena kutokana na uovu ulio ufanya unahisi kuwa uovu uliotenda umekuwa juu kuliko uwezo wa damu ya Yesu lakini hapo juu maandiko yanakuambia neema ya Mungu ni kubwa juu yako.

                                 MADHARA YA UZINZI

§  Huondoa ujasiri wa mwana wa Mungu kusogea mbele za Mungu na kumueleza mahitaji kwani muda mwingi uovu alioutenda humsumbua ndani ya nafsi yake

§  Humtenga mtu na uso wa Mungu hata akiomba Mungu hataki kusikia isaya 59:1-3
§  Huondoa amani. Kwasababu zile roho zilikuwa na lengo hiloili uwemnyonge
§  Hufunga mtu asiwe nakibali cha kuingia mbinguni
§  Mapepo ya aina mbalimbali kama umaskini ,mapepo ya kuvunja ndoa, kukataliwa nk huingia ndani ya mtu na kufanya makao
§  Huleta laana kwa mtu aliyefanya uzinzi. Kumb 27:20-26
§  Hurithiwa kizazi hadi kizazi
§  Kufa kwa kipawa au talanta. Mathayo 25: 14-29  Husababisha kuvunjika kwa ndoa na hii ni kwasababu mtuamefanya uasherati jambo ambalo ni kinyume na amri za Mungu shetani hufanya makao ndani ya mtu na kumfanya mtumwa wa uzinzi na uasherati.na ndio maana mtu anaota anaota ndoto amelala na mtu wa jinsia tofauti wakifanya uzinzi wakati hajaoa au ameoa au kuolewa. hapo damu ya yesu na jina la Yesu lazima viingilie kati maana hilo sasa katika ulimwengu wa roho ni agano tosha kabisa kuvuruga maisha ya mtu
§  Hupelekea mtu kukosa kibali cha kuoa au kuolewa kwasababu mtuanakuwa amesha olewa katika ulimwengu wa roho hivyo nivigumu kuolewa na ndio maana watuwanaachika sana na dawa ni damu ya Yesu pekee.
§  Husababisha kufarakanishwa kwandoa .jambo ambalo mpaka damu ya Yesu iingilie kati

MAMBO YA KUZINGATIA ILI UEPUKANE NA UZINZI

Haijalishi umeanguka katika dhambi ya uzinzi mara ngapi bali fanya au jifunze kufanya yafuatayo ili upate kuushinda, lakini kumbuka Mungu anasema ili ushinde ni lazima uwe umeyatoa maisha yako kwake ndiposa utakapokuwa na ile nguvu ya kushinda (rumi 6:19-23) na hii haijarishi wewe ni mlei au papa au padiri au shemasi au mchungaji haijarishi inawezekana kuna uovu una urudia maranyingi na kumbe viwango vyako vya kujimimina kwa Yesu havitoshi kulifisha tatizo la kuirudia dhambi yaani unairudia rudia kwasababu hujajimimina sawa sawa kwa Bwana Yesu.
§  Usipende kukaa sehemu au jirani na vitu vinavyoweza kuwa kichicheo cha kukuingiza katika mawazo ya uzinzi. Mfano ikiwa unapokaa kunapicha za uchi basi unapoziona mara nyingi ni lazima utaishia kujiuliza maswali juu ya vitendo hivyo, Mungu aliye hai na akusaidie uzitoe hizo picha ndani kwako. JE UMEWAHI KUJIHOJI WATU WAVYOEKA PICHA ZA UCHI UKUTANI LENGO LAO NI NINI? JE, WEWE UNAYEWEKA PICHA ZA UCHI ZA MTU UKO TAYARI WEWE UPIGWE PICHA NA UBANDIKWE UKUTANI? ACHA UCHAFU HUO
§  Unapotumia mtandao usipende kutazama picha za uchi au chochote au maelezo yanayohusu mahusiano wakati huja funga ndoa itakuingiza jaribuni
§  Epuka makundi ya marafiki ambao mara nyingi niwafuatiliaji wa masuala ya kimapenzi maana utajikuta nawe umeingia. Maandiko yanasema usikae na wenye mizaha ,wanalisikia neno la Mungu lakini wanapuuzia Mungu hayupo radhi na wapumbavu hebu jiepushe nao. Methali 4:14-18
§  Mwombe Mungu toba ya kweli ukifunga na kuomba juu ya jambo hilo nakujitahidi kuyatenda yaliyo mema Mungu akiuona uaminifu wako atakurudishia hali yako njema ila pasipo toba ya kweli na uaminifu utapata shida. Mathayo 26;41
§  Tumia muda hata wa nusu saa kila siku kutafakari matendo makuu ya Mungu kupitia neno lake na kutafakari madhara yanayo weza mpata mtu anapotenda dhambi. Mathayo 11:28
§  Tumia muda ule ukiwa huna kazi fanya mazoezi au kusoma neno la Mungu au kuwatembelea wahitaji na sio kajadili au kufikiri upuuzi. Yakobo 1:27
§  Epuka kukaa peke yako unaweza kujkuta unaingia hata kwenye uzinzi kwa njia ya mustabartion (kujichua) na hii inawakumba wengi na wengi wana hisi sio kosa hebu acha mara moja maana utapata madhara kimwili na kiroho
§  Weka nia kutoka ndoni ya kuacha ya kwamba kuanzia sasa hutafanya, Rumi 6: 12-14
§  Mwambie Mungu ahsante kwa kukupa uhai maana kusudi lake ili utubu, anajua akikuchukua mapema bado hujajikamilisha matengenezo ya roho yako. Yakobo 4:7-10
§  Hebu achana naye yule unayefanya naye mahusiano, na wengine wanahisi wataoana kumbe mapepo yamewaongoza ili kuwa haribu na kuwa chezea tu. Yakobo 4:4-5
§  Ikiwa kuna mke wa mtu unamazoea naye kupitiliza hakikisha unapunguza mizaha ikiwa ni mtumishi wa Mungu kuna mtu unaweza ukawa unaelewana naye sana mpaka mnapitiliza, epuka maana utaangamia unaweza ukahisi ni upendo wa kawaida kumbe shatani anawanyemelea kwenye hiyo mizaha yenu.
§  Vunja hiyo roho kwa damu ya yesu
Mpendwa kuna uwezekano mkumbwa wa mtu kuanguka katika dhambi ya uzinzi kutokana na mapepo ya uasherati na uzinzi kumwingia mtu huyo na hapa utakuta mtu akilala usiku anaota amelala na mwanaume na anashiriki naye tendo la ndoa wakati haja olewa au hajaoa ,au mtu anaota ndoto anawatoto halafu katika hali ya kawaida sio mtu wa ndoa ina maana katika ulimwengu wa kiriho amezaa au amezalisha watoto wa kipepo ,au mtu anakuwa anahamu sana ya kufanya mapenzi kusiko kwa kawaida ,au utakuta mtu anapenda sana kuangalia picha za uchi za watu .kwa ufupi hizo ni dalili kuwa kuna pepo la uzinzi lina kupelekea  kuwa na hali hizo na usipo kuwa makini unaweza kufikia hatua ya kuwa mbakaji au kahaba kwa sababu ya jini mahaba (ashtaroti) hapa unatakiwa kutubu katika roho na kweli ukimaanisha kuacha(kutokurudia) kasha itia damu ya Yesu katika mfumo wa uzazi ,akili nafsi yako ,kasha zungumza na hilo pepo kuwa unakata mahusiano yaliyojengeka(kwa damu ya Yesu na kwa jina la Yesu )vunja muunganiko na anga la uzinzi uliko unganishwa ,jifukine kwa damu ya Yesu.(mada hii nitaizungumzia kwa upana )                   
Kwa namna ya pekee namshukuru Mungu kwa kunipa wasaa na kibali cha kuzungumza machache, juu ya namna ya kuishinda dhambinya uzinzi, namnin namshukuru Mungu kwa ajilin yako wewe uliyesoma ujumbe huu, Mungun akutie nguvu na kukuzidishia neema na Baraka. Nami ninazidi kumuomba Mungu kupitia jina la Yesu Kristo ili akupe neema ya kushinda juu ya roho hii ya uzinzi inayokuandama. Mwenyezi Mungu na akubariki kwa Baraka zote za mwilini na za rohoni Aminaaa!!!


       E. Mkinga


EmoticonEmoticon