Wednesday, 4 October 2017

LIJUE SURUHISHO KUU LA CHANGAMOTO UNAZOPITIA KATIKA MAISHA YAKO

Tags

LIJUE SURUHISHO KUU LA CHANGAMOTO UNAZOPITIA KATIKA MAISHA YAKO

             

 (Jitahidi usome mpaka mwisho kuna kitu kitakusaidia sana)

Ina wezekana unapitia changamoto mbalimbali katika maishayako inawezekana ni change moto katika masomo yako au katika ndoa yako au katika utumishi wako au katika uchumba wako au katika uchumi wako ,kutokanana changamoto hizo inawezekana ukakata tamaa  juu ya kuhakikisha kwamba unafikia  malengo yako,au ukakata tama hata kumtumikia Mungu aliye hai ,najua unaweza usinielewe juu ya suruhisho hili kuu lachangamotozako lakini najua ukinielewa na kuziweka changamoto zako ndani ya suruhisho hili kuu ,changamoto zako zitayeyuka,na machozi yako ya huzuni yatageuka kuwa machozi ya furaha na shangwe.

Hakuna changamoto isiyo na mlango wa kuingilia na isiwe na mlango wa kutokea,mpendwa kwahizo changamoto zako lipo jibu usiwaze au kufikiri kuwa changamoto hizo zitakuua ,bali fikiria kuwa hizo changamoto zipo kwaajili ya kukusababishia ufanisi wa maishayako ,ukikatatama wewe mwenyewe tafsiri yake ,nikwamba utakuwa umeruhusu mwenyewe mlango wa kushindwa maana ukisoma( mithali 23;7)  “maana aonavyo nafsini mwake,ndivyo alivyo.akuambia,haya,kula,kunywa lakini moyo wake hauwi pamoja nawe”.Acha kufikiri kushindwa.

NB;simaanishi kuwa mwanadamu hapaswi kupitia changamoto lakini namaanisha  kuna changamoto nyingine haupaswi kuzipitia maana ni uonezi tu wa shetani au kuna uovu ulio sababisha ,wengi huwa wanajifariji wakiona changamoto wanayoipitia haitatuliki hujifariji wakisema kuwa  kuwa changamoto anayo pitia ni mpango wa Mungu kumbe ndio kutekwa kwenyewe,hebu shituka

Mungu wakati anakuumba alijua kuwa utakutana na changamoto na kwaakili zako changamotonyingine hutaweza kuzitatua hatakama una hali ya uungu ndaniyako na ndio maana baada ya kutambua hilo akatoa suruhisho mapema ili tusiangamie hatakama changamoto hizo zimekupelekea kwenye majonzi lakini hazitaleta maangamizi maana lipo saruhisho kuu linalo tumulika wakati wote mpendwa jibu la changamoto zako lipo katika  ( Ufunuo 5:1-10) "Kisha nikaona katika mkono wa kuume wake yeye aliye keti juu ya kile kiti cha enzi kitabu kilicho andikwa ndani na nyuma,kimetiwa muhuri saba nikaona malaika mwenye nguvu akihuburi kwa sauti kuu.N’nani astahiliye kukifungua kitabu,na kuzivunja mihuli zake? Wala hapakuwa na mtu mbinguni,wala juu ya nchi,wala chini ya nchi,aliye weza kukifungua hicho kitabu,wala kukitazama,nami nikalia sana kwa kuwa hapakuonekana mtu astahiliye kukifungua hicho kitabu,wala kukitazama,na mmoja wapo wa wale wazee akaniambia ,usilie;tazama,Simba aliye wa kabila la Yuda,shina la Daudi ,yeye ameshinda apate kukifungua kile kitabu ,na zile muhuri zake saba,nikaona katikati ya kile kiti cha enzi mwana-kondoo amesimama,alikuwakana kwamba amechinjwa,mwenye pembe saba na macho saba ,ambazo ni Roho saba za Mungu zilizo tumwa katika Dunia yote .Akaja akakitwaa kile kitabu katika mkono wa kuume wake yeye aliyeketi juu ya kile kiti cha enzi ,hata  alipo kitwaa kile kitabu hao wenye uhai wanne na wale wazee ishirini na wanne wakaanguka mbele ya mwana kondoo ,kila mmoja wao anakinubi na vitasa vya dhahabu vilivyo jaa manukato ambayo ni maombi ya watakatifu .Nao waimba wimbo mpya wakisema wastahili wewe kukitwaa hicho kitabu na kuzifungua muhuru zake ;kwa kuwa ulichinjwa ukamnunulia Mungu kwa damu yako watu wa kila kabila na lugha na jamaa na taifa ukawafanya kuwa ufalme wa makuhani kwa Mungu wetu;nao wana miliki juu ya nchi" soma zaidi kuna kitu cha ajabu sana kimejificha hapo pia ongeza ufahamu  kwa kusoma (Isaya 53 7;11:2;) (math 27;57)

     (Soma kwa makini maana milima huyeyuka mbele za bwana)
Ndungu maandiko yanaposema kuwa hapakuwa na mtu wa kukifungua kile kitabu na ile muhuri yake ila mwana- kondo ,simba aliye kabila la Yuda shina la Daudi yeye ameshinda ilikwamba apate kukifungua kile kitabu na muhuri zake ,inamaanisha kuwa wapo watu ulio waomba wakusaidie lakini inawezekana wameshindwa nawe umelia sana bila kuona msaada ,lakini hapa anakupa uhakika yakuwa yeye ndiye aliye shinda ili apate kuifungua ili muhuri sasa muhuri ni changamoto anazo pitia mwanadamu ,dhambi vifungo magonjwa ambayo mwanadamu anakutana nayo.

Mwenyezi Mungu baada ya kuona kwamba hakuna kitu kinacho weza kuwaokoa wanadamu na changamoto zao,ndiposa akaamua imwagike damu ya mwanae mpendwa ndiyomaana hapo juu anasema huyo mwana-kondoo alikuwa kana kwamba amechinjwa (na hicho ndicho kifochake bwana wetu Yesu kristo msalabani kinacho kupa uhakika wa muhuri za matatizo yako kuvunjika maana yeye ndiye anaye stahili na mwenye uwezo aivunjaye muhuri zote ,ina maana nikama vifungo vilivyo mfungwa mwanadamu) na ndio maana kwenye (ufunuo 12;11) anasema nao wakamshinda kwa damu ya mwana-kondoo na kwa maneno ya ushuhuda wao; ambao hawakupenda maisha yao hata kufa.”
Chakufanya ni wewe kufanya uamuzi sasa kutoka moyonimwako na kuamini  kwamba hakuna mwingine ataweza kukusaidia kwakuwa kama kuhangaika umehangaika sana vyakutosha ukifanya hivyo kwaimani hakika utatoa shuhuda zako juu ya hiki ninacho kwambia

  MAMBO YA KUFANYA BAADA YA KUSOMA NA KUELEWA VIZURI HAPO JUU

Kwanza unatakiwa kujua Kuwa ile hati ya mashitaka yaliyo kuletea wewe changamoto yalisha gongomelewa pale msalabani ,na ile hati ya mashitaka ndiyo yanayo elezwa katika (ufu 5 :1-10 )   na baada ya kifo chake msalabani ndipo Wokovu wawanadamu ulipitangazw rasmi na mashitaka yote yaka fungwa pale yameng'ang'aniwa na BwanaYesu (Wakolosai 2 ;14 )

v  Sogea mbele ya kiti chake cha rehema  na uutubie uovu wako na kujikabidhi kwake toka moyoni mwako ,unapo mpa moyo wako usiwaze changamoto zako wala kulia kutokana na uchungu ulio nao hapa jikaze mweleze tu Mungu uovu wako hatakama anaujua lakini yeye anasema njoni na tuhojiane ,yupo tayari kukusamehe (Isay 41 ;21),yaani wengine huwa wanachukulia suala la toba kama vile kamchezo fulani ,ndugu Mungu anataka kuona mtu anaye tubu na aliyekusudia kweli kutubu na  kuziacha, nisawa na mtu ikiwa anashida ya msingi sana huwa haileti picha nzuri anapo chukua simu yake na kumbipu mtu anaye fikiri kwamba anaweza kumsaidia zaidi anapaswa kumpigia ,mfano ;unapoomba nafasi ya masomo katika shule au chuo fulani huwa una mbipu mkuu wa shule au unapaswa kupiga?na ndio maana kwenye ufunuo 12 anasema ambao hawakupenda maisha yao hata kufa inamaana walio jitoa kweli na wanahitaji msaada kweli. 

v  Amini kuwa utakapo anza kumweleza changamoto zako atakusikia na atakujibu (Ebra 11;1-9).

v  Amini kuwa yupo karibu na wewe kwa asililia kubwa
v  Ondoa mawazo ya kutojibiwa au mawazo ya kwamba wenda hakusikii kwasababu sikunyingine umewai omba bali tambua ya kuwa leo nisiku nyingine

v  Unapo anza kumweleza usiisikilize sauti itakayo jitokeza ikikwambia unachoomba nisawa na bure ,au ikisema ha nawewe unaomba ?au ikisema huyo Mungu unaye mwomba unauhakika kuwa yupo? Nk ,Usizizikilize sauti za kipuuzi kama hizo wewe baki na wazo moja la ushindi kwa damu ya Mwana –kondoo  maana imeandikwa "...nao watamshinda kwa damu ya mwana -kondoo .."soma (ufunuo 12;11)

v  Sasa mweleze huku ukimsikiliza anacho kwambia mfano; akikwambia inua mikono yako juu basi unapaswa kutii au akikwambia ukawasemehe kwanza ulio wakosea basi fanya hivyo maana hapa atakupa ufungua husika ulio ambatana na upendo wake yaani damu ya Yesu maana damu ya Yesu ni upendo wa Mungu Baba kwa wanadamu au anaweza kama husikii kitu akikwambia basi endelea kumweleza ,usiache mpaka utakaoona una amani moyoni mwako .Roho mtakatifu akufundishe zaidi na Mungu aliye hai    akusaidie katika jina la Yesu kristo.Amina.
                           
                    E .mkinga
          


EmoticonEmoticon