MSAMAHA
UKITAKA KUPONA BASI SOMA TANGU MWANZO HATA MWISHO NA ULIFANYIE KAZI.
Wapendwa Bwana Yesu asifiwe , niwakati mwingine tena Mungu
ametupa kibali cha kujifunza sote neno lake kwa Roho wake mtakatifu atuongoze
tuweze kuya jua maandiko Amina , tunaendelea na mwendelezo wa somo letu la TOBA
NA MSAMAHA na sasa tunajikita zaidi katika msamaha.Ingawa nimetoa jingine linalotoa maana ya toba
Kabla ya kuangalia maana ya neno Msamaha,nataka ujue kuwa hapa nitazungumzia zaidi msamaha wa mwanadamu kwa mwanadamu mwenzake maana watu wengi wamefungwa kutokana na kuto samehe au kusamehe kwa kinywa tu,Mungu anakawaida ya kusemehe ,pia ili mtu apate msaada kiurahisi kwa Mungu basi ni lazima mtu huyu awe na moyo wa kusamehe Maana maranyingi Mungu humtendea mtu kulingana na mtu mwenyewe alivyo
Kabla ya kuangalia maana ya neno Msamaha,nataka ujue kuwa hapa nitazungumzia zaidi msamaha wa mwanadamu kwa mwanadamu mwenzake maana watu wengi wamefungwa kutokana na kuto samehe au kusamehe kwa kinywa tu,Mungu anakawaida ya kusemehe ,pia ili mtu apate msaada kiurahisi kwa Mungu basi ni lazima mtu huyu awe na moyo wa kusamehe Maana maranyingi Mungu humtendea mtu kulingana na mtu mwenyewe alivyo
Maana ya neno MSAMAHA ;maana yake ni kuachilia kile ambacho
kilikuwa kina kutesa moyoni mwako au ni hali ya kuweka huru maadui zako kwa
kuwaachilia toka moyoni mwako kwakuwa waliwekwa ndani ya moyo wako wakisumbua
moyo na ufahamu wa mtu kwa muda mrefu au mfipi. ninazungumza haya kwakuwa
ukisoma kitabu cha (MATHAYO 5;43-45 ),inazungumzia kwa habari ya upendo kati ya
mtu na mtu inasema."mmesikia kwamba imenenwa umpende jirani yako na umchukie
adui yako lakini mimi nawaambia wapendeni adui zenu waombeeni wanao waudhi ili
mpatekuwa wana wa Baba yenu ailye mbinguni”.
MPENDWA inawezekana kuna watu wamekuudhi sana sio kidogo wenda
walikusema vibaya au ni mume anakudharau au mke anakudharau ndoa ina sumbua kwa
hivi umejikuta una chuki na mwenzi wako na ukapata maumivu ndani ya nafsi yako
pole mungu yuko upande wako anacho taka ukubali kumuachilia huyo uliye mweka
ndani yako na hakika utajikuta umebadirika nasema hivi kwakuwa hata ukimuwaza
sana haita kusaidia na utaishia kuumia tu hebu msamehe toka moyoni pasipo
kumuwazia mabaya mungu atakubariki na utapona hakika nahata ukitaka kusamehewa
dhambi zako unapaswa kusamehe kwanza wenzako katika (MATHAYO 6;9-13) ina toa
kanuni za kusamehewa dhambi mstari ule wa 12 inasema “utusamehe deni zetu kama
sisi nasi tuwasamehevyo” wadeni wetu.
MSAMAHA PIA SIO TU
MWANADAMU KUMSAMEHE MWENZIO BALI HATA MUNGU ILI AWEZE KUKUSAMEHE LAZIMA WEWE
PIA USAMEHE WENZAKO HIHI NI KANUNI YAKE KATIKA (mathayo 6;12 );na hata (marko
11;25-26 )inasema “ninyi kila msimamapo na kusali sameheni mkiwa na neno juu ya
mtu ilina Baba yenu aliye mbinguni awasamehe na ninyi makosa yenu lakini kama
ninyi hamsamehe wala Baba yenu aliye mbinguni hata wasamehe ninyi makosa yenu.”
NDUGU UNAPASWA KUACHILIA MSAMAHA TOKA MOYONI MWAKO IKIWA NI
MCHUMBA WAKO ALIKUTAPELI MSAMEHE ULIPOWEKA CHUKI NDANI YAKO JUU YA MTU ALIYE
WAHI KUKUIBIA SAMEHE AU MCHUNGAJI WAKO ALIKUSEMA VIBAYA AU ULIWAHI BAKWA
UNAUCHUNGU MOYONI KUTOKANA NA JAMBO FULANI LILILO WAHI KUKU TOKEA MWACHIE YESU
UWE SALAMA MAANA PASIPO HIVYO UNAWEZA KUPOTEZA MAISHA YAKO AU KUDHOHOFIKA SANA
ACHA KUYA WAZA HAYO MAANA HATA UGONJWA WAKO ULIO NAO WENDA NI KUTOKANA NA
KUTOSAMEHE.Haijarishi amekukosea marangapi (mathayo 18;21-22 ),INAWEZEKANA HATA MUNGU WENDA
ULIWAHI MWOMBA LAKINI HAKUKUJIBU NA UKA MCHUKIA NA KUSEMA HAKUNA MUNGU EBU
MSAMEHE AU ULIWAHI TAMANI KUJIUA JISAMEHE MWENYEWE NA MUNGU ATAKUPA UHURU WA
KWALI
NB;Baada na kabla ya kutamkiana msamaha lazima kuwe na sala
maalum na baada ya kutamkiana pia lazima kuwe na sala au maombi maalum ya kuwatenga na
uadui katika ulimwengu wa kiroho.Na jambo hili linafanyika kwasababu mwenye kupatanisha ni Mungu kwa damu ya Yesu mwanae pekee ,kwahiyo baada ya ninyi kusameheana basi inafuata nafasi ya Mungu kuwasameheninyi kwani mlimuudhi pia na yeye ,kwakuwa ukimkosea Mwanadamu katika ulimwengu wa roho umemkosea na Mungu.na ikiwa haujui namna ya kufanya basi muone mchungaji au kuhani mwenye uelewa na hiki ninacho kizungumza maana wengine nao wanaamini kuwa mkisha sameheana ninyi basi inatosha kumbe msamaha unakuwa bado hauja kamilika,ni lazima kusemezana na Mungu wenu ili kila uumbaji utambue na kuachilia baraka zenu
HASARA ZA KUTO SAMEHE
- Nisawa na kunywa sumu hukuukitarajia afe mwingine na kumbe unajiua mwenyewe
- Kila mtu akikushauri kitu utaona kuwa anakuonea au kusingizia
- Magonjwa kama vile vidonda vya tumbo magonjwa ya ngozi moyo kuuma kichwa, kukosa nguvu za mwili na za kiroho, kuchanganyikiwa au kupotelewa na akili, uchovu wa mwili , kifafa kukosa usingizi kuuma kichwa msongo wa mawazo nk vinaweza kukuandama (zaburi 38;5-10)
- Hofu humwandama mtu hatakama hakuna jambo guma lakina mtuanakuwa na hofu hata mtu aki mwita anaweza kudhani labla ana muwazia mabaya
- Kushituka shituka hata pasipo adui
- Katopenda kuongea na watu yaanai kuwa mpweke
- Kuto penda kuoa au kuolewa
- Kutoa lugha chafu bila busara
- Ikiwa ni mja mzito mtoto anaweza kuzaliwa akiwa hana furaha
- Huondoa ufanisi wa kazi
- Nivigumu kuingia mbinguni
FAIDA ZA KUSAMEHE
- Mungu atakusamehe nawewe makosa yako .(mathayo 6;14-15)
- Nivigumu mungu kuipokea sadaka yako madhabahuni .(mathayo 5;23-24)
- Utawekwa huru mbali na vifugo vya adui
- Nirahisi kumsikia mungu asemacho au wewe kukutana na mungu unapomwomba
- Uchovu wa mwilimna roho huondoka
- Ufanisi wa kazizako huongezeka
- Mishituko ya ghafla isiyo na sababu hupotea
- Hayo maumivu ya kichwa yataondoka maramoja
- Utamfurahia na kumwinua mungu ya kuwa anaweza
- Baraka za mungu zitakuzukia
- Ndoa hupona maramoja na upendo mkuu utawavamia
- Yaweze kana wewe ni mzazi kuna mtotofulani humpendi baada ya kusamehe ependo utaridi
- Ikiwa umekata tamaa ya kuoa au kuolewa utaoa au kuolewa
- Ikiwa una swali zaidi karibu,Ingawa hap anime jaribu angalau kukupa vipande vichache vyamsingi Mungu akusaidie kukuelewesha katika Roho wake mtakatifu .Amina E.mkinga
EmoticonEmoticon