JE UNAJUA KUWA AINA YA MAISHA UNAYOISHI LEO NI MATOKEO YA MAMBO ULIYOYAFANYA JANA?
(Isome yote kwa tafakari mpaka mwisho ili upate kitu)
Wanadamu wengi wanapenda kuishi maisha ya kifahari kila
mmoja kwa wakati alionao ,nahii inatokana na ukweli wa ugumu wa maisha waliyonayo.inawezekana
na wewe ni mmoja ya watu wanaopenda kuwa na maisha ya kifahari au yenye
mafanikio makubwa ,lakini umejaribu njia mbalimbali lakini umajikuta bado
hufikii lengolako au inawezekana bado hujaanza kufanya jitihada fulani
zitakazokufanya uwenamaisha yakifahari
au ndio unaanza jitihada hizo lakini nataka tujifunze machache juu ya
hili,
Pole kutokana na hali hiyongumu unayoipitia,inawezekana wewe
ni mzazi au ni mfanya biashara au ni Mwanafunzu au kiongozi wa Mkoa au Nchi au
kiongozi wa Dini ,leo nataka nikufungue macho kwa ufupi katika jambomoja
litakalokusaidia ilikesho uwe mtu watofauti (mwenye bajeti ya kukutosha)
Watu wengi huwa wanakosea katika harakatizao za utafutaji
wengi wao wanajikita katika kutafuta kipato au chakula kinachoweza kuwasaidia
kwa siku hiyo hiyo hawaangalii zaidi namna watakavyo ishi kesho,nahii ndio
sababu ya kukuandikia makala hii ili unapoendelea na harakati zako uwe unajua
kuwa unatakiwa kujifunza kutafuta vitu vitakavyo kusaidia kesho kwakuwa mengi
ya leo umesha yatatua (akiba nzuri),hii itakusaidia wakati ukipata tatizo la
ghafla ,utaweza kulitatua kwa upesi na kutunza heshima yako
Aina hii ya maisha uliyo nayoleo ni matokeo ya mambo uliyo
yafanya jana .
(Amua kuanza maisha mapya kwa mtazamo mpya)
Mfano;
Mfano;
- Kwakuwa jana ulikamatwa na hatia ya wizi ,ikakupelekea leo kufungwa gerezan.
- Kwakuwa jana ulifanya kazi kwa uvivu,ikakupelekea leo uwe na majukumu mengi zaidi na umekosa muda wa kuyafanya mengine yamsingi
- Kwakuwa jana hukusoma kwa bidii,imekupelekea leo ufeli mtihali
- Mfanya biashara kulalakwako chini ya sakafu leo ,kumetokana na jitihada zako za jana kwenda kwa mganga wa kipepo kutafuta utajiri.
- Kwa kuwa jana ulijifanya tajiri wa milele ukashindwa kuwasaidia wenzako ,leo Yule uliye mdharau jana anashindwa kukusaidia wewe kwani uchumi wake umekuwa
- Kwakuwa jana ulitenda dhambi,imekupelekea leo ukapata magonjwa ambayo hata hayana majina au yana majina mabaya kama vile kaswende, au yana kivuli cha Taifodi,au mafua au kansa lakini kumbe sio kansa na wataalamu wanaigundua kama kansa halafu wanashindwa kuitibu,mpendwa kwani hujuikuwa ukitaka wanyama na ndege wote wakimbia shambani kwako ni lazima uweke sanamu ya binadamu?
- Kwakuwa jana hukuwakaribisha wateja kwa lugha nzuri,imepelekea leo huna wateja kwenye biashara yako
- Kwakuwa jana hukutimiza wajibu wako kama mwalimu ,ikapelekea leo ukatumbuliwa
- Kwakuwa jana hukuomba kwa bidii ,imepelekea leo shetani amekushinda
- Mlokole amani uliyonayo leo nimatokeo ya tukio ulilo lifanya jana la kumpa bwanaYesu maisha yako ili afanyike kuwa bwana na mwokozi wa maisha yako.
- Mchumba unayemtafuta leo ,ndio aina yamaisha yako yakesho
- Kwakuwa jana hukufanya uamuzi mzuri wa kuoa au kuolewa .leo unapatashida kwenye ndoa yako(lakini usiogope lipo jibu mtegemee Mungu).
- Kwakuwa jana hukujenga nyumba ,leo unaishi nyumba za kupanga
- Wazazi wako hawakuandaa mazingira mazuri ya kiuchumi ,leo wewe unahangaika
(Amua kuanza maisha mapya kwa mtazamo mpya)
Wazazi wako walitenda dhambi ,leo wewe unapata shida
kutokana na uovu wao ( Hes 14:18), na
(Kut 20:5-6),( si maanishi ukapige kwafimbo kaburi lao kama walifariki au uka
wazoza kama ni wazima usifanye hivyo kwani utakuwa una haribu zaidi maisha yako
ya kesho au watoto au kizazi chako)
Kwakuwa jana uliokoka, leo
huna mapepo
Kwakuwa jana ulimpa Yesu maisha yako ,leo unakibali cha
kuingia mbinguni
Kwakuwa jana ulifanya kazi kwa bidii leo unachakula chakutosha
na uchumi wako umeongezaka.
Mpendwa amani unayoiona leo nikwasababu ya mambo fulani
yaliyo fanyika jana(kuna watu walio kaa chini na kutunga sharia za nchi
ilikutunza amani , na wewe leo una amani hata una muda wa kucheka ,wengine walipigania
kwa vitavikali ili kusababisha amani ,ingawa wengi wao hawakufaidi amani hiyo
bali watoto wao ndio walio faidi
Na kuna wengine wana huzuni leo kwasababu kuna jambo
lilifanyika jana,namaanisha matokeo ya afya yako ya sasa ni kutokana na
ulichokifanya masaa kadhaa yaliyopita,unachotakiwa kukifanya ni kubadili mtazamo wako usiangalie aina ya
maisha unayoishi leo bali jiandae na jinsi utakavyoishi kesho kwani leo imeshapita
,na unapoiendeasiku nyingine hakikisha hauna deni lisilo lalazima litakalo kufanya kesho ulikumbuke na kufikiri
kulilipa hii itakusaidia kuwa na amani moyoni mwako.
Kumbuka ukitaka watoto au kizazi chako cha baadaye kiishi
maishamazuri basi weweleo ndio wa kukiandalia mazingira (ndio maana watu
wanawaona wazungu kama watu waliofanikiwa sana kumbe ni kwasababu wao walisha
tambua hili mapema).
NB,usiandae vitu hatari kwaajili ya kuvitumia kesho,mfano ;utakuta
watu au Nchi fulani zinaandaa mabomu na siraha kwaajili ya vita hii sio jambo zuri
,maandiko yanasema auaye kwa upanga atakufa kwa upanga
Anza leo kuandaa maishayako yakesho, ikiwa unataka kesho uwe
vizuri kiroho basi anza leo kutubu juu ya uovu wako ,ukitaka kesho uwe na uchumi mzuri basi anza kufanyakazi leo kwa bidii ,usitumie
rasilimali zako vibaya hata kama hauna uhitaji wa kuzitumia kwani utakapokuwa
na uhitaji itakiwa imesha haribika au imepungua ubora wake ,ukipata pesa leo
sio lazima utumie zote leo bali wekaakiba hata ya miaka hamsini ijayo ,jenga
mwili wakoleo kwa kutumia vyakula vyenye virutubisho na kufanya mazoezi ili
kesho uwe na afya njema
(Amua kuanza maisha mapya kwa mtazamo mpya)
(Amua kuanza maisha mapya kwa mtazamo mpya)
NB; Asilimia kubwa ya matatizo yanayo jitokeza leo hayajatokana
na sababu za leo bali ni matokeo ya jambo fulani lililo anzia masaa machahe
yaliyopita au miaka iliyopita au miezi iliyopita ,mbu anaye kung’ata leo
malaria utayapata kesho.haya ni baadhi tu ya mawazo yanayo kualika kufanya maandalizi mapema yatakayo
kusaidia kujenga mafanikio yako ya kiriho
na kimwili .Mwenyezi Mungu akubaliki ,lindasana moyo wako kuliko vyote
uvilindavyo maana ndiko zitokako chemichemi za uzima wa milele.
(Mtazamo huu kama umeupenda uutumie)
E.Mkinga.
E.Mkinga.
EmoticonEmoticon