Sunday, 8 October 2017

MATENDO KATIKA IMANI (UHUSIANO KATI YA IMANI NA MATENDO)

Tags



MATENDO KATIKA IMANI ( UHUSIANO KATI YA IMANI NA MATENDO )
                  (ijue Imani halali iletayo  mafanikio halali)
Mpendwa wangu ninakusalimu katika jina la Bwana Yesu aliye hai ,natumaini wewe ni mzima na sio uzima ule wabandia utokao kuzimu bali niule original kutoka kwa BwanaYesu ,lakini ingawa ninatambua yakuwa wengine wanauzima bandia kutoka kuzimu ambao baada yamuda mfupitu watapata shida na hata mlango wakuingia mbinguni utakuwa umefungwa kwao kwakuwa kimsingi hawatambuliki katika kitabu cha walio mkubali Yesu bali katika kile cha waasi .Pia kwao hao nafasi iwazi Yesu anawahitaji maana anawapenda,kwa upendo wa agape. 

Siku ya leo natamani tujifunze kwaufupi  juu ya IMANI maana yake ,na ili imani iweze kutenda kazi nifanye nini ? kwa maana imani niufunguo wa mambo mengisana na hii ndiyo inayo takiwa yaana (IMANI ILETAYO MIUJIZA).

IMANI, neno hili lina maana yake kibiblia ukisoma ( Waebrania 11;1-2 ) "Biblia inaanza kwakusema Basi Imani nikuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo ni bayana ya mambo yasiyo onekana ,maana kwa hiyo wazeewetu walishuhudiwa".Hii ni maana ya imani kibiblia lakini kikawaida kilamwanadamu anayo imani lakini inatofautiana nayamwingine na inawezekana wote wakawa na imani lakini sio kamahi ya Waebrania 11, na niwachache tu wenyenayo hii ya kwenye andiko hili ambayo ndiyo kusudi la Mungu kwa mwanadamu sasa nataka nawewe mpendwa Mungu akujalie imani hii ya Ebrania 11

                                 AINAZA IMANI

Maranyingi nimezoea kutenganisha hali hizi kama aina za imani kwakuwa ndizo zinazo leta tofauti baina ya moja nanyingine kiutendaji kamatulivyoona hapo juu maana ya imani hiyo ni kwaujumla na aina hizo za imani nihizi.

• Imani ya kumwamini Mungu pasipo kumwamini Yesu kristo 
• Imani ya kumwamini Mungu na uwepo wa Yesu kristo
• Imani ya kumwamini shetani 
• Imani ya kumwamini Mungu na shetani 
• Imani ya kuliamini dhehebu au dini na kumpinga Mungu (pasipo kujuwa) nk
Nimezigawa ainahizi ili uweze nielewa vizuri

IMANI YA KUMWAMINI MUNGU NA UWEPO WA YESU KRISTO
             (ijue Imani halali iletayo  mafanikio halali)
Hapa mtu anakuwa anaamini yakuwa Mungu pekee ndiye mweza na hufanya kazi na jeshi lake lote (utatu mtakatifu) Mungu Baba ,mwana na Roho mtakatifu sasa tunaweza kusema kuwa imani hii ya kumwamini Mungu na utendaji wa mwanae Yesu kristo hili ni kusudi la mungu kadiri ya maandiko (WARAKA 1 WA PETRO 2:6-7 )maandiko yanasema “kwakuwa imeandikwa katika maandiko Tazama naweka katika sayuni jiwe kuu la pembeni ,teule ,lenye heshima na kila amwaminiye hatatahayarika” (Kwaufupi jiwe ni Yesu kristo ) pia ukisoma (WAEBRANIA 3:12-13) ina sema “Angalieni nduguzangu usiwe katika mmoja wenu moyo ,mbovu wa kuto kuamini kwa kujitenga na mungu aliye hai” .Mpendwa hapa wanadamu hujitenga kutokana na uovu wao kuwaheshimu waganga wa kipepo kuogopa wanadamu badala ya Mungu kupinga ubatizo wa Roho Mtakatifu na kushadadia ubatizo wa majipekee ,Kuenenda katika kimwili katika kuyatafakari mambo ya Mungu na uweza wake ,Kufifisha uweza wa Mungu na mamlaka yake ndani ya wanadamu haya nibaadha yanayo dhihirisha kuwa mtu hamwamini Mungu hatakama anasali kilasiku au ni mchungaji au ministranti au padre au papa nk ikiwa unaitegemea nguvu nyingine zaidi ya Mungu kupitia Yesu kristo basi wewe ni msindikizaji hivyo chukuwa hatua maana imani huja kwa kusikia neno la Mungu kama hililina lo hubiriwa ,

 pia ukisom katika (YOHANA  6 :28-30) hapa Yesu aliulizwa .”Basi wakamwambia tufanyeje ilitupate kuzitenda kazi za Mungu” Yesu akajibu akawaambia “hii ndiyo kazi ya Mungu mwaminiyeye aliye tumwa nayeye”.maandiko haya yanamwelekea yeye mwanyewe yaani Mungu mwenyewa anahitaji watu wamwendee kupitia Yesu kristo ukisoma (Yohana 6;35) Yesu akawaambia mimi ndimi chakula cha uzima Yeye ajaye kwangu hataona njaa kabisa naye aniaminiye hataona kiu kamwe,lakini naliwaambia yakwamba mmeniona wala hamwamini wote anipao Baba watakuja kwangu walayeyote ajaye kwangu sitamtupanje kamwe” 
             (usikate tamaa endelea kusoma nawe utaimarika)
Mpendwa yapo maandiko mengi yanayo thibitishaya kuwa Imani ya kweli ni ile ya kumwamini Mungu katika Jina la yesu maana utendaji kazi wamungu umeambatana na Sadaka ya Yesu msalabani kwahivi lazima yesu ahusike ndio maana hata katika maombi alisema amwombaye Baba aombe kwajina lake Yesu ili apewe .hatawale mitume aliwasisitiza sana suala la imani akasema ukiwanaimani hata ikiwa kama chembe ya haradali utaweza kuuambia mlima uhame mahaliulipo nao utakutii Sasa je wewe umewahi kuuambia mlima uhame nao ukakutii?(mlima ni vikwazo katika safari ya imani ya watakatifu wa duniani) unaumwa miaka yote unaomba likini huponi ,mwingine ni mtumishi wa mungu huduma yake bado haioneshi yakuwa inaongozwa na Mungu aliye hai HEBU JICHUNGUZE UNAMICHANGANYO?. WEMGINE WANAENDAKWA WAGANGA WA KIPEPO KUOMBA MSAADA WAKIPATA WANASEMA MUNGUAMEWASAIDIA HALAFU WANATOA HADI SHUHUDA KWA WATU WA MUNGU ALIYE HAI HAWAJUIYA KUWA WANAJIAIBISHA TU KWAHIVI WAO HAWAJUI YA KUWA MBINGUNI HAWAINGII WALIO NA IMANI YA UDHAHIFU (MICHANGANYO).
Maandiko yanasema mbinguni hakitaingia kinyonge ,pia katika Ufunuo wa yohana maandiko yanazungumza kitu cha ajabu sana  anasema nawasio amini hawataingia uzimani .Mpendwa ni jukumu lako kumwamini mungu na uweza wake ,kumtegemea maishani mwako acha woga haya yote yuanawezekana ukimpayesu maishayako maana Biblia inasema IMANI HUJA KWA KUSIKIA NA KUSIKIA HUJA KWANENO LAKE KRISTO .
Sasa je wewe umelisikia na kuliamini neno la nani ?la mchawi wako?,mganga wa kipepo au umeliamini neno la Yesu kristo na kulifanyia kazi? Kumwamini Mungu kupitia mwanaye Yesu kristo na kazi zake azitendazo,bila kuwa na tegemeo jingine ,hii ndiyo imani itakayo weza kumwonesha mwanadamu njia sahihi ya mbinguni na kumpa ushindi akiwa duniani This is super faith or stong faith or powefull faith which have the ability to overthrow the mountains. As it was done to the Israelites at the sham by Moses

Pia unaweza kusoma,( MATHAYO 14:31) (MARKO 5:25-33) (MATHAYO 17:14-18) (MATHAYO 21:21-22) Mwanadamu anazaliwa bila imani na akiwa duniani anaposikia nakujifunza mambo mbalimbali imani huanza kujengeka inamaana imani uliyonayo ni matoko ya mazingira yako uliyonayo .Sasa ninakueleza juu ya  kuwa matendo katika imani nikimaanisha kuwa kila imani inamatendo yanayohusika na imani hiyo, na pasipo matendo hayo basi imani hiyo haiwezi kuwa na matunda ,ukisoma (YAKOBO 2:14-20 ) 14 “Nduguzangu yafaa nini mtu akisema yakwamba anayo imani lakini,hana,matendo?Je ile imani yaweza kumwokoa? 15 ikiwa ndugu mwanamume au ndugu mwanamke yu uchi na kupungukiwa na ridhiki 16 na mtuwakwenu akawaambia Enendeni zenu kwaamani mkaotemoto na kushiba lakini asiwape mahitaji ya mwili yafaanini?17 vivyo hivyo na imani isipokuwa inamatendo imekufa nafsini mwake18 lakini mtu atasema wewe unayo imani, namimi ninayo matendo.Nioneshe imaniyako pasipo matendo nami nitakuonesha imaniyangu kwanjia yamatendo yangu 19 wewewaamini yakuwa Mungu nimmoja;watenda vema masheteninao waamini na kutetemeka 20 lakini wataka kujua wewemwanadamu usiyekitu,kwamba imani pasipomatendo haizai?.

 Mpendwa utakuta unapo endelea kulisoma eneo hili hata mistari ya mbele yake ana shuhudia yakuwa hata Baba yetu Ibrahimu alihesabiwa haki kwa matendo yake  ndiposa imani yake ilipofanya kazi .kwahiyo ikiwa wewe ni mmoja ya wele wanao mwamini Mungu aliye hai na mwanae Yesu kristo basi yafanye matendo yapatanayo na imani hiyo yaani kujitahidi kuzitenda  amri zake mfano ,USIUE, USIABUDU MIUNGUWENGINE, USIZINI USIMSHUHUDIE JIRANI YAKO UWONGO ,USIWAZE UCHAFU UKAUTAFAKARI HUO BADALA YA MUNGU,HESHIMU WAZAZI WAKO KUMBUKA KUIHESHIMU NA KUITAKASA SIKU YA BWANA MUNGU NK
. Baada ya kuyatenda haya na mengine yafananayo yaliyo mema nakuhakikishia utamwomba Mungu naye atasikia na kukujibu ,Utakapo fanya lolote lililo jema hakika litazaa matunda na kila utakacho kifanya kitafanikiwa ,kwakuwa yeye amesema utafuteni kwanza ufalme wa Mungu na haki yake nahayo mengine utazidishiwa .
           (endelea kusoma kwa kutamani kujifunza na kubadilika)
FUNGU HILI LA IMANI AINA HII YA KWANZA NDIO LENYE NGUVU KULIKO YOTE DUNIANI NA MBINGUNI YAANI KUMWAMINI MUNGU BABA ,MWANA NA ROHO MTAKATIFU, UKITIA SHAKA JUU YA UMOJA HUU BASI LAZIMA IMANIYAKO IWE NA KUTU, MUNGUAKUSAIDIE  
                                                                                         MPENDWA MARANYINGI KATIKATI YA CHANGAMOTO AU JARIBU NDIPOMTUANAPOWEZA KATATAMAA NA KURUHUSU HOFU MFANO MTUANAPOONA ANAKEMEA PEPO ALIANZA VIZURI NA ANAPOENDELEA AKISIKIA PEPOAMEANZA MATUSI NA ANA FICHUA UOVU WAKE MKEMEAJI BASI ANAINGIZA HOFU NINACHATAKAKUSEMANI KWAMBA UKIWAKWENYE PITO BASI CHA KWANZA
.                  

            (ijue Imani halali iletayo  mafanikio halali)   
PAMBANA NA ROHO YA HOFU NA MASHANA AU KUTO KUWANA UHAKIKA MAANA HIYO NI SIRAHA ANAYOITUMIA SHETANI KULETA MAANGAMIZI inawezekana ndugu zako mchumba au mke au mwajiri anakutisha kwajambo fulani na linakuletea hofu ya maisha kiroho na kimwili nakushauri kuwa wewe amini uwezo wa Mungu aliye mkuu zaidiyakeanaye kutisha , ikiwa wanakuonea Basi Mungu atajitukuza kwakuwa ulimwamini tangu mwanzo lakini usifanye maigizo ya imani hii ikiwa huyatendi mapenzi ya Mungu Itakula kwako Maana katia ya vitu vikumbwa ni imani ya namna na matendo yake hii na ndiyo inayo mtesa ibilisi usiku na mchana hata sasa .Hebu tamani uwenayo maana hata Bwana Yesu alisema unapoomba omba kwa Mungu kupitia jina lake na uamini yakuwa umesha ya pokea uliyoomba niyakwako na ndiposa yatakapo jidhihirisha katika ulimwengu wa nyama

IMANI YA KUMWANINI MUNGU PASIPO KUMWAMINI YESU KRISTO

Hii ni aina ya imani ambayo baadhi ya wanadamu wanayo ,wao wanajua ya kuwa hakuna mwingine ila Mungu tu ndiye anaye shahili kumwamini ,pia husema au huamini yakwamba hawawengine kama vile Yesu ni wanadamu tu na wana amini kuwa hakuna  Roho mtakatifu  ,Huu ni mtazamo wao na ndivyo wanavyo amini .

kwaufupi imani hii haina uwezomkuu kwakuwa Mungu ili amkomeshe shetani ali amua kumtumia Yesu afe msalabani kifo cha aibu tena kutemewa mate na kuvuliwa nguo mbele za watu pia kwaku imwaga damu kama sadaka ilikuukomboa ulimwengu na maandiko yanasema Kwamaana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu hata akamtoa mwanawe pekee ili kila mtu amwaminiye asipotee bali awena uzima wa milele maana Mungu hakumtuma mwanaye ulimwenguni iliauhukumu ulimwengu bali ulimwengu uokolewe katika yeye ,amwaminiye yeye hakuhukumiwa;asiye amini amekwisha hukumiwa;kwasababu hakuliamini jinala mwana wapekee wa Mungu .Kwahivi shetani anapo sikia jina la Yesu ndio kiboko chake milele.na umoja huu wa utendaji kazi wa Mungu haukuanza mwaka 2017 bali tangu uumbaji walikuwa wana fanyakazi kwaumoja kwahiyo lazima uamini Mungu na jeshilake la utendaji

IMANI YA KUMWAMINI SHETANI

Hii ni aina ya imani ambayo wanadamu humwamini shetani na wanafanya yampendazayo ,kuna wengine wana fanya pasipo kujua kuwa wanamtumikia shetani ingawa hawataki lakini wapo wale wanao mwamini na kutoa shuhuda kwawatu juu ya uweza wa shateani.

kwaufupi imani hii nayo wala haina ukuu kama ile ya kwanza ya kumwamini Mungu na jeshi lake yaani, Baba ,Mwana na Roho mtakatifu, hii ni kwasababu shetani ni mkuu wa giza na alitupwa kuzimu baada ya ile vita kuu ya mbinguni kwakuwa alikosa nidhamu mbinguni ,hakutaka kumtii Mungu na ndicho kilicho mponza na akatupwa na malaika waliokuwawana ya kubali mawazoyake nao ndio leowanaitwa mapepo majini mizimu nk na wanafanya kazi Duniani  kwahivyo wakaendelea kuwadanganya watu wa Mungu nao ndio wanao mwabudu na kumwamini (wamwaminio),ingawashatani alishashindwa vita ile,kwahiyo hata kama akitafuta kuwatesa mwanaomwamini Mungu na jeshi lake lazima atashindwa kwakuwa Alisha nyang’anywa ufunguo wa mamlaka na kafara kuu izidiyo kafara zote ilisha tolewa

 (UFUNUO WA YOHANA 12:7-12 )Kulikuwa na vita mbinguni;Mikaeli na malaika zake wakapigana na Yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake ; nao hawakishinda wala mahalipao hapakuenekena tena mbimguni ,Yule joka akatupwa Yule mkubwa joka wa zamani aitwaye ibilisi na sheteni audanganyaye ulimwengu wote akatupwa hata nchi namalaika zake wakatupwa pamoja naye ,nikasikia sauti kuu mbinguni ikisema sasa kumekuwa wokovu na nguvu na ufalme wa Mungu wetu na mamlaka ye kristo wake, kwa maana ametupwa chini mshitaki wandugu zetu yeye awashitakiye mbele za Mungu wetu usiku na mchana nao waka mshinda kwa Damu ya mwana kondoo na kwa neon la ushuuda wao”mpendwa Mungu ndiye aliye shinda vita hivi na akafanikiwa kuwatetea watotowake kwa Damu ya mwanae Yesu kristo  ndiposa shetani naye alipowekewa sikuyake ya kuangamizwa milele baadaya udanganyifu wake huu (UFUNUO 12;12) “Kwahiyo shangilieni enyi mbingu nanyi mkaao humo,ole wan chi na bahari kwamaana Yule ibilisi ameshuka kwenu mwenye ghadhabu nyingi , akijua ya kuwa anawakatimchache tu”,haleluyaaa .

kwahiyo mpendwa  ikiwa nawe unaamini imani hii ya shetani badirika maana siku ya mwisho usije kuangamizwa na huyo unaye mwamini (shetani),anaye fanya kazi kupitia wachawi waduniani na waganga wakipepo nk,maana yeye amepangiwa siku yake ya kuangamizwa mileleMungu anakupenda kupitia mwanaye Yesu kristo njoo kwake nawe utakuwa huru
Tutaendelea
     
             E.mkinga


EmoticonEmoticon