Sunday, 8 October 2017

JIWEKE HURU KWA NJIA YA TOBA NA MSAMAHA.

Tags



                             TOBA NA MSAMAHA.


             (Huu ni mwendelezo wa lile somo tulilojifunza mwazoni la msamaha,sasa hili ni la toba ).


Mpendwa wanadamu wengi nyakati hizi wanaishi katika hali ya maumivu mengi sana. leo nataka tujifunze kwa ufupi juu ya TOBA NA MSAMAHA vina wezaje kubadiri maisha ya mtu yaliyo jaa majonzi .

KWA KAWAIDA WANADAMU TUNAISHI KATIKA MAZINGIRA YA UOVU ULIO KITHIRI KATIKA DUNIA HII NA HII NI KWASABABU DHAMBI NI TAMU LAKINI MATOKEO YAKE NI UCHUNGU UHARIBIFU MAJONZI NA MAHANGAIKO .
( mwanz 3;1-19 )ukisoma maeneo haya uta shuhudia namna dhambi ilivyo tendwa na Adamu na mkewe Hawa walifurahia uzuri wa lile tunda lakini matokeo yake wakajitenga na uso wa Bwana wakapata majonzi mawazo na mashaka juu ya uovu walioutenda na baada ya pale vizazi vingi vikaishi katika uovu na namna yoyote ya upatanisho iliyo fanyika haikuweza kuridhishwa na Mungu milele .Ndiposa mtu mmoja ilipaswa kujitoa kwaajili ya kumkomboa mwanadamu na dhambi zake maana mwanadamu alikuwa amejitenga kwakiasi kikubwa na Mungu wake ndiyo maana anapata shida hatakumwona Mungu wake katika maisha yake.sasa nasi leo tunaanza na maana ya maneno haya mawili TOBA NA MSAMAHA

TOBA (repentance) Hii ni hali ya kujutia makosa yako kutoka ndani ya moyo wako au kutoka katika vilindi vya moyo wako kwa kukusudia kuacha uovu huo kwakugeuka kutoka katika utendaji ule wa kiovu ,ambayo ita badirisha au itapelekea maisha yako ya kiroho na kimwili kubadirika ,HII NI YA MTU BINAFSI NDANI YA MOYO WAKE na KUMBUKA HAUWEZI KUFANYA TOBA PASIPO UOVU ULIOPO (DHAMBI) je dhambi ninini? Nikwenda kinyume na utaratibi uliowekwa au ni kuvunja utaratibu fulani kwa kujua au kutojua (KOSA) Mungu aliweka utaratibi wa namna ya kuishi utaratibu ambao hauta muudhi mwanadamu yeyote au Mungu mwenyewe maana husababisha kutokuwa na amani kuu (PARADISO) kwamfano; Mungu alisema usiue lakini wewe ukiua inamaana utakuwa kinyume na utaratibu na matokeo yake utakuwa mtu wa mahangaiko pasipo amani (mwanzo 4;8-15),mtuanaweza kuua kwelengo zuri la kuboresha maisha yake (KUUA KICHAWI ) Lakini hatakama analengo zuri (katika macho ya kibinadamu),kwakuwa yupokinyume na sheria iliyowekwa tena sio ya mwanadamu bali nisheria yaMungu mtuhuyu hatakuwa na amani kwakuwa ile damu inamfuatilia katika ilimwengu wa roho yeye pasipo kujua ndio maana utakuta mtu anaota ndoto mbaya ana mwona yule mtu aliye mwuua hatakama alikuwa mtotodogo akiwa tumboni utakuta anamtokea au wanamtokea ndotoni au mtuhuyu anaweza hata kupagawa nawengine utakuta wanaishi maisha kama vilemazuri lakini hatakama ni tajiri lakini hana amani hata  mbali na utajiri wake akili hata haitulii ,kumbe ni matokeo ya uovu (umwagaji wa damu isiyo na hatia.
          (endelea Soma katika roho na kweli)
Mpendwa  kuua kupo kwa namna nyingi wenda kwa upanga .kuloga kuua kwa maneno yaani kusema maneno yanayo leta maumivu ndani ya mtu na akafa kimwili au kiroho .dhambi au makosa mengine ni kama vile wizi.ulevi uzinzi.urafi.kuwaza mabaya kupenda kuona mabaya uongo uchawi hasira na nyingine nyingi
.
MPENDWA IKIWA UMETENDA KOSA DAWA YAKE NI TOBA NA SIO KUVUNJA DAWA YA DHAMBI NI TOBA YA NDANI NA MUNGU YUKO TAYARI KUSAHEHE WAKATI MTU AMEKUSUDIA KUACHANA NA UOVU WAKE NA KUYAANZA MAISHA MAPYA , KUTOKANA NA TOBA HIYO YALE YOTE YALIYO MPATA KUTOKANA NA DHAMBI HUONDOKA KWAKUWA HAYANA KIBALI TENA CHA KUMWANDAMA

Karibu mpendwa jibu ni yesu pekee zaidi yake hapana mwangine damu yake inanena mema kuzidi unavyo isikia na kuielewa damu hiyo imeambatana na mema mengi juu yako na lengo kuu la damu hiyo ni kufanya ukombozi wawanadamu wote na dhambi zao kwa kila kabira na rangi zao Yesu yu karibu nawe umemuuthi yatosha chukua uamuzi wa kurudi kwake nuia moyoni kutubu ukifikiri juu ya utajiri wako kwakuwa ulipata kwanjia isiyo halani na ukaendelea hivyo maandiko yanasema haujui mudawako au saa yako iliyo pagwa kuachana na dunia
.
SEMA MANENO HAYA KWA IMANI TARATIBU KWA TAFAKARI YA MOYONI. MUNGU BABA NINAKUJA MBELE ZAKO MIMI NI MWENYE DHAMBI KWA DAMU YA YESU NAKUOMBA UNISAMEHE NA KUNIONDOLEA HATIA HII YA DHAMBI INIFUATIAYO MAISHANI MWANGU KWA DAMU YA YESU NISAMEHEWE UOVU HUU MKUBWA([waweza taja kimya kimya uovuwako hukuuki nuia kuuacha 
)
KWA DAMUYAKO BWANA YESU ILIYO MWAGIKA PALE KARIVALI ASANTE BWANA WANGU KWA REHEMA ZAKO NIWEZESHE KUTEMBEA SAWASAWA NA MAPENZI YAKO AMINA .

Baada ya kuamua kutubu kutoka moyoni ndiposa mtu anaongozwa sala ya toba(sala ya maungamo) kwakumuwekea mikono kama vile Anania alivyo fanya kwaSauli,ingawa Mungu alikuwa anaweza kumaliza kila kitu pale njiani lakini kwakuwa maskani ya Mungu ni pamoja na wanadamu kwasababu amewachagua wanadamu kama makuhani wanao  fanya kazi yake kama walivyo agizwa na BwanaYesu mwanaye,hapa hawa watumishi wanalo jukumu la kuwasaidia kukiri maneno ya kuutubia ule uovu (kuungama),kwahiyo hapa atakaye kuwa anaungama yaani kuhalalisha kosa alilo tenda ili aombewe akiongozwa na mtumishi wa Mungu kama alivyo saidiwa Sauli na Anania(mdo 9;1-17)
Hii ni namna fulani tu ya kujionesha kwa makuhani ambayo inampa mtu huyu ushirika na jumuhia ya Mungu ili asitengwe kwani kuhani ameshuhudia nia yake ya toba na kumpa ushauri na kumsaidia hata kimaombi kwa maana kazi ya kuhani ni kupeleka mbele za Mungu shida za watu,ingawa pazia lili pasuka na kutoa ruhusa ya kila mwanadamu kuwa na uwezo wa kwenda moja kwa  moja kwa Mungu na kusema shida yako,Lakini bado Mungu  anaendelea kutumia watumishi wake kwaajili ya kuwatoa magamba katika macho yao wale wasioona ambao hata hawawezi kusegea mbele ya kiti cha rehema kwaujasiri ,mtumishi wa Mungu anamsaidia kumuunganisha roho yake na Mungu ,yaani anamsaidia kutambua na kukiri kosa ili kutubu  kutubu ni kazi ya aliye tenda dhambi bali kuungama kuhani anaweza kuhusika iliwaweze kumjua vema na kuunganika vema na Mungu kwa maombi ya kuhani  na maongozi yake, kwani mtu anaweza kuwa amechakaa sana kiroho na hawezi hata kujua afanye nini ili Mungu amsaidie  (Isaya 43;8),ndipo mtumishi anasimama kwaajili ya kumsaidia ,ingawa kuhani mkuu ni Yesu mwenyewe lakini kwakuwa Mungu alitambua kuwa kutakuwa na wengine ni viziwi na vipofu kiroho wanao hitaji msaada wa kutolewa magamba,kupitia kuwekewa mikono,sauli alipo anguka bale barabarani Mungu Alisha kamilisha msamaha,lakini ilitakiwa apatikane kuhani ili atoe malipizi,ambaye alikuwa Anania

Ndio maana utakuta mtumishi wa Mungu ana mwombea sala ya maungamo ilikukamilisha toba aliyoifanya moyoni  kwa mtu aliye tayari kurudi kwa Yesu ,kitendokile cha kutubia maovu yake tena mbele za watu wengi au mmoja  kina saidia kufifisha uwezo wa dhambi na kuona aibu kuitenda tena  kwa kuwa mtu anakuwa anajiweka wazi kisha anakuwa huru nafsini mwake ,lakini kitu cha kwanza lazima mtu atubie uovu wake moyoni mwake ,kwani hatakama mtumishi wa Mungu atamsaidia lakini ndani ya mtu huyo kama hakuna mzigo wa kutubia uovu wake nisawa na bure,na hatakama mtu akasema nimetubu dhambi zangu lakini hakwenda kutolewa magamba kupitia  kuhani ambaye Mungu anamtumia,mpendwa kamahili halina umuhimu basi Anania asinge takiwa kuonana na Sauli kwaajili ja kujieleza shida yake eti kwasababu Alisha kutana na Yesu pale njiani .

Ndio maana kuna makanisa mengine yana shutumiwa kuwa kwanini watu wana tubu dhambi zao kwa mwanadamu ,ikiwa kuna watu au makanisa yanayo fanya hivi bila kuzingatia maana ya toba na kuungama basi waumini wote wa  kanisa hilo watakuwa na magambamachini mwao , ingawa kuna makanisa mengine yanaonewa kwakuhusishwa kwenye suala la kutubu kwa kuhani  jambo ambalosio kweli maana watu wengi wana shindwa kutofautisha kati ya toba na kuungama ,mpendwa toba inafanyika rohoni mwamtu lakini kuungama ndio ile mchungaji anamsaidia kumpamwongozo juu ya uovu alio utenda na Msamaha wa Mungu  ndani ya mtu  au mtu anapo kwenda kwa padiri ina maanisha mtu anakwenda kuungama (kujionesha kwa kuhani kwamba amerudi kundini na kazi ya kuhani maana yake anampa malipizi sawa sawa na Roho mtakatifu anavyo mwongoza .na kumwonya ili aianze safari upya.barikiwa
( lakini usiache kwenda kanisani kujumuika na wenzako wampendao Mungu katika jina la Yesu .Amina
                        E.mkinga
Top of Form


EmoticonEmoticon