KITAKACHO TOKEA SIKU
YA MWISHO PARAPANDA YA BWANA ITAKAPOLIA
(1KORINTHO 15;50-58).Maandiko yanaweka wazi juu ya siku ya
mwisho parapanda ya Bwana itakapolia maandiko yanasema "ndugu zangu nisemayo ni
haya ya kuwa nyama na damu haziwezi kuurithi ufalme wa Mungu; wala uharibifu
kuurithi kutokuharibika angalieni nawaambia ninyi siri; hatuta lala sote
tutabadilika kwa dakika moja kufumba na kufumbua wakati wa parapanda ya mwisho maana
parapanda italia na wafu watafufuliwa wasiwe na uharibifu nasitutabadilika
maana sharti huu uharibikao uvae kutokuharibika nao
huu wa kufa uvae kutokufabasi huuuharibikao utakapovaa kutokuharibika nahuu wa
kufautakapovaa kutokufa hapondipo litakapokuwa lile neno lililoandikwa
mautiimemezwa kwa kushinda kuwapiewe mauti kushinda kwako? uwapi ewe mauti
uchungu wako ? uchungu wa mauti ni dhambi na nguvu za dhambi ni torati lakini Mungu na ashukuriwe atupaye kushinda kwa Bwana wetu Yesu kristo ,basi
nduguzangu wapendwa mwimarike msitikisike mkazidisana kutenda kaziya Bwana
sikuzote kwakuwa mwajua ya kwamba taabu
yenu siyo bure katika Bwana."
KANUNI KUU YA KUINGIA
MBINGUNI NI MATENDO MEMA
(ufunuo 14;13) yohana katika mafunuo akaambiwa kanuni ya
kuingia mbinguni inasema "nikasikia sauti
kutoka mbinguni ikisema ,Heri wafu wafao katika Bwana tangu sasa Naam asema
Roho wapate kupumzika baadea ya tabu zao kwakuwa matendo yao yafuatana nao."
Ukisoma katika kitabu cha (ufunuo 20;11-13) ,inasema "kisha nikaona kiti cha enzi ,kikubwa cheupe
nayeye aketiye juu yake ambaye nchi na mbingu zikakimbia uso wake ,na mahali pao hapakuonekana,nikawaona wafu
wakubwa kwa wadogo wamesimama mbele ya hicho kiti cha enzi ;na vitabu vika funguliwa;na
kitabu kingine kikafunguliwa ambacho ni cha uzima;na hao wafu wakahukumiwa
katika mambo hayo yaliyo andikwa katika vile vitabu sawasawa na matendo yao
,bahari ikawatoa wafu walio kuwamo ndani yake;na mauti na kuzimu zika watoa
wafu walio kuwamo ndani yake,wakahukumiwa kila mtu kadri ya matendo yake".mpendwa
hapa utagundua kuwa bado Mungu alimfunulia Yohana kwa habari ya mtu mwenye
sifa za kuingia mbinguni ,parapanda ya
mwisho itakapo lia , hapa hakuna namna ya kukwepa wala njia ya mkato bali ni
kubadirika kwa kutubia uovu wetu na kuyatena mema ndiyo njia salama kwakuwa siku hiyo mahali popote utakapo zikwa au utakapo filia
ndipo utakapo tokea ikiwa uliliwa na simba basi pale simba alipo weka kinyesi
chake ndipo kaburi lako lilipo na ndipo utakapo tokea ,parapanda ya Bwana itakapolia
iliwale wenye sifa za kuvishwa mwili mpya wavishwe tayari kuingia mji mtakatifu
na wale wasio na sifa watatupwa kwenye tanuri la moto maana watakunjwa pamoja
na uovu wote wa dunia kama karatasi .pia soma (Isaya 58;7-15) kupata upana zaidi na
Mungu akubariki na kukufundisha kwa Roho wake mtakatifu (Tutaendelea)
E.mkinga
Kumbuka ku share kwenye Facebook /watsapp/Twitter,na mitandao mingine
Kumbuka ku share kwenye Facebook /watsapp/Twitter,na mitandao mingine
EmoticonEmoticon