JIFUNZE KUISHI MAISHA YAKO HALISI KWANI KUNA
FAIDA NYINGI ZA KUISHI MAISHA HALISI
MAISHA HALISI ;Ni maisha ambayo mtu anayaishi
kutegemeana na tabia zake halisi ,vionjo vyake halisi,mawazo yake halisi
utamaduni wake halisi .nimeamua kutoa mada hii kwasababu kuna watu hawaishi maisha halisi ,(unaweza ukasema huyu ni paka kumbe ni
simba),yaani mtu anakuwa anaishi maisha ya simba wakati yeye ni Panya matokeo
yake akija paka huyu panya anashindwa kukimbilia shimoni (anashikwa na
aibu)kwakuwa yeye huwa anajifanya kuwa
yeye ni simba na matokeo yake anaishia kukamatwa na kuangamizwa kwasababu
aliishi maisha yasiyo yake ndiposa akakosa uhuru na amani ya kujitetea hata
mbele za watu.Au kwakuwa mtu anajulikana
kama mtu wa juu sasa akionekana
anatembea kwa mguu badala ya kupanda daladala ,watu watamuonaje ?,ili aonekane kuwa anapesa ,hivyo anaamua
kupanda daladala wakati nyumbani chakula hakuna matokeo yake analala bila kula
,anaishia tu kujutia
Nimeamua nizungumze mada hii kutokanana kubaini kuwa watuwengi
wanapenda kuishi maisha ya kuigiza, yaani haishi jinsi yeye alivyo bali anaishi
kama mtu fulani alivyo au kama mtu fulani anavyo penda na wengine wanaiga hata
tamaduni za makabila mengine hata kama tamadudi zao ninzuri yaani hazina
madhara kiroho wala kimwili na baadaye tamaduni hizo za kuiga zinageuka na kuwa tanzi kwake
na baadaye maisha yake yanaanza kumsumbua ,naye pasipokujua kuwa hiyohali mbaya
anayoiona maishani mwake ambayo ni kero kwake na ikiwezekana kwa jamii kuwa
imetokana na maisha yasiyo halisi ambayo amekuwa akiyaishi na tiba yake
nigharama.
NB,simaanishi kuiga ni kosa bali sio vizuri kuiga kila kitu kwani unaweza kupoteza hata
uwezo wako ambao wenda ulikuwa mzuri kuliko huo unaoiga,(Mungu aliumba kila mtu
na aina yake ya maisha iliyo njema na yakumpendeza yeye ,(karama)ilikukamilisha
lengo lake Duniani .
Hapa makundi yote ya wanadamu yanahusika katika
maisha haya ya kuigiza ( kuishi maisha yasiyo halisi )
- Kundi la kwanza, ni watu wa nchi fulani ,utakuta watu ni raia wanchi fulani wenye tamaduni zao lakini wanapenda kuishi kama watu wanchi fulani,na mwishowe watashindwa kufanya mambo yanayo endana na nchi yao.Mfano waisraeli wange iga tamaduni na aina ya maisha ya wamisri kipindi cha Musa na Farao unafikiri Mungu angeendelea kuwa Mpiganaji wao? Au hujui kuwa miungu ya wamisri ingewatawala bila wao kujua na wangeshindwa kutimiza ndoto zao na kusudi la Mungu lisinge timia ?,simaanishi kwamba kuiga tamaduni za nchi fulani ni kosa bali ,utamaduni huo unapo igwa uwe nisawasawa na mpango wa Mungu lakini bila kusahau kusudi maalum la Mungu kwenye hiyo nchi yenu ninini, ili kuendelea kutembea kwenye kusudi.Mfano Nchi inapo iga habari za wokovu na kuzileta nchini kwao,nijambo zuri lakini ukirudi kwenye kusudi ,je, kusudi la Mungu anapenda hiyo nchi iokolewe,na kusudi la Mungu kuiokoa nilipi mbali na kuwa huru?kamajibu ni ndio basi wokovu ni lazima uingizwe nchini tena kwa kasi na ufanisi mkubwa .
- Kundi la pili watumishi wa Mungu,hapa utakuta mtumishi anaiga namna fulani ya maisha ya mtumishi fulani yeye anaamini kuwa huyo mtumishi anafanya vizuri hajui kuwa wenda kuna mapungufu ,amesahau kuwa mtumishi yeyote wa Mungu anatakiwa aige tamaduni za Mungu mwenyewe,Kupitia aina ya maisha aliyo yaishi Yesu kristo kwani kwake ndio kisima cha aina zote za maisha ya wanadamu wote kadiri Mungu alivyo kusudia,na ndio maana mtumishi wa aina hii hawezi kukua sana kwa viwango vya juu sawasawa na Mungu alivyo mkusudia kwakuwa yeye anamtegemea Mwana damu pasipo yeyemwenyewe kujua,simaanishi kuwa kuiga sio vizuri bali muulize Mungu kuwa wewe amekuitia huduma gani?na unaifanyaje?Kama huja nielewa muulize mtume Paulo aliiga kwa nani utumishi au petro nkkama sio kwa Yesu mwenyewe unafikiri petro angeiga kwa Paulo (mdo 11;1-43)au kwa Adrea ingekuwaje?ndio maana sifa moja wapo ya mchungaji lazima awe na mahusiano mazuri na Mungu iliasije aka anza kuiga utumishi wa mtu na kuiacha kazi aliyo itiwa .Pia ukitaka kujua zaidi waulize watoto wa skewa (Mdo 19;14) ,yaani hawa watoto walikuwa wanataka kutoa mapepo kwa kutumia upako wa Paulo baada ya kutumia upako halisi utokao kwa Yesu mwenyewe na kukaa ndani yao,madhara yake utayaona kwenye hilo andiko
WACHUMBA
- Kundi la wachumba,hili nalo ni kundi hatari sana wengi wana lalamika sana juu ya uchumba wao kuvunjika hawajui tatizo lao wanaishi kwa kuigiza,kila mtu haishi maisha yake halisi jinsi alivyo .Naanza na wanawake (mabinti),maranyingi kunauigizaji mkubwa wanao ufanya ili kuhakikisha kwamba wanapendwa,kwa mfano ,ikiwa binti akamwambia mchumba wake kuwa hajawaitembea na mwanaume yeyote halafu bahati mbaya au nzuri mwanaume akasikia siri zake zote na idadi ya watu aliowai kutembea nao unafikiri huyo binti atafanyaje ?na huo uchumba kama utaendelea je,utaendelea kwa stailigani?hii ni kwasababu mwanzoni aliishi kwa kuigiza,yaani hakuwa halisi.
- Pia kundi hili la wanawake wengiwao wanapenda kuiga maisha ya kifahari na kupelekea ndoa zao kusumbua ,Mfano;Mwanamke anapotamani utajiri wa mume wa mke mwenzake kwakuwa anagari na akitazama mumewake hana ,kutokana na uchumi wake kuwa duni,na ikiwezekana huyo mwanamke hata aina ya vyakula anapenda kuiga aina za vyakula vyagharama ambavyo nirahisi kutumiwa na wenye pesa za kutosha ,hivyo inapelekea kumsumbua mume wake bila kujalikuwa wao uchimi wao bado hauruhusu hivyo itapelekea maisha yao kuwa magumu zaidi na kuzozana kila siku pia mwanamke anaweza kuanza kumdharau mume wake kwakushindwa kuchukuliana na hali ya uchumi wao na hata kupeana majina kama vile (mwanaume suruali),jambo ambalo limetokana na kutaka kuiga maisha ya watu wenye uwezo kiuchumi. ( hapa suruhisho ni kuridhika kwanza na hali ya maisha yenu kisha muulizeni Mungu ni aina gani ya maisha aliyowaitia kisha anzeni jitihada za kufikia huko kwa njia zisizo mkwaza mwingine
- Wengi wao wanapenda kuvaa nywele za bandia mpaka wasomi, yaani hawajatambua kuwa wanaweza kutengeneza nywele zaozilizo halisi na zikawapendezesha kiasi cha kumtabasamisha kila anayezitazama,hasara za nywele hizo za bandia wengine wanajikuta kupata magonjwa ambayo hawakutarajia ,mfano;kansa,wengine wanaoza vichwa ,yaani hawajui kuwa nywele njingine ni za maiti ,mpendwa au hujui kuwa mapepo mengine yanayo wapata wanawake nikutokana na kuwa na michanganjiko mingi ya matumizi ya vitu.
KUMBUKA;wachumba wengi wanaachana kwasababu ,sikuya
kwanza walipo kutana mwanamke alipendeza kwa vitu vya visivyo halisi yaani
visivyo vya mwili wake mwanaume akajua
kuwa ndivyo Yule mwanamke alivyo, asijue kuwa kunavitu amevitumia ndivyo
vilivyo mpendezesha, sasa mpendwa
unafikili siku mwanamke huyo akifulia basi hata wigi halikaitena(halitapendeza)
na ndio chanzo cha upendo kupungua napengine kuachana kabisa (ishi maisha yako
halisi acha kuigiza shida unazitengeneza mwenyewe ).
- Wanaume ,hili pia ni kundi ambalo wengi wao wanaishi maisha yasiyo halisi na kupelekea kuvunjika kwa ndoa zao au uchumba wao .Kwa mfano; Utakuta kijana (mwanaume kwa maraya kwanza anapo kutana na binti anajifanya kuwa yeye ni tajiri sana wenda akajitahidi hata kuazima nguo za kuvaa ili aonekane kwa binti,au anaweza kuazima hata gari ili aonekane kuwa anauchumi mzuri.
- Mwanaume wingine anadiriki kumdanganya binti ,hapa humnanganya kwa kumwambia kuwa yeye anauchumi mzuri ana muonesha na baadhi ya mali alizonazo kumbe anamdanyanya ili aonekane ,mwingine ana mwambia binti kuwa yeyeanafanyia ofisi fulani ili amteke mwanamke .Sasa mpendwa siku binti akisema leo lazima nishuhudie huko unako fanyia kazi sijui utamwambia ninina ?,na ajabu yake sikuzote maisha ya kuigiza inamaanisha sio maisha halisi yaani yana mwisho wake ,sasa nguvu ya hayo maisha yasiyo halisi (yakuigiza) inapoishia ndipo maisha halisi yanapotaka kuanzia,hivyo kwakuwa mwanzoni walidanganyana hawakuzungumza katika uhalisia ndipo uchumba unapovunjikia (acha kuishi kimtegomtego,ishi maisha halisi)
(Hii ni
mifano tu ya makundi wewe unawezakujua maeneo mengine zaidi )
NB;Mpendwa wewe unafikiri kuwa wanadamu wote
walikuja duniani kufanya vitu vinavyo
fanana?tambua jambo hili kuwa kila mwanadamu alitumwa kufanya kaziyake duniani na zinazo fanana nichache sana ingawa ndani yake kunautofauti mkubwa ,wewe unafikiri kazi au maisha aliyoishi Musa nisawa na kazi aliyo ifanya Ibrahimu?au
utumishi wa Yesu ni sawa na utumishi wa Petro?au wa petro ni sawa na Elia, soma
andiko hili(warumi 12;6-21),kama sio sawa je kwanini wewe unataka ufanane na
mtu ukiona mtufulani amefanya jambo fulani hatakamanijema unaona kuwa amekosea yaani anakuwa amemezwa na
aina fulani au staili fulani ya ufanyaji wa jambo fulani au aina fulani ya maisha ambayo yeye anaipenda ,na anapenda kila mtu
angefanya vile ,hata kama jambo lenyewe ni lakiovu ,(kila mwanadamu kunakitu
kipya ndani yake ambacho kilipaswa akitumie akiwa duniani,mbali na wokovu ambao
nao ni walazima kwa kila mwanadamu)
Na hii imesababisha hata vipawa vya kisayansi
visikue sana kwani watu wanajikita sana kwenye mawazo ya akina plato ,karmax
,Aristotle ,Isack newton nk ,halafu wanaishia hapo bila kuziuliza akili zao na
Mungu wao juu ya mambo mapya aliyo yaweka kiasili ndani yao ,yaani mtu anakuwa
anafikiri kuwa kujua mawazo ya Isack newtorn,plato nk ndio kuwa mwana -sayansi
au ndio kuelimika ,anasahau kuwa tunataka jambo jipya kutoka kwake ambalo
HASARA ZA KUISHI MAISHA YA KUIGIZA (YASIYO
HALISI)
- Kuishi maisha ya kuigiza yasiy halisi,husababisha uchumba kuvunjika rejeamaelezo hapo ju Husababisha manung’uniko ndani ya mtu,anapoona kuna mambo hayaendisawa ,hapa nikwasababu maisha anayoishi siyoyake kwahiyo yanampa shida Siku yamwishoMungu kukushitaki kwasababu ulicho tumwa kufanya duniani hujakifanya bali uliwasaidia wengine kufanya yakwao Inapoteza mfumo mzima wa aina ya maisha ambayo mtu alitakiwa ayaishi baadaye(future),au picha ya maisha . Maisha ya kuigiza yana mfanya mtu awemwongo,mfano;kwakuwa mtu anapenda kujifanya msomi baadaye kila akipigiwa simu akiulizwa yuko wapi anataja eneo ambalo hayupo hapo ,kama ni mtanzania anaweza kusema nipo china kumbe anadanganya Kutengwa na marafiki,mfano ,ikiwa mtu anaigiza kuishi kwa tamaduni za wazungu wakati yeye ni mwafrika na akiona mtu anatabia za kiafrika mtu huyo huanza kuonesha dharau kwa yule mwenye tabia za kiafrika kutokana na kero hiyo urafiki wao unaweza kuishia hapo Husababisha mtu asiendelee kiuchumi,hii ni pale mtu anapojifanya kuwa ni msomi au tajiri au akajifanya kama vile anauchumi wakutosha,matokeo yake akiishiwa pesa atashindwa kufanya kazi na watu wa chini au atashindwa kusukuma mkokoteni au atashindwa kulima shambakwa mkono wake kwasababu ya aibu iliyo tokana na maisha ya kuigiza , na kuishia kwenye manung’uniko. Hudidimiza huduma za kiriho,hapa mtu anakuwa anaiga aina ya utumishi wa mtu mwingine na kusahau utumishi alio itiwa yeye. Inaweza kusababisha kupotea za uhai wa mtu,pale mtu anapojifanya dactari kumbe sio dactari na kupelekea kupoteza uhai wa mtu, Inapelekea mtu hatakama hakuna aliye mpigiasimu akiwambele za watu anajifanya kuna mtu amempigia simu ,anajifanya ameipokea na anaigiza kamavile anaongea na mtu mkubwa sana ili aonekane mtu wa tofauti kati ya watu ,matokeo yake kama alisahau kupunguza sauti ya kuitia ,ghafla simu ikaita hukuipo sikioni ,ndipo ana aibika kuwa ahaaa kumbe alikuwa haongei na mtu ,ila alitaka aonekane kuwa yeye anafahamiana na watu wakubwa.mpendwa (ishi maisha halisi iliuwe na amani) FAIDA ZA KUISHI MAISHA HALISI
- Humfurahisha Mungu kwani ,hii ni kutokana na mtu kuishi sawa sawa na kusudi la Mungu
- Nirahisi kufanikiwa kimwili na kiroho.
- Huleta ufanisi mkubwa kiroho na kimwili,kwani mtuanakuwa na uwezo wa kufanya jambo katika hali ya kipekee zaidi.
- Husaidia kuimarira uchumba ,hapa kila mtu anakuwa anajua uhalisia wa mwingine kwa hivyo nivigumu kumuhimiza mwingine kufanya jambo ambalo sio uhalisia wao kwakuwa linaweza lika waletea majonzi au kuwapotezea muda
- Humfanya mtu kuwa na uhakika na amani tele juu ya maisha yeke
NB;simaanishi kuwa kujifunza kupitia maisha ya watu
ni kosa bali namaanisha,kukopi aina na mwenendo ya maisha ya mtu nakuyafanya kuwa yako,siojambo zuri , imeandikwa amelaaniwa amtegemeaye mwanadamu
,amfanyaye kuwakinga yake…(Yer 17 5-8) ,pia soma (Isay 30;1-2), hapa simaanishi
ule mchezo wa kuigiza kwa muda kwaajili
ya kuelimisha jamii au kwaajili ya kutatua tatizo fulani kwa ghafla kwa muda
mfupi ,kama vile baadhi ya watu walivyo
fanya kwenye biblia ingawa ilisababisha madhara .Mfano Ibrahimu alijifanya kuwa
Sara sio mke wake (Mwanzo 20;1-2),na maanisha pale mtu anapoishi maisha yasiyo
fanana nayeye alivyo katika uhalisia wake .mfano mtu anakuwa anaishi kama
mshauri mzuri kumbe hana sifa za kumshauri mtu na hivyo katika kushauri kwake
anajikuta anaumiza watu yeye bilakujua,au mtu anapojifanya dactari kumbe ni
mfanya mazingaombwe tu na kuleta maafa kwenye afya za watu.(acha kuishi maisha
yasiyo halisi).
SURUHISHO
Hapa nina toa baadhi tu ya suruhisho
- Anza kujifunza kuishi katika uhalisia wako bila kujali watu watakuonaje baada ya kuzoea utajikuta umekuwa huru
- Maisha halisi ya yanayo takiwa kuiga kila kitu au kukopi ni Maisha ya Yesu kristo yasiyo na dhambi ,hii ni kwasababu maisha ya Yesu ndiyo yaliyobeba staili za maisha ya kila mwanadamu ,na ndio maana biblia inasema kila mwanadamu amechorwa kwenye vitanga vya mikono yake (Isaya 49 ;16) haya nimaneno yaajabu sana ambayo ukienda haraka huwezi yaelewavizuri ina mana hata aina ya maisha yako ipo kwake ,pia( Isay 30;1) ,( 2 wakorinto 4;18) maisha yako halisi yapokwenye ulimwengu wa roho ambayo bilaYesu lazima utayatafuta maisha ya mapepo ndio utaanzakuyaishi ukifikiri ni maishayako kumbe umetekwa .mpendwa usiige kirahisi tu maisha ya mtu,kwani hujui ameyaiga wapi maisha yake . Mungu anaangalia kusudi la kukuumba wewe na ndipo anayawezesha maisha yako kadiri ya neno lake (Yer 1;11-12).barikiwa
E.mkinga
EmoticonEmoticon