1.
MWONGOZO WA
KUWAJUA MALAIKA WATENDAO KAZI NA MUNGU
MBINGUNI NA DUNIANI NA NAMNA WANAVYO TENDA KAZI.
Najua umesha soma vitabu vingi au
kuangalia mahubiri mbali mbali yanayo zungumzia kuwajua mapepo au majini na
majina yao, sasa leo naomba tujifunze japo kwa ufupi juu ya malaika ili
tujue namna wanavyo fanya kazi kama wajumbe
wa baraza la mbinguni kwani ufahamu huu utatufanya tuwe karibu na Mungu
kama wengine wanavyo tumia mapepo au wanavyo kuwa karibu na
majini. karibu twende pamoja
MFANO WA MUONEKANO WA MALAIKA
MALAIKA NINANI?
Neno la kiingereza "angel" linatokana na neno la kigiriki "angelos" lenye maana ya "Mjumbe" katika Agano
la Kale, pia kwa Kiebrania neno "malaika"
ni "malak" pia lina maana
ya "mjumbe". Nabii malaki
alipata jina lake kutoka neno hili. Yeye mwenywe alikuwa mjumbe na alitabiri
kuhusu kuja kwa mjumbe wa agano ambaye ni Yesu Kristo (Malaki 3:1) Ingawaje
neno malaika katika Biblia, maana yake ni mjumbe, karibu mara nyingi hutumika
kwa viumbe wa mbinguni, pengine hutumika kwa wajumbe ambao ni wanadamu. Pia ni
viumbe wenye uweza mkuu sana (2 Petro 2: 11)
Kwa Mujibu wa katekisimu katoliki
Malaika ni roho tupu walioumbwa na Mungu, ili wamtukuze milele, wamlinde kila
mtu na kumtumikia Bwana Yesu katika kutuokoa. “Angalieni, msidharau mmojawapo wa wadogo hawa, kwa maana nawaambia ya
kwamba malaika zao mbinguni sikuzote huutazama uso wa Baba yangu aliye
mbinguni” (Math18:10).
Hawa ni viumbe (Roho) au wajumbe walioumbwa na Mungu kwa ajili ya kufanya kazi ya Mungu kazi ya kuwatumikia wanadamu na kumtukuza Mungu mbunguni. Kwa ufupi wao wapo kwaajili ya kumtumikia Mungu, Neno “malaika” humaanisha “Mjumbe.” Wa habari za Mungu kwa mwanadamu malaika wapo wa aina mbalimbali na vitengo tofauti hili linathibitishwa pale biblia inapo sema kuwa kuna malaika mkuu (Angels: God’s Messengers) ( Danieli 12; 7 ), (Yuda 1;9 ), kwahivi ikiwa kuna malaika mkuu basi wapo na wengine wenye vitengo vinavyofuata au tofauti na mkuu.
Katika
Agano la kale malaika wa Mungu anajulikana (sio kutokana na umbo lake) kwa
habari njema anayo leta; mara nyingi anaonekana kama mtu. Maranyingi si rahisi kubainisha tofauti kati ya Mungu na huyo mleta habari
njema wake( Kutoka 3;2-6) kwa nje ubainisho
kati yake na mtu unaelezwa kwa majina ya kiebrania “Serafi” ambao ni viumbe wa mbinguni
wanaozunguka kiti cha enzi na “Makerubi” ambao wanaonekana kama walinzi wa
mahali patakatifu na bustani ya Edeni.
SIFA ZA MALAIKA
v Malaika wana tabia au
uwezo wa kujibadirisha kwa mfano wa kitu chochote kulingana na mazingira
mfano; anaweza kuwa jiwe au kuwa kama
Binadamu , Mti, Nyumba n.k, kwa mfano;
wale malaika walio mtokea Ibrahimu. (Ebrania 13:2)
v Malaika wanaweza kuasi: (Yuda 1:6)(Ezekieli 28:17,)( Isaya
14:12-15.)
v Malaika wanazo nguvu nyingi. ( 2 Petro 2:11)
KUNA MALAIKA WA NAMNA
AU AINA AU NGAZI TOFAUTI TOFAUTI KAMA IFUATAVYO
Kuna malaika wa aina nyingi tofauti
tofauti na idadi yao haijatajwa waziwazi hii ni kudhihirisha kwamba ni jeshi
kubwa sana linalo jumuisha vitengo tofauti tofauti vya malaika, ndiyo maana
tutajifunza japo kwa uchache ili tuwe na mwanga tu utakao tuongoza kufahamu
zaidi (Ufunuo 5;11)hapa katika kitabu
hiki Biblia ina sema Yohana aliona malaika wengi sana elfu kumi mara elfu kumi
na elfu mala elfu ni ni kuonesha kwamba walikuwa wengi hata
hakumbuki idadi au haijui idadi yao alio waona (Luka 2:13,) (Danieli 7;10), (Waebrania 12:22.)
1. Malaika mwenye nguvu
na mwenye mamlaka zaidi ni Mikaeli
(malaika wa vita) au Yesu Kristo, yule malaika mkuu. (1 The 4:16)”Kwa sababu Bwana
mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu,
na Parapanda ya Mungu; naowalio kufa katika kristo watafufuliwa kwanza”. Pia soma (Yuda1; 9)
-
Mikaeli ambaye
ni malaika mkuu anawaongoza malaika wote watakatifu, na jina lake linamaanisha "Nani kama Mungu?"au ‘ambaye ni kama
Mungu, (Danieli 11:1, 12: 1, 1
Wathesalonike 4:16; Yuda 1: 9; Ufunuo 12: 7‐10). Unapo soma maeneo mbalimbali kwa mfano (Lk 10:18) yanaonesha
kuwa na uthibitisho wa kwamba wenda Bwana Yesu akawa ndiye malaika mikaeli , Sasa swali; katika
usomaji wako wa maandiko, nani ambaye ni
kama Mungu halafu tena ni kama binadamu
zaidi ya Yesu na je jina Bwana ni la nani zaidi ya Yesu?
v (Kwa mujibu wa vitabu mbalimbali vya kiroho), “JINA LA MUNGU” lilikuwa ndani ya malaika wake, na
ndio maana tunaona huyo malaika wa Bwana, anaitwa Bwana, mara Mungu kwa
kuchanganya changanya, malaika huyu wa Bwana ni Yesu Kristo Mwenyewe ambaye
alirithi jina lililotukuka kupita la malaika (angalia Waebrania 1:1-4), na jina
hilo ni “Mungu” (Ebr 1:8,9). Jina linamaanisha pia asili, hivyo kwa kuwa jina
la Mungu lilikuwa ndani yake yule malaika; hii inamaana yule malaika naye
alikuwa na asili ya Uungu, kitu pekee kinachothibitisha kuwa yule malaika ni
Yesu Kristo mwenyewe aliyezaliwa zamani za kale na Baba, na kwa kuwa ni mwana
wa Mungu, ana asili na sifa za kiuungu na ana haki ya kutumia jina la Baba
yake.
v
Zekaria
3:1-2 inasema, “Kisha akanionyesha Yoshua, kuhani mkuu, amesimama mbele ya
malaika wa Bwana, na Shetani amesimama mkono wake wa kuume ili kushindana naye.
Bwana akamwambia Shetani, Bwana na akukemee Ewe Shetani; naam, Bwana,
aliyechagua Yerusalemu, na akukemee; je! Hiki si kinga kilichotolewa motoni?”
v
Hapa tunamwona malaika wa Bwana akimwambia
shetani kwamba”Bwana na akukemee”, Ukisoma fungu la 3 utaona Yoshua alikuwa
amevaa “mavazi machafu” hii inawakilisha dhambi. Halafu shetani akaja kwa
Yoshua akidai kuwa yuko upande wake, na malaika wa Bwana hivyo hivyo, alikuja
kumuondolea Yoshua uovu wake, hivyo akamwambia shetani kwamba Bwana na akukemee.
Je ni wapi tena tunaona jambo kama hili hili?
v
Yuda 1:9 inasema, “Lakini Mikaeli, malaika
mkuu, aliposhindana na Ibilisi, na kuhojiana naye kwa ajili ya mwili wa Musa,
hakuthubutu kumshitaki kwa kumlaumu, bali alisema, Bwana na akukemee.”
v
Hapa tunaona kama hilo hilo lilitoke wakati wa
Musa, na malaika aliyefanya hivyo ni Mikaeli malaika mkuu; kwa hakika “malaika
wa Bwana” ndiye “Mikaeli”.
v
Danieli 12:1,2 inasema, “Wakati huo Mikaeli
atasimama, jemadari mkuu, asimamaye upande wa wana wa watu wako;…na wakati huo
watu wako wataokolewa; kila mmoja atakayeonekana ameandikwa katika kitabu kile.
Tena, wengi wa hao walalao katika mavumbi ya nchi wataamka, wengine wapate
uzima wa milele, wengine aibu na kudharauliwa milele.”
v
Zingatia Danieli 12:1, inamwita Mikaeli kama
“Jemedari Mkuu”, na katika Ufunuo 12:7 “Mikaeli na Malaika zake anapigana na
shetani na malaika zake”. Shetani ni mkuu wa malaika zake na malaika zake
humwabudu yeye na kutii amri zake; na malaika zake ni jeshi lake, vivyo hivyo
Mikaeli ni mkuu wa malaika zake, na malaika zake ni jeshi lake, nao hutii amri
zake (Ebrania 1:6-7
. Ukiona mambo hujayapata kama
inavyotakiwa maana yake yupo azuiaye.Yupo saizi ya ibilisi ambaye anaitwa
Malaika Mikaeli. Shetani alikuwa malaika lakini alimwasi Mungu na Mikaeli ndiye
aliyemshughulikia.
Ukiona mambo kwenye maisha yako
yameshindikana usifikiri Mungu hajakusikia maombi yako na amekuacha, kuna
kizuizi cha mkuu wa anga mahali ambaye amekuzuia na huyo lazima ashughulikiwe
na yale majibu yako yaje kwako kwa jina la Yesu.
2. Maserafi, makerubi,
3. Rafaeli ( Malaika wa
Uponyaji),pia kuna
4. Gabrieli (Malaika wa
taarifa) hawa ni baadhi tu , Gabrieli ni
mmoja wa wajumbe wakuu wa Mungu, jina lake linamaanisha "shujaa wa
Mungu," au Mungu ni nguvu yangu , na alipewa ujumbe muhimu kama vile
ujumbe aliopewa Danieli (Danieli 8:16;9:21), aliopewa
Zekaria (Luka 1: 18‐ 19), na Maria (Luka 1: 26‐38). (Luka 2:9-14 )
Hawa ni baadhi tu.
JE MALAIKA WALIKUWAPO TANGU LINI
Malaika
waliumbwa zamani kabla ya dunia kuumbwa, (
Mwanzo
1:1-) Viumbe vyote vya kiroho viliumbwa wakati huu kabla ya mwanzo, hakuna
aliyekuwa akiishi. Mungu aliwapa uzima kwanza kisha, wakashuhudia uumbaji
mwingine. Mungu
alipo iumba dunia malaika walipaaza sauti zao na kushangilia (Ayubu
38:4-7), na kwa njia ya kristo Yesu vitu vingine vikaumbwa (Wakolosai
1:13-17) nao hawaoi wala kuzaa (Marko 12;25).
Pia viumbe vyote vya
kiroho vinamwabudu Mungu. Mungu ni mkuu kuliko mapepo na malaika wote.
Aliishi kabla yao na aliwaumba. Watu wengi kanisani mwetu wana mawazo ya
juu sana kuhusu malaika na viumbe vya kiroho; wanaongelea malaika na
mapepo kana kwamba hao ndio Mungu.( (Nehemia
9:6) (Malaika na viumbe vya
kiroho sio Mungu bali vinamwabudu Mungu.)
MAKERUBI.
Makerubi
wana husianishwa na kiti cha enzi cha Mungu ,Yaani Mungu huketi juu yao. Mungu
huketi juu ya Makerubi (Zaburi 80:1) (Zaburi 99:1) (Ezekieli 10:1, 2.). "makerubi," ni viumbe hai ambao hulinda utakatifu wa
Mungu kutoka kwa uchafu wowote wa dhambi (Mwanzo 3:24; Kutoka 25:18, 20)
Pia ni aina ya Malaika
wanao beba uwepo wa Bwana, ni malaika wangazi ya juu mbele ya Bwana, (Ezekieli 28;13-18) pia yeye huonekana kwa sura za wanyama zaidi ,(Ezekieli 10;1-22 )na hasa kuanzia mstari
wa 10;10 -17 maandiko yana mwita kuwa ni kerubi afunikaye (Ezekieli
28;13-18 ).
Ngazi hii ya kerubi
ndiyo ambayo hata shetani alikuwa hapa katika ngazi hii ya Malaika (Ufunuo 12;7,) Ndiposa
katika kitabu hiki cha ufunuo 12 tunaona kuwa Mikaeli kama
malaika mkuu akiwa na malaika wengine walio chini yake wakishirikiana katika
vita.
Makerubi ndio wa kwanza kutajwa katika Biblia
katika (Mwanzo 3:24, )"Basi
akamfukuza huyo mtu, akaweka Makerubi, upande wa mashariki wa bustani y Edeni,
na upanga wa moto uliogeuka huko na huko, kuilinda njia ya mti wa uzima." Na kama tulivyo tangulia kusema ya kuwa Kabla ya
shetani kufanya uasi wake, shetani
alikuwa kerubi soma (Ezekieli 28:12-15).Na baada ya kuasi akageukana kuwa malaika mwasi, Na
hata sanduku la agano pamoja na makala zake zilizomo zilikuwa na uwakirishi wa
makerubi . (Kutoka 25:17-22), (kutoka 26:1-31),(kutoka36:8; 1),( Wafalme
6:23-35); (wafalme 7:29-36; 8:6-7), (1 Mambo ya
Nyakati 28:18; 2),( Mambo ya Nyakati 3:7-14; 2),( Mambo ya Nyakati
3:10-13; 5:7-8), (Waebrania 9:5)
(Ufunuo 4:6-9) pia inaonekana kuelezea juu ya
makerubi. Makerubi hutumikia kwa kusudi la kutukuza
utakatifu na nguvu za Mungu. Hii ni mojawapo ya jukumu lao kuu kama
tunavyojifunza katika Biblia. Mbali na
kuimba sifa za Mungu, wao.
Sura ya 1 na 10 ya kitabu cha Ezekieli
huelezea "wale viumbe hai wanne" (Ezekieli 1:5) kuwa viumbe hawa ni sawa
na makerubi (Ezekiel 10). Kila mmoja alikuwa na nyuso nne -ule wa mtu, simba, ng'ombe, na
tai (Ezekieli 1:10;) pia 10:14) , na kila mmoja alikuwa na
mabawa manne. Katika muonekano wao, makerubi "walikuwa na sura ya mwanadamu" (Ezekiel 1:5). Makerubi hawa walitumia mbili
ya mbawa zao kwa kuruka na zingine mbili kwa ajili ya kufunika miili yao (Ezekieli 1:6, 11, 23). Na ndiyo maana wanaitwa Kerubi
afunikaye, pia chini ya mabawa yao makerubi walionekana kuwa na umbo lenye
mfano wa mkono wa mwanadamu (Ezekieli 1:8; 10:7-8, 21).
Hivyo tunaweza kusema Kiti cha Enzi cha
Mungu kinazungukwa na wanyama wanne wenye vichwa tofauti. Hawa ni Simba, Ndama,
Tai na Mwanadamu, wanatambulikana kama Makerubi na wana mabawa sita
wanakizunguka Kiti cha Enzi cha Mungu (Ufunuo 4:6-9). Wameumbika katika viungo mchanganyiko,
katika Ezekieli wakiwa walinzi wa Yehova wa Israeli na wanaonekana wenye mabawa
manne katika viwiliwili vyao vya juu. Hapa hawajatajwa kuwa na mabawa mawili
katika miguu yao kama wale Makerubi wanaokizunguka Kiti cha Enzi cha Mungu, au
wale wa moto katika Agano la Kale. Idadi ya hao Makerubi kuwa wanne inatokana
na Uumbaji.
MASERAFI
Maserafi ni viumbe, malaika wanao husishwa na maono ya nabii Isaya juu ya Mungu wake katika hekalu wakati Mungu alimwita kwa huduma yake ya unabii (Isaya 6:1-7). Sasa ukisoma katika. ( Isaya 6:2-4 ), Maandiko yanasema " Juu yake walisimama maserafi; kila mmoja alikuwa na mabawa sita; kwa mawili alifunika uso wake, na kwa mawili alifunika miguu yake, na kwa maawili aliruka. Wakati, kila mmoja na mwenzake, wakisema, Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu, ni Bwana Mungu wa majeshi; Dunia yote imejaa utukufu wake. Na misingi ya vizingiti ikatikisika kwa sababu ya sauti yake aliyelia, nayo nyumba ikajaa moshi".
Pia hawa ni
viumbe wanao mwabudu Mungu Maserafi
;( Isaya 6:1-3)
Viumbe hawa pia waliwahi kujihusisha na
utakaso kwa ajili ya nabii Isaya wakati yeye alianza huduma yake ya kinabii.
Mmoja aliweka makaa ya mawe ya moto juu ya mdomo wa Isaya "Tazama hili
limekugusa midomo yako, na uovu wako umeondolewa, na dhambi yako imefunikwa" (Isaya 6:7). maserafi nao ni watiifu sana kwa Mungu kama
walivyo mmalaika wengine kama vile makerubi, maserafi hasa walijishugulisha
katika kumwabudu Mungu.
Maserafi wana mabawa sita; (Isaya 6:2,6). Wana nguvu uwezo wa kuondoa makosa yaletayo dhambi na kuwaandaa manabii kwa kuwatakasa (Isaya. 6:7). Kuwa na mabawa sita inadhihirisha ukuu na uwezo wao katika utendaji wao wa kazi mbalimbali.
Kwa hiyo hawa maserafi ni “moto wa mbinguni” (Kum. 8:15),( Isa. 14:29; 30:6). Mungu aliwatuma ili waweze kuwaadhibu watu waliotenda dhambi. KWAHIVI TUNA WEZA KUSEMA WANAWAKILISHWA KWA NJIA YA MOTO.
Pia kuna malaika wengine wakuu wanatajwa
mfano Gabrieli, mikaeli, Urieli malaika
mkuu wa dunia na watu wakali) na Raphaeli, Ragueli (ambaye analipiza kisasi juu
ya
dunia na
mwangaza) na Saragaeli. Hawa wanapatikana katika kitabu cha Henoko
(Luka1;26-38),(Luka1;11-20),(Danieli10;13)pia(Daniel12;1 )
(Ufunuo12;7-8) ,Hawa maserafi wana tambulikana kama makerubi wanao kizunguka Kiti cha Enzi cha Mungu kama tunavyoona hapo juu ( Hii ni kwa ufupi ). Barikiwa na Roho mtakatifu atufundishe zaidi kwani sisi wanadamu tunajua kwa sehemu.
(Luka1;26-38),(Luka1;11-20),(Danieli10;13)pia(Daniel12;1 )
(Ufunuo12;7-8) ,Hawa maserafi wana tambulikana kama makerubi wanao kizunguka Kiti cha Enzi cha Mungu kama tunavyoona hapo juu ( Hii ni kwa ufupi ). Barikiwa na Roho mtakatifu atufundishe zaidi kwani sisi wanadamu tunajua kwa sehemu.
UTHIBITISHO KWAMBA MALAIKA WANA WEZA KUWA KATI YETU.
Katika Maandiko, tunaona matukio mengi
ambayo malaika walikuwa sehemu muhimu ya mpango wa Mungu. Mstari mmoja
unaonyesha uwezekano wa malaika kutembea miongoni mwetu hii leo: "Msisahau
kuwafadhili wageni; maana kwa njia hii wengine
wamewakaribisha
malaika pasipo kujua" (Waebrania 13: 2).
Kumbukumbu dhahiri ni kwa Ibrahimu, ambaye malaika wake alimtokea kama wanaume (Mwanzo 18). Aya hii
inaweza
au isiweze kuthibitisha kwamba malaika
kwa kweli hutembea kati yetu bila kujua.
Kuna mifano kadhaa ya maandiko ya
kukutana na malaika, kwa hiyo tunajua kwamba Mungu anaweza kutumia malaika
kutekeleza mambo fulani. Jambo tusilolijua kwa uhakika ni mara ngapi malaika
wanajiruhusu kuonekana na watu. Malaika anaweza kuwafundisha watu (Mwanzo 16: 9), kuwasaidia
watu (Danieli 6:22), kutoa ujumbe kwa watu (Luka 1:35), kuonekana katika maono na ndoto (Danieli 10: 13),
kulinda watu (Kutoka 23:20), na kusaidia kufanya
mipango ya Mungu.(Got questions ).
NI JINSI GANI MALAIKA WANAVYOTUHUDUMIA?
Kwa mwamini, kule kufahamu kwamba malaika wapo kwa
faida yake hii ni msaada wa kutosha. Hii ni sawa na mtu anavyo weza kumwamini
daktari anapomfanyia upasuaji, hatakama amepigwa sindano ya ganzi lakini bado anamuamini
daktari, huyu ni mwanadamu si zaidi sana malaika wanao fanya kazi ya Mungu?.
Kwa kifupi ni kwamba, kweli malaika wanaishi na wapo
kwa ajili ya kutusaidia kama tunamcha Mungu. Ukweli hautegemei yale
tunayoyaona. Tatizo la wanadamu tunapenda kuviamini zaidi vitu vinavyo
onekana ambavyo ni vya muda tu,
tunasahau kuwa visivyo onekana ni vya
milele ((2Wakorintho 4:18).
Wakati jeshi la mbinguni wanapotumwa kuwakusanya
wateule pamoja kwa ajili ya hukumu Yesu atakaporudi, wateule wataweza kukutana
na kuwaona malaika kwa mara ya kwanza mwaliko huenda ukawa hivi, ‘Bwana amekuja
anawaita!" (Yohana 11:28): "Unifumbue macho yangu, ili niyatazame
maajabu yatokayo katika Sheria yako". (Zaburi 119:18).
Biblia
inasema pia Atakuagizia malaika zake wakulinde katika njia zako zote (Zaburi 91;11) Kumbe wako
viumbe ambao wamewekwa na Mungu kwa shughuli mbalimbali ikiwa ni pamoja na
ulinzi wa watu wa Mungu, wakati lile kundi la pili si kundi jema wao wapo kwa
ajili ya kudhuru, kushawishi kutenda uovu, kukatisha tamaa na kuwapinga wanadamu
wenye asili ya uumbaji wa Mungu kwa sura na mfano wake wakitesa na kuua na
kuharibu, haya sio mawazo ya kipuuzi kama wanavyo fikiri wana sayansi ambao
hawaamini katika mambo yasiyoweza kupimwa na kuthibitika kwa kuonekana kwa
macho.Pia huongoza katika njia sahihi. (Kut
23;20-22)
Tunapaswa kuwa na heshima kwa Mungu wetu
na kujua mipaka tuliyo nayo, Mungu amewaumba malaika ili awatumie kwa mapenzi
yake na sio wana damu kuwa amrisha wanacho taka hatakama ni cha kiovu bali
jambo sahihi ni kumwomba Mungu atuagizie malaika hii, walau itapendeza kwani
yeye ndiye ajuaye ni malaika yupi atakaye faa, zaidi sana unaweza tu kuzungu
mza na malaika ambaye amesha kwisha kutumwa kwako (Lk 1:26-38) hapa utakuta malaika walitumwa ndipo hao wandamu
wakaweza kuzungu mza nao, (Waebrania 1;1314
)“ Je yuko malaika aliyemwambia wakati wowote Uketi mkono wangu wa kuume
hata nitakapoweka adui zako chini ya nyayo zako? Je hao wote si roho watumikao
wakitumwa kuwahudumu wale watakaourithi wokovu? Ninacho taka kumaanisha ni hiki unapotambua malaika
waliotumwa kwaajili yako halafu ukazungumza nao ndiyo unaweza kupata msaada kwa
mfano inajulikana kuwa kila mwanadamu anamalaika wake walinzi hivyo unaweza
kuzungumza nao, lakini kuwaamuru moja kwa moja bila mapenzi ya Mungu hainogi sana
Ni kweli kwamba huenda mwanadamu akawa
ni muhimu zaidi mbele za Mungu kuliko malaika lakini lazima tutambue pia kuwa
wenda nafasi ya malaika ikawa tofauti na sisi wanadamu kwa kumjua Mungu au kuwa
karibu na Mungu “Angalieni, msidharau
mmojawapo wadogo hawa, kwa maana nawaambia ya kwamba malaika zao mbinguni
sikuzote huutazama uso wa Baba yangu aliye mbinguni” (Math18:10).hivyo kuwa sikiliza na
kuwaheshimu ni vema kwani itatusaidia kumjua zaidi Mungu.
Hakuna matukio katika Maandiko ambapo
wanadamu waliweza kutoa amri za malaika, ama kwa jina lao au kwa jina la Yesu.
Hakuna vifungu ambapo mtu ana mamlaka juu ya kazi ya
malaika. Tunajua kwamba wao ni viumbe wa
cheo cha juu, kwa sababu Yesu amejiweka yeye mwenyewe "kiwango cha chini
kuliko malaika" ili azaliwa na kuteseka kama mwanadamu (Waebrania 2: 7‐9; Zaburi 8: 4).
Mafundisho kwamba waumini wana mamlaka
juu ya malaika ni uongo. Kanuni zifuatazo za Biblia zinaonyesha kwamba malaika
hawatii amri za wanadamu:
• Tazama maneno ya Musa "Tulimlilia Mwenyezi‐Mungu, naye akakisikiakilio chetu, akatuletea malaika
aliyetuondoa Misri" (Hesabu 20:16). Waisraeli
hawakuamuru malaika kuja kwao. Walimwomba Mungu, ambaye chini ya amri yake
malaika hufanya kazi. Shadraki, Meshaki, na Abednego walikataa kuinamia sanamu
ya Nebukadneza (Danieli 3:17‐18). Mungu kwa rehema yake "alimtuma malaika wake na
kuwaokoa watumishi wake"
AMINI KWAMBA
UNALINDWA NA JESHI KUBWA SANA LA MALAIKA.
Elisha aliomba maombi ili Bwana amfungue
macho mtumishi wake (2Wafalme 6;1317) mara moja mtumishi wa Elisha alifunguliwa macho yake
na aliona jeshi kubwa sana la kiroho (malaika), hata ingawa jeshi la washami
lilipozwa na Israel walipata ushindi wa bila mapigano lakini tunapata ufunuo
mkubwa wa kuweko kwa kundi kubwa la malaika wanao wahudumia wale wanaourithi
wokovu. Ikiwa huduma hii kubwa ya malaika ilikuwa hivi wakati wa Elisha ni
muhimu kufahamu kuwa nyakati za agano jipya sisi tuko chini ya agano lililo
bora zaidi na roho hawa hutumwa kwaajili ya kutuhudumia Biblia inasema hivi
katika (Waebrania 1;1314 )“ Je yuko
malaika aliyemwambia wakati wowote uketi mkono wangu wa kuume hata nitakapoweka
adui zako chini ya nyayo zako? Je hao wote si roho watumikao wakitumwa
kuwahudumu wale watakaourithi wokovu?”
Agano jipya pia linatupa ufunuo fulani
kuhusu malaika na huduma zao aidha, Paulo mtume alikuwa akiwafundisha wakristo
kule Efeso kuwa na ufahamu kuhusu maswala ya ulimwengu wa kiroho, ( Waefeso 6;10-18),
ulimwengu wa kiroho unamajeshi makubwa ya makundi ya malaika ,makundi haya
yamegawanyika katika sehemu kuu mbili, malaika wateule yaani wale walioonyesha
utii kwa Mungu walipopata nafasi ya kutumia utashi wao na kundi linguine ni la
malaika walioasi kutoka katika kundi la
malaika wateule lakini waliamua kwa utashi wao kumfuata shetani na hivyo kuwa
pamoja na shetani na kumtumikia yeye na kupewa majina mengi yanayofanana na
utendaji wao wa kazi majina waliyopewa ni Mashetani, majini,
mapepo, roho chafu, maruhani, na
kadhalika, jina linalotumika katika Biblia kuhusu viumbe hao ni Pepo wachafu,
hili ndilo tutakalolitumia zaidi katika kitabu hiki au somo hili. Ni
jambo la furaha sana kujifunza kuhusu malaika.
MUHIMU
Malaika wapo
katika uwepo wa Mungu au wanafanya kazi ndani ya ramani au ulimwengu wa Roho wa
Mungu, kwasababu wao pia ni rohowema, kumbuka hapa sizungumzii roho au malaika
waasi, kwa maana hiyo wapo malaika wema
na wabaya malaika wabaya malaika wabaya nikama vile mashetani wanaofanya kazi
za kishetani ndio maana ili malaika wema
watusaidie vizuri tunapaswa kuwa watakatifu, hiki ni kitu kinacho wafanya
wafanye makao ndani yetu na kuzungukia Mambo yetu yote kila mmoja na kazi yake
.
Wao wana ya
tambua matakwa ya Roho mtakatifu hata kabla wewe huja yajua ndio maana kuna
wakati mtu anaweza kupata ujumbe fulani kiroho halafu akasema ahsante Roho
mtakatifu kwa kunipa ujumbe kumbe kunawakati hatujui kuwa ni kweli Roho
mtakatifu anatufundisha lakini kumbe
aliye mpa ujumbe ni malaika wa upashaji
wa habari { Gabrieli } .Ufahamu
tunapanua hivi. kuna Mungu Baba, Huyu ni roho,
Kuna Mungu mwana huyu ni Mwili na Roho , Kuna Mungu roho Mtakatifu huyu
naye ni Mungu Yule Yule lakini ameonekana kwa sura, kazi au kitengo tofauti ,
hivyo malaika naye ni roho lakini inategemea anajihusisha kufanya nini hawa
wote ni roho unapo wafahamu vizuri kunawakati itakusaidia sana nisawa na wakati
unakemea pepo, sawa ni shetani yule yule
lakini usipo tambua ni pepo gani ili umlenge moja kwa moja unaweza ukachukua
muda sana kumwondoa sio kwa sababu hauna
nguvu za Mungu bali ni kwa sababu haumjui unaye pambana naye.
KWANINI
TUWATUMIE MALAIKA KATIKA MAMBO YETU?
Hapa simaanishi
kuwaabudu bali tunapaswa kuwaheshimu na
kuwa karibu nao kwani wameumbwa kwaajili ya kumtumikia Mungu katika maisha yetu wanadamu.
v Inaonesha hawa pendezewi na mwanadamu kupotea
dhambini ndiyomaana mtenda dhambi mmoja anapotubu na kugeuka kumwelekea Mungu,
“malaika hushangilia.” (Luka 15:10)
v Hufanya kituo mahali palipo patakatifu palipo
andaliwa kwaajili ya utukufu wa Mungu
mfano ibada n.k
v Mungu ana watumia sana kuwaimarisha na
kuwalinda watumishi wake wa aminifu hapa duniani. (Waebrania 1:14)
v Wana uwezo wa kukunyakua kutoka juu, ili utue
chini kwa usalama (muulize Yesu alipochukuliwa mpaka juu ya mnara wa hekalu ili ajaribiwe
ali ambiwa nini na ibilisi ? ndipo utakapo jua kazi kubwa ya malaika ambayo
haya ibilisi anaijua)
v Malaika anaweza kutuongoza mpakapale tulipo
tengenezawa(Kut 23;20-22)
v Malaika wanaweza
kuwafunga vinywa maadui ikiwa ni mpango wa Mungu mfano; nabii Danieli alitupwa
ndani ya shimo la simba, haku umizwa. Kwa nini?
Kwasababu “Mungu wangu mwenyewe alimtuma malaika wake na kufunga vinywa vya
simba.” (Danieli 6:22).
v Malaika wanaweza kukuchukua katika roho na
kukupeleka pahala fulani ili kukuonesha mambofulani au kuna wakati unaweza
kupelekwa katika altare ya Yesu yaani katika ulimwengu wa kiroho ili Yesu
akutatulie mamboyako,( operation iliyoko
katika ulimwengu wa kiroho) hii
unaweza ielewa vizuri ukikutana na watu ambao walikuwa na vimbe katika sehemu
fulani za miili yao halafu hospitari
wakaambia vipimo havisomi lakini baada ya Malaika wa uponyaji kushughirika
wakajikuta vimbe zime yeyuka
USHUHUDA; Mimi mwenyewe
niliwahi fanyiwa upasuaji operation/surgery ya shingo ilikuwa haina uwezo wa
kugeuka nyuma kalibu wiki zima, pia
niliponywa macho yalipokuwa yaki uma ghafla utadhani yamewekwa pilipili
au vumbi lakini huku nikisikiliza wimbo uitwao (ALTARE KWA BWANA YESU NDIO
HAZINA YETU MALAIKA NIPELEKENI YESU UNIOKOE ) nikiwa katika muunganiko wa
ki-roho na ndipo nilipo gundua kuwa kumbe malaika wana mchango mkubwa sana
maishani mwetu, hii ni kwasababu niliomba
na kukemea sana siku nzima lakini
sikupona, nafikiri kuna wakati
unatakiwa upelekwe katika wodi la kiroho ili ufanyiwe uchunguzi na Bwana
Yesu pata wimbo huo utafakari. NB; Huu ushuhuda sijaumaiza nikipande
tu kwa ufupi.
v Unaweza kuepushwa na janga fulani ikiwa ni
mapenzi ya Mungu kwa mfano; Lutu na binti zake kwa msaada wa malaika wali
okolewa na kupelekwa nje ya mji wa Sodoma na Gomora ulio teketezwa kwa moto
kutokana na uovu
v Kwa sababu hata Ibrahimu aliwatumia ili
kuwaomba kupunguzwa kwa adhabu.
v Malaika anaweza kuleta taarifa .” (Ufunuo 14:6, 7)
mfano; pale kaburini walio kwenda
kulitazama kaburi la Yesu malaika akawatokea na kuwaambia kwanini mnamtafuta
aliye hai kati ya waliokufa? Mariamu alipashwa habari na Malaika wa Bwana
kuwa ata pata mimba na kumzaa mtoto wa kifamle
Pia taarifa ya kuwa
Sara mke wa Ibrahimu atazaa mtoto mwakani mida kama hii ni malaika walio
mtokea Ibrahimu
Tukianza kujifunza juu ya malaika Mungu ataendelea kutufundisha.
NB: Kunawakati malaika
huwapa watu taarifa halafu wao wanasema ni machale yao sasa sijui machale ndio
nini .
v Pia wana uwezo wa kuondoa matatizo yetu mfano
; pale walipo liondoa jiwe katika kaburi la Yesu ili asitoroke .
v Wanaweza kututia nguvu tunapo ishiwa nguvu ,
malaika alimtokea Yesu na “akamtia
nguvu.” (Luka 22:43)
v Petro kutoka gerezani. Ilikuwa ni kwa msaada wa malaika (Matendo 12:6-11).
v Wao hufanya makao kwa wale walio safi kiroho
wanao pigania utakatifu au wema au usafi (Zaburi 34:7).
NB: Hata hivyo, ni lazima tukumbuke kwamba malaika wana
mtumikia Mungu wala si wanadamu. (Zaburi 103:20, 21)
Wanafuata mwongozo wa Mungu bali si maagizo au mao
ya wanadamu. Hivyo,
Mungu ndiye tunaye paswa kumuomba msaada, sio malaika. (Mathayo 26:53).
Pia, Maandiko
yanatuambia kwamba sala zetu na ibada yetu inapaswa kuelekezwa kwa Mungu peke
yake. (Kutoka 20:3-5; Zaburi 5:1, 2; Mathayo 6:9) Malaika
waaminifu hututia moyo tufanye hivyo. (Ufunuo 19:10)
Labda Mungu
akikwambia uwatume au kuwaagiza na sio kwa mapenzi yako bali msikilize Mungu
hii ni kwasababu usije ukadhani unawatuma kumbe wakawa hawa kuelewi maana hauja
angalia mapenzi ya Mungu ninini, tambua kwamba malaika wapo makini sana
kumsikiliza zaidi Mungu na huu ndiyo uaminifu walio nao.
MFANO WA KUOMBA MSAADA WA MALAIKA
Ee Mungu mwenye nguvu,
nina kuja kwako kwa unyenyekevu kupitia
jina la mwanao Yesu kristo nakuomba uniagizie malaika wa vita/wa
uponyaji/taarifa/mlinzi/, ili wanisaidie kupigana na maadui zangu kwa jina la
Yesu mwanao nimeomba amina.
Au
Mungu Baba ninakuja mbele zako kwa njia ya
kristo mwanao mpendwa, nina jua
unanisikiliza daima, hivyo ninatamani
kupata taarifa au ujumbe juu ya mgonjwa
huyu au tatizo…….. kwakuwa wewe ni Mungu
wa siri, nina kusihi Bwana na Muumba wangu uniagizie malaika ili anijurishe
namna ya kulitatua tatizo hili, maana nina amini utakapo nipa taarifa utanipa
na namna ya kulitatua, Roho mtakatifu niongoze kuelewa ujumbe nitakao
letewa,ninapopata ujumbe, adui ashindwa kuuiba kwa jina la Yesu amina. (Sasa
wakisha kuja hapo ndio unaweza watumia kuwa uliza maswali au kuwaomba msaada
zaidi na wao watajua namna ya kukusaidia lakini haya yote lazima uwe na macho
ya rohoni)
Nimekupa
muongozo huu kwasababu hawa hawana mamlaka kuliko Mungu bali hufuata maagizo ya
Mungu yaani wao
humtumikia Mungu ila kwa kuwa mimi na wewe tuna wafahamu na kazi zao,
basi tuna mwomba Mungu msaada wao ,ni sawa na mtu anapo hitaji msaada
fulani wa wanajeshi, kumsaidia suala
fulani, ni muhimu kumuona kiongozi mkuu ili
awatume kukusaidia na wakitumwa na mkuu
hufanya kazi kwa nguvu zote. Sasa kiongozi mkuu wa jeshi la malaika ni yesu
kristo ambaye ndiye malaika mikaeli.
Tunawathamini
sana malaika hao waaminifu ambao siku zote hutekeleza maagizo ya Mungu! Huwa
tumia kuwa saidia na kuwa linda watumishi wake waaminifu walio duniani hii ina
tutia sana nguvu kwa sababu kuna viumbe
wa roho hatari ambao wanaitwa roho waovu wanaotaka kutudhuru
NB: Hawa ni baadhi tu ya malaika wapo
wengi sana lakini tukiwa na ufahamu tu, juu ya uwepo wao na kazi zao katika
maisha ya mwanadamu, inaweza kutusaidia.
Na kazi hizi zote anaye zifanya ni Mungu yuleyule mmoja kupitia jeshi lake la
malaika kila mmoja na kitengo chake.
SHETANI HUJIFANYA
KAMA MALAIKA WA NURU.
kwa kuwa uwiano wa uovu na giza, na
uzuri na mwanga, ni mfano inayofanana yenye nguvu katika historia ya mwanadamu.
Katika Biblia, nuru ni mfano wa kiroho wa kweli na asili ya Mungu isiyobadilika
(Yakobo
1:17). Hutumiwa mara kwa mara katika Biblia kutusaidia kuelewa kwamba
Mungu ni mzuri kabisa na wa kweli (1 Yohana 1: 5). Tunapokuwa
"katika nuru," tuko pamoja Naye (1 Petro 2: 9).
FAHAMU
ZAIDI KUHUSU MALAIKA
·
Malaika wema kazi yao ni kutuombea, kutumwa na Mungu
kwetu, na wanatulinda kama Malaika walinzi. (Ebr, 13:2). Ambapo kila
·
Mwanadamu anaMalaika wake wa kumlinda na kumuongoza
Roho na Mwili, ndie Malaika wake mlinzi, (Zab, 91:11, Mt. 18:10).
·
Malaika wote sio sawa, wapo Malaika Wakuu, Malaika
wanaomtumikia Mungu Mbinguni kwa mfano Makerubi na Maserafi, na pia wapoMalaika
walinzi.
·
Malaika wakuu ni Mikaeli, Gabrieli na Raphaeli (Dn,
10:13, Tobiti 12:15, Lk 1:26).
·
Mashetani kazi yao ni kuteswa Motoni na hutaka kudhuru
Roho na Miili ya wanadamuna kutupoteza milele. (1 Petro, 5:8, Yoh, 8:44).
·
Hapo Mwanzo Mungu aliumba Malaika katika hali ya njema
na Heri kubwa. Kisha aliumba mbingu na nchi, na viumbe vyotevinavyoonekana na
visivyoonekena. (Kol, 1;16, Mwa, 1;31)
·
Malaika ni viumbe vilivyo Roho tupu na vyenye akili na
utashi. (Zab 91:11, Ebr 1:7, Uf, 12:7-9).
·
Malaika wengine walikosa kwa kumkaidi Mungu, wakatupwa
motoni na ndio Mashetani ambao Mkubwa wao ni Lusiferi. (Yn, 8:44: Uf12:7-9,).
·
Mungu aliumba Malaika ili Wamtukuze, Wafurahi nae
Mbinguni na wawe Matarishi/wajumbe wake kwa Wanadamu. (Tob 12:12, Lk.16:22).
Imeandaliwa na E.mkinga
NB;kusharea
kwenye makundi ya mitandao mbalimbali ya kijamii kama vile
WatsApp,
Instagram ,Twitter,Facebook
KISIMA CHA BARAKA
10 comments
Mtumishi ubarikewe kwa huduma yako
Amina sana.!
Nashukuru sana Mungu akubariki.
Nashukuru sana Mungu akubariki.
Amina ubarikiwe na Bwana kwa ufunuo huu
Ubarikiwe sana mtumishi hakika nmejifunza na kupata mwongozo mzuri
Acha kudanganya na kuchanganya watu, Yesu ni Yesu na mikaaeli ni Mikaeli usichanganye kabisa.
Fuatilia vizuri hii mistari hapo chini...
*Soma ufunuo 4: yote na ufunuo 5:yote
*Soma mithali 8:22-35
* Yesu ni mwana wa Mungu, na Yesu ni Mungu. Katika utatu mtakatifu Mungu Mmoja ( Baba+mwana("neno". sawasawa na yoh1:1,mwanzo 1:2)+Roho mtakatifu
* Jitunzeni mbele yake, mwisikize sauti yake; wala msimtie kasirani; maana, hatawasamehe makosa yenu; kwa kuwa jina langu limo ndani yake.
#mikaeli,rafaeli,gabrieli nk..
# hiyo "eli" au "el" humaanisha Mungu wamebeba jina la Mungu plus sifa ya task aliyonayo kwa ajili ya Mungu( Kiebrania "Mik mo elohim?" - "Ni nani aliye kama Mungu?")
Kutoka 23:21
ikasikia sauti ya mwanadamu katikati ya mto Ulai, iliyoita na kusema, Gabrieli, mfahamishe mtu huyu maono haya.
Danieli 8:16
naam, nilipokuwa nikinena katika kuomba, mtu yule, Gabrieli, niliyemwona katika njozi hapo kwanza, akirushwa upesi, alinigusa panapo wakati wa dhabihu ya jioni.
Danieli 9:21
Malaika akamjibu akamwambia, Mimi ni Gabrieli, nisimamaye mbele za Mungu; nami nimetumwa niseme nawe, na kukupasha habari hizi njema.
Luka 1:19
Mwezi wa sita, malaika Gabrieli alitumwa na Mungu kwenda mpaka mji wa Galilaya, jina lake Nazareti,
Luka 1:26
13 Lakini mkuu wa ufalme wa Uajemi alinipinga siku ishirini na moja; bali, tazama, huyo Mikaeli, mmoja wa hao wakuu wa mbele, akaja kunisaidia; nami nikamwacha huko pamoja na wafalme wa Uajemi.
Danieli 10:13
21 Lakini nitakuambia yaliyoandikwa katika maandiko ya kweli; wala hapana anisaidiaye juu ya hao ila huyo Mikaeli, mkuu wenu.
Danieli 10:21
Sina tatizo sana na mafundisho lakin shida moja inaibuka hapo kwennye statement ya Yesu na huenda ikawa ndie mikaeli.
Hapo ni assumption haina ukweli wowote kibiblia.
SAWA UKO VIZURI UBARIKIWE
YESU NI YESU = MUNGU
MICHAEL = MALAIKA MKUU. ASANTE
EmoticonEmoticon