Friday, 10 November 2017

INGIZA NYIMBO ZAKO ZA GOSPEL YOU TUBE BURE KABISA

Tags

                                

                                                      FURAHIA OFAAA!!!
             
                                        
                                              



Tuna kujuza Kuwa ikiwa unahitaji njimbo zako zionekaze mtandaoni ,basi tutafutekwanamba 0757250806.  Utawekewa nyimbo zako you tube buuuree kabisa barikiwa, mtaarifu na mwenzako




MWONGOZO WA KUWAJUA MALAIKA WATENDAO KAZI NA MUNGU

Tags

  1.   MWONGOZO WA KUWAJUA MALAIKA WATENDAO   KAZI NA MUNGU MBINGUNI NA DUNIANI NA NAMNA WANAVYO TENDA KAZI.
Najua umesha soma vitabu vingi au kuangalia mahubiri mbali mbali yanayo zungumzia kuwajua mapepo au majini na majina yao, sasa leo naomba tujifunze japo kwa ufupi juu ya malaika   ili tujue namna wanavyo fanya kazi kama wajumbe wa baraza la mbinguni kwani ufahamu huu utatufanya tuwe karibu na Mungu kama wengine wanavyo tumia mapepo au wanavyo kuwa karibu na majini.   karibu twende pamoja

 MFANO WA MUONEKANO WA MALAIKA
                             


                                                       
                       MALAIKA NINANI?

Neno la kiingereza "angel" linatokana na neno la kigiriki "angelos" lenye maana ya "Mjumbe" katika Agano la Kale, pia kwa Kiebrania neno "malaika" ni "malak" pia lina maana ya "mjumbe". Nabii malaki alipata jina lake kutoka neno hili. Yeye mwenywe alikuwa mjumbe na alitabiri kuhusu kuja kwa mjumbe wa agano ambaye ni Yesu Kristo (Malaki 3:1) Ingawaje neno malaika katika Biblia, maana yake ni mjumbe, karibu mara nyingi hutumika kwa viumbe wa mbinguni, pengine hutumika kwa wajumbe ambao ni wanadamu. Pia ni viumbe wenye uweza mkuu sana (2 Petro 2: 11)

Kwa Mujibu wa katekisimu katoliki Malaika ni roho tupu walioumbwa na Mungu, ili wamtukuze milele, wamlinde kila mtu na kumtumikia Bwana Yesu katika kutuokoa. “Angalieni, msidharau mmojawapo wa wadogo hawa, kwa maana nawaambia ya kwamba malaika zao mbinguni sikuzote huutazama uso wa Baba yangu aliye mbinguni” (Math18:10).

Hawa ni viumbe (Roho) au wajumbe walioumbwa na Mungu kwa ajili ya kufanya kazi ya Mungu kazi ya kuwatumikia wanadamu na kumtukuza Mungu mbunguni. Kwa ufupi wao wapo kwaajili ya kumtumikia Mungu,  Neno “malaika” humaanisha “Mjumbe.” Wa habari za Mungu kwa mwanadamu malaika wapo wa aina mbalimbali na vitengo tofauti hili linathibitishwa pale biblia inapo sema kuwa kuna malaika mkuu (Angels: God’s Messengers)  ( Danieli 12; 7 ), (Yuda 1;9 ), kwahivi ikiwa kuna malaika mkuu basi wapo na wengine wenye vitengo vinavyofuata au tofauti na mkuu.

Katika Agano la kale malaika wa Mungu anajulikana (sio kutokana na umbo lake) kwa habari njema anayo leta; mara nyingi anaonekana kama mtu. Maranyingi  si rahisi kubainisha  tofauti kati ya Mungu na huyo mleta habari njema  wake( Kutoka 3;2-6) kwa nje ubainisho kati yake na mtu unaelezwa kwa majina ya kiebrania  “Serafi” ambao ni viumbe wa mbinguni wanaozunguka kiti cha enzi na “Makerubi” ambao wanaonekana kama walinzi wa mahali patakatifu na bustani ya Edeni.

                            


                      SIFA ZA MALAIKA   

v Malaika wana tabia au uwezo wa kujibadirisha kwa mfano wa kitu chochote kulingana na mazingira mfano;  anaweza kuwa jiwe au kuwa kama Binadamu ,  Mti, Nyumba n.k, kwa mfano; wale malaika walio mtokea Ibrahimu. (Ebrania 13:2)
v Malaika wanaweza kuasi: (Yuda 1:6)(Ezekieli 28:17,)( Isaya 14:12-15.)
v Malaika wanazo nguvu nyingi. ( 2 Petro 2:11)

KUNA MALAIKA WA NAMNA AU AINA AU NGAZI TOFAUTI TOFAUTI KAMA IFUATAVYO

Kuna malaika wa aina nyingi tofauti tofauti na idadi yao haijatajwa waziwazi hii ni kudhihirisha kwamba ni jeshi kubwa sana linalo jumuisha vitengo tofauti tofauti vya malaika, ndiyo maana tutajifunza japo kwa uchache ili tuwe na mwanga tu utakao tuongoza kufahamu zaidi (Ufunuo 5;11)hapa  katika kitabu hiki Biblia ina sema Yohana aliona malaika wengi sana elfu kumi mara elfu kumi na  elfu mala elfu  ni ni kuonesha kwamba walikuwa wengi hata hakumbuki idadi au haijui idadi yao alio waona (Luka 2:13,) (Danieli 7;10), (Waebrania 12:22.)

1.    Malaika mwenye nguvu na mwenye mamlaka zaidi ni Mikaeli (malaika wa vita) au Yesu Kristo, yule malaika mkuu. (1 The 4:16)”Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na Parapanda ya Mungu; naowalio kufa katika kristo watafufuliwa kwanza”. Pia soma  (Yuda1; 9)
-         Mikaeli ambaye ni malaika mkuu anawaongoza malaika wote watakatifu,  na jina lake linamaanisha "Nani  kama Mungu?"au ‘ambaye ni kama Mungu,  (Danieli 11:1, 12: 1, 1 Wathesalonike 4:16; Yuda 1: 9; Ufunuo 12: 710). Unapo soma maeneo mbalimbali kwa mfano (Lk 10:18) yanaonesha kuwa na uthibitisho wa kwamba wenda Bwana Yesu akawa ndiye malaika mikaeli , Sasa swali; katika usomaji  wako wa maandiko, nani ambaye ni kama Mungu halafu tena ni kama binadamu  zaidi ya Yesu na je jina Bwana ni la nani zaidi ya Yesu?

v  (Kwa mujibu wa vitabu mbalimbali vya kiroho), “JINA LA MUNGU” lilikuwa ndani ya malaika wake, na ndio maana tunaona huyo malaika wa Bwana, anaitwa Bwana, mara Mungu kwa kuchanganya changanya, malaika huyu wa Bwana ni Yesu Kristo Mwenyewe ambaye alirithi jina lililotukuka kupita la malaika (angalia Waebrania 1:1-4), na jina hilo ni “Mungu” (Ebr 1:8,9). Jina linamaanisha pia asili, hivyo kwa kuwa jina la Mungu lilikuwa ndani yake yule malaika; hii inamaana yule malaika naye alikuwa na asili ya Uungu, kitu pekee kinachothibitisha kuwa yule malaika ni Yesu Kristo mwenyewe aliyezaliwa zamani za kale na Baba, na kwa kuwa ni mwana wa Mungu, ana asili na sifa za kiuungu na ana haki ya kutumia jina la Baba yake.
v Zekaria 3:1-2 inasema, “Kisha akanionyesha Yoshua, kuhani mkuu, amesimama mbele ya malaika wa Bwana, na Shetani amesimama mkono wake wa kuume ili kushindana naye. Bwana akamwambia Shetani, Bwana na akukemee Ewe Shetani; naam, Bwana, aliyechagua Yerusalemu, na akukemee; je! Hiki si kinga kilichotolewa motoni?”
v  Hapa tunamwona malaika wa Bwana akimwambia shetani kwamba”Bwana na akukemee”, Ukisoma fungu la 3 utaona Yoshua alikuwa amevaa “mavazi machafu” hii inawakilisha dhambi. Halafu shetani akaja kwa Yoshua akidai kuwa yuko upande wake, na malaika wa Bwana hivyo hivyo, alikuja kumuondolea Yoshua uovu wake, hivyo akamwambia shetani kwamba Bwana na akukemee. Je ni wapi tena tunaona jambo kama hili hili?
v  Yuda 1:9 inasema, “Lakini Mikaeli, malaika mkuu, aliposhindana na Ibilisi, na kuhojiana naye kwa ajili ya mwili wa Musa, hakuthubutu kumshitaki kwa kumlaumu, bali alisema, Bwana na akukemee.”
v  Hapa tunaona kama hilo hilo lilitoke wakati wa Musa, na malaika aliyefanya hivyo ni Mikaeli malaika mkuu; kwa hakika “malaika wa Bwana” ndiye “Mikaeli”.
v  Danieli 12:1,2 inasema, “Wakati huo Mikaeli atasimama, jemadari mkuu, asimamaye upande wa wana wa watu wako;…na wakati huo watu wako wataokolewa; kila mmoja atakayeonekana ameandikwa katika kitabu kile. Tena, wengi wa hao walalao katika mavumbi ya nchi wataamka, wengine wapate uzima wa milele, wengine aibu na kudharauliwa milele.”
v  Zingatia Danieli 12:1, inamwita Mikaeli kama “Jemedari Mkuu”, na katika Ufunuo 12:7 “Mikaeli na Malaika zake anapigana na shetani na malaika zake”. Shetani ni mkuu wa malaika zake na malaika zake humwabudu yeye na kutii amri zake; na malaika zake ni jeshi lake, vivyo hivyo Mikaeli ni mkuu wa malaika zake, na malaika zake ni jeshi lake, nao hutii amri zake (Ebrania 1:6-7
. Ukiona mambo hujayapata kama inavyotakiwa maana yake yupo azuiaye.Yupo saizi ya ibilisi ambaye anaitwa Malaika Mikaeli. Shetani alikuwa malaika lakini alimwasi Mungu na Mikaeli ndiye aliyemshughulikia.
Ukiona mambo kwenye maisha yako yameshindikana usifikiri Mungu hajakusikia maombi yako na amekuacha, kuna kizuizi cha mkuu wa anga mahali ambaye amekuzuia na huyo lazima ashughulikiwe na yale majibu yako yaje kwako kwa jina la Yesu.  
                                
2.    Maserafi,  makerubi,
3.    Rafaeli ( Malaika wa Uponyaji),pia kuna
4.    Gabrieli (Malaika wa taarifa) hawa ni baadhi tu , Gabrieli ni mmoja wa wajumbe wakuu wa Mungu, jina lake linamaanisha "shujaa wa Mungu," au Mungu ni nguvu yangu , na alipewa ujumbe muhimu kama vile ujumbe aliopewa Danieli (Danieli 8:16;9:21), aliopewa Zekaria (Luka 1: 18 19), na Maria (Luka 1: 2638). (Luka 2:9-14 )
Hawa ni baadhi tu.

       JE MALAIKA WALIKUWAPO TANGU LINI
           
Malaika waliumbwa zamani kabla ya dunia kuumbwa, ( Mwanzo 1:1-) Viumbe vyote vya kiroho viliumbwa wakati huu kabla ya mwanzo, hakuna aliyekuwa akiishi. Mungu aliwapa uzima kwanza kisha, wakashuhudia uumbaji mwingine. Mungu alipo iumba dunia malaika walipaaza sauti zao na kushangilia (Ayubu 38:4-7), na kwa njia ya kristo Yesu vitu vingine vikaumbwa (Wakolosai 1:13-17) nao hawaoi wala kuzaa (Marko 12;25).          

Pia viumbe vyote vya kiroho vinamwabudu Mungu. Mungu ni mkuu kuliko mapepo na malaika wote. Aliishi kabla yao na aliwaumba. Watu wengi kanisani mwetu wana mawazo ya juu sana kuhusu malaika na viumbe vya kiroho; wanaongelea malaika na mapepo kana kwamba hao ndio Mungu.( (Nehemia 9:6) (Malaika na viumbe vya kiroho sio Mungu bali vinamwabudu Mungu.)
    
                          MAKERUBI.

Makerubi wana husianishwa na kiti cha enzi cha Mungu ,Yaani Mungu huketi juu yao. Mungu huketi juu ya Makerubi (Zaburi 80:1) (Zaburi 99:1) (Ezekieli 10:1, 2.). "makerubi,"  ni viumbe hai ambao hulinda utakatifu wa Mungu kutoka kwa uchafu wowote wa dhambi (Mwanzo 3:24; Kutoka 25:18, 20)
Pia ni aina ya Malaika wanao beba uwepo wa Bwana, ni malaika wangazi ya juu mbele ya Bwana, (Ezekieli 28;13-18) pia yeye huonekana kwa sura za wanyama zaidi ,(Ezekieli 10;1-22 )na hasa kuanzia mstari wa 10;10 -17 maandiko yana mwita kuwa ni kerubi afunikaye (Ezekieli 28;13-18 ).
Ngazi hii ya kerubi ndiyo ambayo hata shetani alikuwa hapa katika ngazi hii ya Malaika (Ufunuo 12;7,) Ndiposa katika kitabu  hiki cha ufunuo 12 tunaona kuwa Mikaeli kama malaika mkuu akiwa na malaika wengine walio chini yake wakishirikiana katika vita.

Makerubi ndio wa kwanza kutajwa katika Biblia katika (Mwanzo 3:24, )"Basi akamfukuza huyo mtu, akaweka Makerubi, upande wa mashariki wa bustani y Edeni, na upanga wa moto uliogeuka huko na huko, kuilinda njia ya mti wa uzima." Na kama tulivyo tangulia kusema ya kuwa Kabla ya shetani kufanya  uasi wake, shetani alikuwa kerubi soma (Ezekieli 28:12-15).Na baada ya kuasi akageukana kuwa malaika mwasi, Na hata sanduku la agano pamoja na makala zake zilizomo zilikuwa na uwakirishi wa makerubi . (Kutoka 25:17-22), (kutoka 26:1-31),(kutoka36:8; 1),( Wafalme 6:23-35); (wafalme 7:29-36; 8:6-7), (1 Mambo ya  Nyakati 28:18; 2),( Mambo ya Nyakati 3:7-14; 2),( Mambo ya Nyakati 3:10-13; 5:7-8), (Waebrania 9:5)
(Ufunuo 4:6-9) pia inaonekana kuelezea juu ya makerubi. Makerubi hutumikia kwa kusudi la kutukuza utakatifu na nguvu za Mungu. Hii ni mojawapo ya jukumu lao kuu kama tunavyojifunza katika Biblia. Mbali na kuimba sifa za Mungu, wao.

Sura ya 1 na 10 ya kitabu cha Ezekieli huelezea "wale viumbe hai wanne" (Ezekieli 1:5) kuwa viumbe hawa ni sawa na makerubi (Ezekiel 10). Kila mmoja alikuwa na nyuso nne -ule wa mtu, simba, ng'ombe, na tai (Ezekieli 1:10;) pia 10:14) , na kila mmoja alikuwa na mabawa manne. Katika muonekano wao, makerubi "walikuwa na sura ya mwanadamu" (Ezekiel 1:5). Makerubi hawa walitumia mbili ya mbawa zao kwa kuruka na zingine mbili kwa ajili ya kufunika miili yao (Ezekieli 1:6, 11, 23). Na ndiyo maana wanaitwa Kerubi afunikaye, pia chini ya mabawa yao makerubi walionekana kuwa na umbo lenye mfano wa mkono wa mwanadamu (Ezekieli 1:8; 10:7-8, 21).

Hivyo tunaweza kusema Kiti cha Enzi cha Mungu kinazungukwa na wanyama wanne wenye vichwa tofauti. Hawa ni Simba, Ndama, Tai na Mwanadamu, wanatambulikana kama Makerubi na wana mabawa sita wanakizunguka Kiti cha Enzi cha Mungu (Ufunuo 4:6-9). Wameumbika katika viungo mchanganyiko, katika Ezekieli wakiwa walinzi wa Yehova wa Israeli na wanaonekana wenye mabawa manne katika viwiliwili vyao vya juu. Hapa hawajatajwa kuwa na mabawa mawili katika miguu yao kama wale Makerubi wanaokizunguka Kiti cha Enzi cha Mungu, au wale wa moto katika Agano la Kale. Idadi ya hao Makerubi kuwa wanne inatokana na Uumbaji.
                                   MASERAFI
                                           
Maserafi ni viumbe, malaika wanao husishwa na maono ya nabii Isaya juu ya Mungu wake katika hekalu wakati Mungu alimwita kwa huduma yake ya unabii (Isaya 6:1-7). Sasa ukisoma katika.  ( Isaya 6:2-4 ), Maandiko yanasema  " Juu yake walisimama maserafi; kila mmoja alikuwa na mabawa sita; kwa mawili alifunika uso wake, na kwa mawili alifunika miguu yake, na kwa maawili aliruka. Wakati, kila mmoja na mwenzake, wakisema, Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu, ni Bwana Mungu wa majeshi; Dunia yote imejaa utukufu wake. Na misingi ya vizingiti ikatikisika kwa sababu ya sauti yake aliyelia, nayo nyumba ikajaa moshi".

Pia hawa ni viumbe wanao mwabudu Mungu Maserafi ;( Isaya 6:1-3)

Viumbe hawa pia waliwahi kujihusisha na utakaso kwa ajili ya nabii Isaya wakati yeye alianza huduma yake ya kinabii. Mmoja aliweka makaa ya mawe ya moto juu ya mdomo wa Isaya "Tazama hili limekugusa midomo yako, na uovu wako umeondolewa, na dhambi yako imefunikwa" (Isaya 6:7).   maserafi nao ni watiifu sana kwa Mungu kama walivyo mmalaika wengine kama vile makerubi, maserafi hasa walijishugulisha katika kumwabudu Mungu.

Maserafi wana mabawa sita;
 (Isaya 6:2,6). Wana nguvu uwezo wa kuondoa makosa yaletayo dhambi na kuwaandaa manabii kwa kuwatakasa (Isaya. 6:7). Kuwa na mabawa sita inadhihirisha ukuu na uwezo wao katika utendaji wao wa kazi mbalimbali.
Kwa hiyo hawa maserafi ni “moto wa mbinguni”
  (Kum. 8:15),( Isa. 14:29; 30:6). Mungu aliwatuma ili waweze kuwaadhibu watu waliotenda dhambi. KWAHIVI TUNA WEZA KUSEMA WANAWAKILISHWA KWA NJIA YA MOTO.

Pia kuna malaika wengine wakuu wanatajwa mfano Gabrieli, mikaeli, Urieli malaika mkuu wa dunia na watu wakali) na Raphaeli, Ragueli (ambaye analipiza kisasi juu ya
dunia na mwangaza) na Saragaeli. Hawa wanapatikana katika kitabu cha Henoko
(Luka1;26-38),(Luka1;11-20),(Danieli10;13)pia(Daniel12;1 )
(Ufunuo12;7-8)
 ,
Hawa maserafi wana tambulikana kama makerubi wanao kizunguka Kiti cha Enzi cha Mungu kama tunavyoona hapo juu ( Hii ni kwa ufupi ). Barikiwa na Roho mtakatifu atufundishe zaidi kwani sisi wanadamu tunajua kwa sehemu.

UTHIBITISHO KWAMBA MALAIKA WANA WEZA KUWA KATI YETU.

Katika Maandiko, tunaona matukio mengi ambayo malaika walikuwa sehemu muhimu ya mpango wa Mungu. Mstari mmoja unaonyesha uwezekano wa malaika kutembea miongoni mwetu hii leo: "Msisahau kuwafadhili wageni; maana kwa njia hii wengine
wamewakaribisha malaika pasipo kujua" (Waebrania 13: 2). Kumbukumbu dhahiri ni kwa Ibrahimu, ambaye malaika wake alimtokea kama wanaume (Mwanzo 18). Aya hii inaweza
au isiweze kuthibitisha kwamba malaika kwa kweli hutembea kati  yetu bila kujua.

Kuna mifano kadhaa ya maandiko ya kukutana na malaika, kwa hiyo tunajua kwamba Mungu anaweza kutumia malaika kutekeleza mambo fulani. Jambo tusilolijua kwa uhakika ni mara ngapi malaika wanajiruhusu kuonekana na watu. Malaika anaweza kuwafundisha watu (Mwanzo 16: 9), kuwasaidia watu (Danieli 6:22), kutoa ujumbe kwa watu (Luka 1:35), kuonekana katika maono na ndoto (Danieli 10: 13), kulinda watu (Kutoka 23:20), na kusaidia kufanya
mipango ya Mungu.(Got questions ).
 NI JINSI GANI MALAIKA WANAVYOTUHUDUMIA?
    
Kwa mwamini, kule kufahamu kwamba malaika wapo kwa faida yake hii ni msaada wa kutosha. Hii ni sawa na mtu anavyo weza kumwamini daktari anapomfanyia upasuaji, hatakama amepigwa  sindano ya ganzi lakini bado anamuamini daktari, huyu ni mwanadamu si zaidi sana malaika wanao fanya kazi ya Mungu?.

Kwa kifupi ni kwamba, kweli malaika wanaishi na wapo kwa ajili ya kutusaidia kama tunamcha Mungu. Ukweli hautegemei yale tunayoyaona. Tatizo la wanadamu tunapenda kuviamini zaidi vitu vinavyo onekana  ambavyo ni vya muda tu, tunasahau kuwa  visivyo onekana ni vya milele ((2Wakorintho 4:18).

Wakati jeshi la mbinguni wanapotumwa kuwakusanya wateule pamoja kwa ajili ya hukumu Yesu atakaporudi, wateule wataweza kukutana na kuwaona malaika kwa mara ya kwanza mwaliko huenda ukawa hivi, ‘Bwana amekuja anawaita!" (Yohana 11:28): "Unifumbue macho yangu, ili niyatazame maajabu yatokayo katika Sheria yako". (Zaburi 119:18).
     
Biblia inasema pia Atakuagizia malaika zake wakulinde katika njia zako zote (Zaburi 91;11) Kumbe wako viumbe ambao wamewekwa na Mungu kwa shughuli mbalimbali ikiwa ni pamoja na ulinzi wa watu wa Mungu, wakati lile kundi la pili si kundi jema wao wapo kwa ajili ya kudhuru, kushawishi kutenda uovu, kukatisha tamaa na kuwapinga wanadamu wenye asili ya uumbaji wa Mungu kwa sura na mfano wake wakitesa na kuua na kuharibu, haya sio mawazo ya kipuuzi kama wanavyo fikiri wana sayansi ambao hawaamini katika mambo yasiyoweza kupimwa na kuthibitika kwa kuonekana kwa macho.Pia huongoza katika njia sahihi. (Kut 23;20-22)

Tunapaswa kuwa na heshima kwa Mungu wetu na kujua mipaka tuliyo nayo, Mungu amewaumba malaika ili awatumie kwa mapenzi yake na sio wana damu kuwa amrisha wanacho taka hatakama ni cha kiovu bali jambo sahihi ni kumwomba Mungu atuagizie malaika hii, walau itapendeza kwani yeye ndiye ajuaye ni malaika yupi atakaye faa, zaidi sana unaweza tu kuzungu mza na malaika ambaye amesha kwisha kutumwa kwako (Lk 1:26-38) hapa utakuta malaika walitumwa ndipo hao wandamu wakaweza kuzungu mza nao, (Waebrania 1;1314 )“ Je yuko malaika aliyemwambia wakati wowote Uketi mkono wangu wa kuume hata nitakapoweka adui zako chini ya nyayo zako? Je hao wote si roho watumikao wakitumwa kuwahudumu wale watakaourithi wokovu? Ninacho taka kumaanisha ni hiki unapotambua malaika waliotumwa kwaajili yako halafu ukazungumza nao ndiyo unaweza kupata msaada kwa mfano inajulikana kuwa kila mwanadamu anamalaika wake walinzi hivyo unaweza kuzungumza nao, lakini kuwaamuru moja kwa moja bila mapenzi ya Mungu  hainogi sana
                                                      
Ni kweli kwamba huenda mwanadamu akawa ni muhimu zaidi mbele za Mungu kuliko malaika lakini lazima tutambue pia kuwa wenda nafasi ya malaika ikawa tofauti na sisi wanadamu kwa kumjua Mungu au kuwa karibu na Mungu “Angalieni, msidharau mmojawapo wadogo hawa, kwa maana nawaambia ya kwamba malaika zao mbinguni sikuzote huutazama uso wa Baba yangu aliye mbinguni” (Math18:10).hivyo kuwa sikiliza na kuwaheshimu ni vema kwani itatusaidia kumjua zaidi Mungu.

Hakuna matukio katika Maandiko ambapo wanadamu waliweza kutoa amri za malaika, ama kwa jina lao au kwa jina la Yesu. Hakuna vifungu ambapo mtu ana mamlaka juu ya kazi ya
malaika. Tunajua kwamba wao ni viumbe wa cheo cha juu, kwa sababu Yesu amejiweka yeye mwenyewe "kiwango cha chini kuliko malaika" ili azaliwa na kuteseka kama mwanadamu (Waebrania 2: 79; Zaburi 8: 4).

Mafundisho kwamba waumini wana mamlaka juu ya malaika ni uongo. Kanuni zifuatazo za Biblia zinaonyesha kwamba malaika hawatii amri za wanadamu:
• Tazama maneno ya Musa "Tulimlilia MwenyeziMungu, naye akakisikiakilio chetu, akatuletea malaika aliyetuondoa Misri" (Hesabu 20:16). Waisraeli hawakuamuru malaika kuja kwao. Walimwomba Mungu, ambaye chini ya amri yake malaika hufanya kazi. Shadraki, Meshaki, na Abednego walikataa kuinamia sanamu ya Nebukadneza (Danieli 3:1718). Mungu kwa rehema yake "alimtuma malaika wake na kuwaokoa watumishi wake"

AMINI KWAMBA UNALINDWA NA JESHI KUBWA SANA LA MALAIKA.

Elisha aliomba maombi ili Bwana amfungue macho mtumishi wake (2Wafalme 6;1317) mara moja mtumishi wa Elisha alifunguliwa macho yake na aliona jeshi kubwa sana la kiroho (malaika), hata ingawa jeshi la washami lilipozwa na Israel walipata ushindi wa bila mapigano lakini tunapata ufunuo mkubwa wa kuweko kwa kundi kubwa la malaika wanao wahudumia wale wanaourithi wokovu. Ikiwa huduma hii kubwa ya malaika ilikuwa hivi wakati wa Elisha ni muhimu kufahamu kuwa nyakati za agano jipya sisi tuko chini ya agano lililo bora zaidi na roho hawa hutumwa kwaajili ya kutuhudumia Biblia inasema hivi katika (Waebrania 1;1314 )“ Je yuko malaika aliyemwambia wakati wowote uketi mkono wangu wa kuume hata nitakapoweka adui zako chini ya nyayo zako? Je hao wote si roho watumikao wakitumwa kuwahudumu wale watakaourithi wokovu?”

Agano jipya pia linatupa ufunuo fulani kuhusu malaika na huduma zao aidha, Paulo mtume alikuwa akiwafundisha wakristo kule Efeso kuwa na ufahamu kuhusu maswala ya ulimwengu wa kiroho, ( Waefeso 6;10-18), ulimwengu wa kiroho unamajeshi makubwa ya makundi ya malaika ,makundi haya yamegawanyika katika sehemu kuu mbili, malaika wateule yaani wale walioonyesha utii kwa Mungu walipopata nafasi ya kutumia utashi wao na kundi linguine ni la malaika walioasi  kutoka katika kundi la malaika wateule lakini waliamua kwa utashi wao kumfuata shetani na hivyo kuwa pamoja na shetani na kumtumikia yeye na kupewa majina mengi yanayofanana na utendaji wao wa kazi majina waliyopewa ni Mashetani,  majini,  mapepo,  roho chafu, maruhani, na kadhalika, jina linalotumika katika Biblia kuhusu viumbe hao ni Pepo wachafu, hili ndilo tutakalolitumia zaidi katika kitabu hiki au somo hili. Ni jambo la furaha sana kujifunza kuhusu malaika.
                                              
                                  MUHIMU
   
Malaika wapo katika uwepo wa Mungu au wanafanya kazi ndani ya ramani au ulimwengu wa Roho wa Mungu, kwasababu wao pia ni rohowema, kumbuka hapa sizungumzii roho au malaika waasi, kwa maana hiyo wapo malaika wema na wabaya malaika wabaya malaika wabaya nikama vile mashetani wanaofanya kazi za kishetani ndio maana ili  malaika wema watusaidie vizuri tunapaswa kuwa watakatifu, hiki ni kitu kinacho wafanya wafanye makao ndani yetu na kuzungukia Mambo yetu yote kila mmoja na kazi yake .

Wao wana ya tambua matakwa ya Roho mtakatifu hata kabla wewe huja yajua ndio maana kuna wakati mtu anaweza kupata ujumbe fulani kiroho halafu akasema ahsante Roho mtakatifu kwa kunipa ujumbe kumbe kunawakati hatujui kuwa ni kweli Roho mtakatifu anatufundisha  lakini kumbe aliye mpa ujumbe  ni malaika wa upashaji wa habari { Gabrieli } .Ufahamu tunapanua hivi. kuna Mungu Baba, Huyu ni roho,  Kuna Mungu mwana huyu ni Mwili na Roho , Kuna Mungu roho Mtakatifu huyu naye ni Mungu Yule Yule lakini ameonekana kwa sura, kazi au kitengo tofauti , hivyo malaika naye ni roho lakini inategemea anajihusisha kufanya nini hawa wote ni roho unapo wafahamu vizuri kunawakati itakusaidia sana nisawa na wakati unakemea pepo,  sawa ni shetani yule yule lakini usipo tambua ni pepo gani ili umlenge moja kwa moja unaweza ukachukua muda sana kumwondoa  sio kwa sababu hauna nguvu za Mungu bali ni kwa sababu haumjui unaye pambana naye.


KWANINI TUWATUMIE MALAIKA KATIKA MAMBO YETU?

Hapa simaanishi kuwaabudu bali  tunapaswa kuwaheshimu na kuwa karibu nao kwani wameumbwa kwaajili ya kumtumikia Mungu katika maisha  yetu wanadamu.

v  Inaonesha hawa pendezewi na mwanadamu kupotea dhambini ndiyomaana mtenda dhambi mmoja anapotubu na kugeuka kumwelekea Mungu, “malaika hushangilia.” (Luka 15:10)
v  Hufanya kituo mahali palipo patakatifu palipo andaliwa  kwaajili ya utukufu wa Mungu mfano ibada n.k
v  Mungu ana watumia sana kuwaimarisha na kuwalinda watumishi wake wa aminifu hapa duniani. (Waebrania 1:14)
v  Wana uwezo wa kukunyakua kutoka juu, ili utue chini kwa usalama (muulize Yesu alipochukuliwa mpaka juu ya mnara wa hekalu ili ajaribiwe ali ambiwa nini na ibilisi ? ndipo utakapo jua kazi kubwa ya malaika ambayo haya ibilisi anaijua)
v  Malaika anaweza kutuongoza mpakapale tulipo tengenezawa(Kut 23;20-22)

v Malaika wanaweza kuwafunga vinywa maadui ikiwa ni mpango wa Mungu mfano; nabii Danieli alitupwa ndani ya shimo la simba, haku umizwa. Kwa nini?  Kwasababu “Mungu wangu mwenyewe alimtuma malaika wake na kufunga vinywa vya simba.” (Danieli 6:22).
v  Malaika wanaweza kukuchukua katika roho na kukupeleka pahala fulani ili kukuonesha mambofulani au kuna wakati unaweza kupelekwa katika altare ya Yesu yaani katika ulimwengu wa kiroho ili Yesu akutatulie mamboyako,( operation iliyoko katika ulimwengu wa  kiroho) hii unaweza ielewa vizuri ukikutana na watu ambao walikuwa na vimbe katika sehemu fulani za miili yao halafu hospitari wakaambia vipimo havisomi lakini baada ya Malaika wa uponyaji kushughirika wakajikuta vimbe zime yeyuka 










USHUHUDA; Mimi mwenyewe niliwahi fanyiwa upasuaji operation/surgery ya shingo ilikuwa haina uwezo wa kugeuka nyuma kalibu wiki zima, pia  niliponywa macho yalipokuwa yaki uma ghafla utadhani yamewekwa pilipili au vumbi lakini huku nikisikiliza wimbo uitwao (ALTARE KWA BWANA YESU NDIO HAZINA YETU MALAIKA NIPELEKENI YESU UNIOKOE ) nikiwa katika muunganiko wa ki-roho na ndipo nilipo gundua kuwa kumbe malaika wana mchango mkubwa sana maishani mwetu, hii ni kwasababu niliomba na kukemea  sana siku nzima lakini sikupona,   nafikiri kuna wakati unatakiwa upelekwe katika wodi la kiroho ili ufanyiwe uchunguzi na Bwana Yesu  pata wimbo huo utafakari. NB; Huu ushuhuda sijaumaiza nikipande tu kwa ufupi.

v   Unaweza kuepushwa na janga fulani ikiwa ni mapenzi ya Mungu kwa mfano; Lutu na binti zake kwa msaada wa malaika wali okolewa na kupelekwa nje ya mji wa Sodoma na Gomora ulio teketezwa kwa moto kutokana na uovu
v   Kwa sababu hata Ibrahimu aliwatumia ili kuwaomba kupunguzwa kwa adhabu.
v   Malaika anaweza kuleta taarifa  .” (Ufunuo 14:6, 7) mfano;  pale kaburini walio kwenda kulitazama kaburi la Yesu malaika akawatokea na kuwaambia kwanini mnamtafuta aliye hai kati ya waliokufa?   Mariamu alipashwa habari na Malaika wa Bwana kuwa ata pata mimba na kumzaa mtoto wa kifamle
Pia taarifa ya kuwa  Sara mke wa Ibrahimu atazaa mtoto mwakani mida kama hii ni malaika walio mtokea Ibrahimu
Tukianza kujifunza juu ya malaika  Mungu ataendelea kutufundisha.

NB: Kunawakati malaika huwapa watu taarifa halafu wao wanasema ni machale yao sasa sijui machale ndio nini .

v   Pia wana uwezo wa kuondoa matatizo yetu mfano ; pale walipo liondoa jiwe katika kaburi la Yesu ili asitoroke .
v   Wanaweza kututia nguvu tunapo ishiwa nguvu , malaika alimtokea  Yesu na “akamtia nguvu.” (Luka 22:43)
v   Petro kutoka gerezani.  Ilikuwa ni kwa msaada wa malaika (Matendo 12:6-11).
v   Wao hufanya makao kwa wale walio safi kiroho wanao pigania utakatifu au wema au usafi (Zaburi 34:7).
NB: Hata hivyo,  ni lazima tukumbuke kwamba malaika wana mtumikia Mungu wala si wanadamu. (Zaburi 103:20, 21) Wanafuata mwongozo wa Mungu bali si maagizo au mao
ya wanadamu. Hivyo, Mungu ndiye tunaye paswa kumuomba msaada, sio malaika. (Mathayo 26:53).

Pia, Maandiko yanatuambia kwamba sala zetu na ibada yetu inapaswa kuelekezwa kwa Mungu peke yake. (Kutoka 20:3-5; Zaburi 5:1, 2; Mathayo 6:9) Malaika waaminifu hututia moyo tufanye hivyo. (Ufunuo 19:10)

Labda Mungu akikwambia uwatume au kuwaagiza na sio kwa mapenzi yako bali msikilize Mungu hii ni kwasababu usije ukadhani unawatuma kumbe wakawa hawa kuelewi maana hauja angalia mapenzi ya Mungu ninini, tambua kwamba malaika wapo makini sana kumsikiliza zaidi Mungu na huu ndiyo uaminifu walio nao.

   MFANO WA KUOMBA MSAADA WA MALAIKA
       
Ee Mungu mwenye nguvu, nina kuja kwako kwa unyenyekevu kupitia  jina la mwanao Yesu kristo nakuomba uniagizie malaika wa vita/wa uponyaji/taarifa/mlinzi/, ili wanisaidie kupigana na maadui zangu kwa jina la Yesu mwanao nimeomba amina.
                                                
                                                 Au

 Mungu Baba ninakuja mbele zako kwa njia ya kristo mwanao mpendwa,  nina jua unanisikiliza daima,  hivyo ninatamani kupata taarifa au ujumbe juu ya  mgonjwa huyu au tatizo……..  kwakuwa wewe ni Mungu wa siri, nina kusihi Bwana na Muumba wangu uniagizie malaika ili anijurishe namna ya kulitatua tatizo hili, maana nina amini utakapo nipa taarifa utanipa na namna ya kulitatua, Roho mtakatifu niongoze kuelewa ujumbe nitakao letewa,ninapopata ujumbe, adui ashindwa kuuiba kwa jina la Yesu amina. (Sasa wakisha kuja hapo ndio unaweza watumia kuwa uliza maswali au kuwaomba msaada zaidi na wao watajua namna ya kukusaidia lakini haya yote lazima uwe na macho ya rohoni)

Nimekupa muongozo huu kwasababu hawa hawana mamlaka kuliko Mungu bali hufuata maagizo ya Mungu  yaani  wao  humtumikia Mungu ila kwa kuwa mimi na wewe tuna wafahamu na kazi zao, basi tuna mwomba Mungu msaada wao ,ni sawa na mtu anapo hitaji msaada fulani  wa wanajeshi, kumsaidia suala fulani,  ni muhimu kumuona kiongozi mkuu ili awatume kukusaidia  na wakitumwa na mkuu hufanya kazi kwa nguvu zote. Sasa kiongozi mkuu wa jeshi la malaika ni yesu kristo ambaye ndiye malaika mikaeli.

Tunawathamini sana malaika hao waaminifu ambao siku zote hutekeleza maagizo ya Mungu! Huwa tumia kuwa saidia na kuwa linda watumishi wake waaminifu walio duniani hii ina tutia sana nguvu  kwa sababu kuna viumbe wa roho hatari ambao wanaitwa roho waovu wanaotaka kutudhuru

NB: Hawa ni baadhi tu ya malaika wapo wengi sana lakini tukiwa na ufahamu tu, juu ya uwepo wao na kazi zao katika maisha ya mwanadamu,  inaweza kutusaidia. Na kazi hizi zote anaye zifanya ni Mungu yuleyule mmoja kupitia jeshi lake la malaika kila mmoja na kitengo chake.
   
SHETANI  HUJIFANYA  KAMA  MALAIKA WA NURU.

kwa kuwa uwiano wa uovu na giza, na uzuri na mwanga, ni mfano inayofanana yenye nguvu katika historia ya mwanadamu. Katika Biblia, nuru ni mfano wa kiroho wa kweli na asili ya Mungu isiyobadilika (Yakobo 1:17). Hutumiwa mara kwa mara katika Biblia kutusaidia kuelewa kwamba Mungu ni mzuri kabisa na wa kweli (1 Yohana 1: 5). Tunapokuwa "katika nuru," tuko pamoja Naye (1 Petro 2: 9).
                                                                                
           
        FAHAMU ZAIDI KUHUSU MALAIKA

·       Malaika wema kazi yao ni kutuombea, kutumwa na Mungu kwetu, na wanatulinda kama Malaika walinzi. (Ebr, 13:2). Ambapo kila
·       Mwanadamu anaMalaika wake wa kumlinda na kumuongoza Roho na Mwili, ndie Malaika wake mlinzi, (Zab, 91:11, Mt. 18:10).
·       Malaika wote sio sawa, wapo Malaika Wakuu, Malaika wanaomtumikia Mungu Mbinguni kwa mfano Makerubi na Maserafi, na pia wapoMalaika walinzi.
·       Malaika wakuu ni Mikaeli, Gabrieli na Raphaeli (Dn, 10:13, Tobiti 12:15, Lk 1:26).
·       Mashetani kazi yao ni kuteswa Motoni na hutaka kudhuru Roho na Miili ya wanadamuna kutupoteza milele. (1 Petro, 5:8, Yoh, 8:44).      
·       Hapo Mwanzo Mungu aliumba Malaika katika hali ya njema na Heri kubwa. Kisha aliumba mbingu na nchi, na viumbe vyotevinavyoonekana na visivyoonekena. (Kol, 1;16, Mwa, 1;31)
·       Malaika ni viumbe vilivyo Roho tupu na vyenye akili na utashi. (Zab 91:11, Ebr 1:7, Uf, 12:7-9).
·       Malaika wengine walikosa kwa kumkaidi Mungu, wakatupwa motoni na ndio Mashetani ambao Mkubwa wao ni Lusiferi. (Yn, 8:44: Uf12:7-9,).
·       Mungu aliumba Malaika ili Wamtukuze, Wafurahi nae Mbinguni na wawe Matarishi/wajumbe wake kwa Wanadamu. (Tob 12:12, Lk.16:22).








            Imeandaliwa na  E.mkinga
NB;kusharea  kwenye makundi ya mitandao mbalimbali ya kijamii kama vile
                                     WatsApp, Instagram ,Twitter,Facebook
                   KISIMA CHA BARAKA
Kisimachabaraka.blogspot.com