Saturday, 1 January 2022

JE YESU NDIYE MALAIKA MKUU MIKAELI?

 HII NI SEHEMU YA KUJIFUNZA NDIOMAANA NIMEANDIKA KUWA HUENDA AKAWA NI NDIYE MALAIKA MKUU KUTOKANA NA VIASHIRIA KADHAA HIVYO KAZI YETU NI KUENDELEA KUTAFAKARI NAKUMWOMBA MUNGU AZIDI KUTUFUNDISHA



*Je Yesu ndiye malaika mkuu Mikaeli?* 


Kama ilivyo kweli, wakati Mkristo wa kweli anapohitaji kuelewa ukweli flani lazima ukweli huo utoke katika Maandiko, kutegemea mawazo ya wanadamu ni hatari kubwa kwa Mkristo yeyote. Biblia inajitafsiri yenyewe na haiitaji utafsiri kutoka nje, kama imemtaja “malaika Mikaeli” pia inaweza kutuambia Mikaeli huyo ni nani, na kama haijatuambia, basi hiyo ni siri ambayo Mungu hakutaka tuifahamu. 


*Lakini Je, Biblia inaonyesha wazi wazi kwamba malaika Mikaeli ni nani? Je malaika Mikaeli ndiye Yesu Kristo?* 




*Je Biblia inathibitisha ukweli huu?* 

*Mwanzo 16:7* “ *Malaika wa Bwana* akamwona kwenye chemchemi ya maji katika jangwa, chemchemi iliyoko katika njia ya kuendea Shuri.”

Katika Mwanzo 16:7-12 *Malaika wa BWANA* alimtokea Hajiri wakati Hajiri alipokuwa anamkimbia bibi yake Sarai mke wa Ibrahimu, *Malaika wa Bwana* huyo akamwambia Hajiri kwamba “Hakika nitauzidisha uzao wako” Mwanzo 16:10, na akamwambia kwamba atazaa mwana na kumwita jina lake Ishmaeli. Baada ya malaika huyo kuondoka, Hajiri “Akaliita jina la Bwana aliyesema naye, *Wewe U Mungu* uonaye, kwani alisema, Hata hapa nimemwona yeye anionaye?” Mwanzo 16:13.

Kulingana na Biblia Hajiri alijua kuwa malaika aliyekuwa anazungumza naye alikuwa ni Bwana Mwenyewe. Harafu baadaye huyo *Malaika wa Bwana* akamtokea tena Hajiri na kumuahidi mambo ambayo malaika wa kawaida hawezi kufanya.

Mwanzo 21:17-18 “ *Mungu* akasikia sauti ya kijana. *Malaika wa Mungu* akamwita Hajiri kutoka mbinguni, akamwambia, Una nini, Hajiri? Usiogope, maana *Mungu* amesikia sauti ya kijana huko aliko. Ondoka, ukamwinue kijana, ukamshike mkononi mwako, kwa kuwa nitamfanya kuwa taifa kubwa.”

Hapa *malaika wa Mungu* anamwambia Hajiri kwamba atamfanya Ishmaeli kuwa taifa kubwa kitu ambacho malaika wa kawaida hawezi kufanya.


Wakati Ibrahimu alipoagizwa na *Mungu* kumtoa kafara mwanawe wa pekee Isaka, katika Mwanzo 22:11-12, *“…malaika wa Bwana* akamwita kutoka mbinguni, akasema, Ibrahimu! Ibrahimu! Naye akasema, Mimi hapa. Akasema, Usimnyoshee kijana mkono wako, wala usimtendee neno; kwa maana sasa ninajua ya kuwa unamcha *Mungu* , iwapo hukunizuilia mwanao, mwanao wa pekee.”

Hapa *malaika wa Bwana* anamwambia Ibrahim kwamba “hukunizuilia mwanao wa pekee” 


*Je malaika wa kawaida anaweza kufanya hivyo?* 

Katika Mwanzo 31 fungu la 11-12 Yakobo anasema, “Na *malaika wa Mungu* akaniambia katika ndoto, Yakobo! Nikasema, Mimi hapa. Akasema, Inua, basi, macho yako, ukaone; mabeberu wote wanaopanda wanyama wana milia, na madoadoa, na marakaraka; maana nimeona yote aliyokutendea Labani. *Mimi ni Mungu* wa Betheli, huko ulikotia mafuta nguzo, na kuniwekea nadhiri. Sasa ondoka, toka katika nchi hii, urudi mpaka nchi ile uliyozaliwa.”

Hapa ni *malaika wa Mungu* anayeongea na Yakobo katika ndoto, harafu malaika huyo anasema kuwa “ *mimi ni Mungu* wa Betheli”, ambaye Yakobo alikuwa amekutana naye katika (Mwanzo 28:20-22). Je malaika wa kawaida aliyeumbwa anaweza kusema *“mimi ni Mungu”* *kama sio Yesu Mwenyewe?* 

Katika Mwanzo 32:22-32 Yakobo akapewa jina la “Israeli”, baadaye Yakobo katika fungu la 30 akasema,

Mwanzo 32:30 “Yakobo akapaita mahali pale, Penueli, maana alisema, *Nimeonana na Mungu uso kwa uso, na nafsi yangu imeokoka.”* 

 *Kulingana na neno la Mungu, hakuna mtu anayeweza kuuona uso wa Mungu Baba* *akaishi* (angalia Kutoka 33:20), *Lakini Yakobo hakufa, hivyo je huyo alikuwa nani?*


Ni wazi kwamba *Yesu* *alionekana kwa watu uso kwa uso na watu hawakufa, na ndiye ambaye hutoa majina mapya, alimpa jina Petro, na Paulo na pia atatupa sisi majina mapya siku ya mwisho.* 

Wakati Yakobo anakaribia kufa wakati anawabariki wanawe katika Mwanzo 48:15-16 alisema, “Akambariki Yusufu, akasema, *Mungu ambaye baba zangu, Ibrahimu na Isaka, walienenda mbele zake, yeye Mungu aliyenilisha, maisha yangu yote, hata siku hii ya leo,* 16 naye *Malaika* aliyeniokoa na maovu yote, na awabariki vijana hawa; jina langu na litajwe juu yao, na jina la baba zangu, Ibrahimu na Isaka; na wawe wingi wa watu kati ya nchi.”

Hivyo Yakobo alitambua kwamba kuna *“Malaika”* aliyemuokoa katika maovu yote, kisha akasema Malaika huyo awabaliki vijana wake, kitu ambacho malaika wa kawaida hawezi kufanya. *Kwa hiyo malaika huyo ni Yesu Kristo Mwenyewe.* 


Tunapita kitabu cha Mwanzo hadi cha Kutoka ambapo tunaona *Malaika huyu wa Bwana alimtokea Musa katika Mwali wa moto.* 

Kutoka 3:2 “ *Malaika wa Bwana* akamtokea, katika mwali wa moto uliotoka katikati ya kijiti; akatazama, na kumbe! Kile kijiti kiliwaka moto, nacho kijiti hakikuteketea.”

3:4 *“Bwana* alipoona ya kuwa amegeuka ili atazame, *Mungu* akamwita kutoka katikati ya kile kijiti, akasema, Musa! Musa! Akasema, Mimi hapa.”

3:6 “Tena akasema, *Mimi ni Mungu* wa baba yako, *Mungu wa *Ibrahimu,* *Mungu* *wa Isaka, na Mungu wa Yakobo. Musa* akaficha uso wake; kwa maana aliogopa kumwangalia *Mungu.”* 


*Je umeona malaika huyu katika fungu la 4 na 6 ameitwa Mungu na Bwana?* *Na Kwanini Musa alificha uso?* Kwa sababu alifahamu fundisho la kwamba *, “hakuna mtu aliyemwona Mungu akaishi”,* lakini kwa kweli huyo hakuwa Mungu Baba bali alikuwa ni *“malaika wa Mungu”,* hata Stefano katika Matendo 7:30-31 anathibitisha ukweli huu

Matendo 7:30-31 “Hata miaka arobaini ilipotimia, malaika  swa *Bwana akamtoke*  katika jangwa la mlima wa Sinai katika mwali wa moto, kijitini. Musa alipouona, akastaajabia maono yale, na alipokaribia ili atazame, sauti ya *Bwana* ikamjia,”


Hapa tunaanza kupata mahusiano kati ya *Yesu* na *malaika* huyu wa *Bwana* , kwa sababu katika fungu la 13-14 Musa alipouliza kwamba wana wa Israeli wakimuuliza jina lake atawambiaje? “ *Mungu* akamwambia Musa, *MIMI NIKO AMBAYE NIKO;* akasema, Ndivyo utakavyowaambia wana wa Israeli; *MIMI NIKO* amenituma kwenu.” Na Yesu katika Yohana 8:58 anasema, “Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambia, Yeye Ibrahimu asijakuwako, mimi niko.”


*Kwanini malaika huyu wakati mwingine anaitwa Mungu au Bwana?* 

Katika Kutoka 13:21 ni “Bwana ndiye anayewatangulia wana wa Israeli katika wingu lililo mfano wa nguzo”, lakini katika Kutoka 14:19 “malaika wa Mungu” ndiye aliyewatangulia wana wa Israeli katika nguzo ya wingu. 


*Je kwanini malaika huyu mara anaitwa Bwana au Mungu?* Mungu Mwenyewe alisema,

Kutoka 23:20,21 “Tazama, mimi namtuma malaika aende mbele yako, ili akulinde njiani na kukupeleka mpaka mahali pale nilipokutengezea. Jitunzeni mbele yake, mwisikize sauti yake; wala msimtie kasirani; maana, hatawasamehe makosa yenu; kwa kuwa jina langu limo ndani yake.”

 *“JINA LA MUNGU”* lilikuwa ndani ya malaika wake, na ndio maana tunaona huyo malaika wa Bwana, anaitwa Bwana, mara Mungu kwa kuchanganya changanya, malaika huyu wa Bwana ni *Yesu Kristo* Mwenyewe ambaye alirithi jina lililotukuka kupita la malaika (angalia Waebrania 1:1-4), na jina hilo ni “Mungu” (Ebr 1:8,9).


Jina linamaanisha pia asili, hivyo kwa kuwa jina la Mungu lilikuwa ndani yake yule malaika; hii inamaana yule malaika naye alikuwa na asili ya Uungu, kitu pekee kinachothibitisha kuwa Yule malaika ni Yesu Kristo Mwenyewe aliyezaliwa zamani za kale na Baba, na kwa kuwa ni Mwana wa Mungu, ana asili na sifa za kiuungu na ana haki ya kutumia jina la Baba yake.


Tukiruka hadi kitabu cha Hesabu tunaona Balaamu pia alikutana na malaika wa Bwana…

Hesabu 22:35 *“Malaika wa Bwana* akamwambia Balaamu Enenda pamoja na watu hawa, lakini neno lile nitakalokuambia, ndilo utakalosema…”

Hesabu 23:4-5 *“Mungu akakutana* na Balaamu;… *BWANA* akatia neno katika kinywa chake Balaamu…”

Katika Hesabu 22:35 malaika wa Mungu ndiye angetia neno katika kinywa cha Balaamu, lakini katika 23:4-5 ni Mungu au Bwana anayetia neno katika kinywa cha Balaamu. Hivyo “malaika wa Bwana”, “Bwana”, na “Mungu” ni majina ambayo yametumiwa kwa kuchanganya changanya. Pia angalia mafungu yafuatayo chini…

Hesabu 22:22 “Hasira ya Mungu ikawaka kwa sababu alikwenda; malaika wa Bwana akajiweka njiani, ili kumpinga…”

23 “Na yule punda akamwona *malaika wa Bwana* amesimama njiani, na upanga wake mkononi mwake amekwisha kuufuta; punda akageuka upande ili kuiacha njia…”

26 “Malaika wa Bwana akaendelea mbele akasimama mahali pembamba sana, hapakuwa na nafasi ya kugeukia mkono wa kuume, wala mkono wa kushoto.”

*

27 “Yule punda akamwona malaika wa Bwana, akajilaza chini…; hasira yake Balaamu ikawaka, akampiga punda kwa fimbo yake.”

31 “Ndipo Bwana akafunua macho ya Balaamu akamwona malaika wa Bwana amesimama njiani, ana upanga mkononi mwake, umekwisha kufutwa naye akainama kichwa, akaanguka kifudifudi.”

32 “Malaika wa Bwana akamwambia…Tazama mimi nimekuja ili kukupinga, kwa sababu njia yako imepotoka mbele zangu.”


 *Je umeona katika fungu la 31 Balaamu “akainama kichwa, akaanguka kifudifudi” kumusujudu malaika wa Bwana?* 

Na malaika huyo akaipokea ibaada bila kusita! 

Na Je pia umeona katika fungu la 32 *malaika wa Bwana* anamwambia Balaamu “njia yako imepotoka mbele zangu,”? Kwa hakika malaika wa kawaida hawezi kupokea ibaada au kutoa madai kama hayo, *malaika huyo alikuwa ni Yesu Kristo* Mwenyewe.

34 “Balaamu akamwambia malaika wa Bwana, Nimefanya dhambi; maana sikujua ya kuwa wewe umesimama njiani ili kunipinga; basi sasa, ikiwa umechukizwa, nitarudi tena.”


 *Tukiruka hadi kitabu cha Waamzi tunaona Gidioni pia alitokewa na malaika huyu wa Bwana…* 

Waamuzi 2:1 “Kisha malaika wa Bwana alikwea juu kutoka Gilgali kwenda Bokimu. Akasema, Mimi nimewaleta ninyi mkwee juu kutoka nchi ya Misri, nami nimewaleta hata nchi niliyowaapia baba zenu; nami nilisema, Mimi milele sitalivunja hilo agano langu nililoagana nanyi;”

Je umeshika hapo? *Malaika wa Bwana hapa anasema “yeye ndiye aliwatoa Waisraeli kutoka Misri”,* *na “aliwaleta kwenye nchi aliyowaahidi baba zao”, tena anadai “hatalivunja agano la milele alilofanya nao”.*  


 *Hata hivyo ukiangalia mafungu yanayofuata utaona kuwa maneno Bwana, malaika wa Bwana/Mungu yametumiwa kwa kuchanganya changanya.* 

16 *“Bwana* akamwambia, Hakika nitakuwa pamoja nawe, nawe utawapiga Wamidiani kama mtu mmoja.”

20 “ *Naye malaika wa Mungu* akamwambia, Itwae nyama na mikate isiyotiwa chachu, uiweke juu ya mwamba huu, ukaumwage huu mchuzi. Akafanya hivyo.”

21 “ *Ndipo malaika wa Bwana* akanyosha ncha ya fimbo ile iliyokuwa mkononi mwake, akaigusa ile nyama na ile mikate; moto ukatoka mwambani, ukaiteketeza ile nyama na mikate; *malaika wa Bwana* akaondoka mbele ya macho yake.”

22 “Gideoni akaona ya kuwa ni *malaika wa Bwana;* Gideoni akasema, Ole wangu, *Ee Bwana MUNGU!* Kwa kuwa nimemwona Bwana uso kwa uso.”

23 *“Bwana* akamwambia Amani iwe pamoja nawe; usiogope; hutakufa.”

Katika fungu la 23 *Bwana* anamhakikishia Gidioni kwamba hatakufa. Kwanini Gidioni aliogopa wakati alipokuwa ameonana na *malaika wa Bwana* uso kwa uso? 

Kwa sababu inajulikana miongoni mwa wateule kwamba mtu akiuona uso wa *BABA* atakufa (angalia Kutoka 33:20), hivyo Gidioni aliogopa, lakini Bwana alimthibitishia kuwa hatakufa, kwa sababu *malaika wa Bwana hakuwa BABA;* *bali alikuwa Yesu Kristo, huyu ndiye Mungu* ambaye watu wanaweza kumwona na wakaishi.


*Katika Waamzi 13* tunaingia katika hadithi ya Mama yake na Samsoni, ambapo tunaona *malaika wa Bwana* alimtokea na kumwelekeza chakufanya kwa mtoto ambaye angemzaa kwa ahadi…

Waamuzi 13:3 *“Malaika wa Bwana* akamtokea yule mwanamke, akamwambia, Tazama, wewe sasa u tasa, huzai; lakini utachukua mimba, nawe utamzaa mtoto mwanamume.”

Kama ukisoma fungu la 9, 13 na 15, utaona kuwa *malaika wa Bwana alimtokea pia* Manoa kumsisitiza chakufanya kwa mtoto atakayezaliwa. *Manoa alipojaribu kumuuliza jina lake yule malaika wa Bwana, alisema “jina langu ni la ajabu”* (angalia Waamuzi 13:18), *Mwenye jina la ajabu kwa kweli ni Yesu Kristo* (angalia Isaya 9:6).

 *Baadaye, malaika wa Bwana* alipoondoka, “Manoa akamwambia mkewe, Hakika yetu tutakufa sisi, kwa sababu *tumemwona Mungu* .” Waamuzi 13:22.


*Sasa nauliza…Kwanini wote hao hawakufa ikiwa walimwona BABA?* Ni kwa sababu *“malaika wa Bwana” hakuwa BABA, bali alikuwa Yesu Kristo Mwenyewe.* Pia *“Hakuna mtu aliyemwona Mungu BABA wakati wowote, ” Yohana 1:18, Yesu peke yake ndiye aliyemwona Mungu (Yohana 5:37: 6:46),* hivyo tunauhakika *malaika wa Bwana* aliyewatokea watu zamani alikuwa ni *Yesu Kristo Mwenyewe.* 


Pia inajulikana vizuri *kwamba Yesu Kristo ni Mwokozi* wetu wa kutuokoa kutoka katika uovu (dhambi) wetu, lakini katika Mwanzo 48:16 *Yakobo anasema “Malaika aliyeniokoa na uovu wote.* 


 *Je inawezekanaje malaika wa kawaida aweze kumuokoa mtu na uovu wake? Kwa hakika hapana! Bali Malaika huyo ni Yesu Kristo* *Mwenyewe.*


*Angalia pia Isaya* anafundisha kuwa malaika huyu aliwaokoa watu wa *BWANA* na kuwaongoza siku zote za kale.

Isaya 63:7-9 inasema, “Nitautaja wema wa *Bwana,* sifa za *Bwana* kwa yote aliyotukirimia *Bwana;* na wingi wa wema wake kwa nyumba ya Israeli, aliowakirimia kwa rehema zake, na kwa wingi wa wema wake. Maana alisema, Hakika ndio watu wangu hawa, wana wasio na hila; akawa Mwokozi wao. Katika mateso yao yote yeye aliteswa, na malaika wa uso wake akawaokoa; kwa mapenzi yake, na huruma zake, aliwakomboa mwenyewe; akawainua, akawachukua siku zote za kale.”

Hebu zingatia hapa Isaya anatuambia *“malaika wa uso wake” Bwana, neno “uso* ” la kiebrania ni “ *panim* ” na limetafsiriwa katika KJV kama *“presence* ”. Hivyo Malaika huyo ambaye alikuwa kama “uwepo wa *Bwana* ” pia jina la Bwana lilikuwa ndani yake alikuwa anamwakilisha *BWANA MWENYEWE* , na hawezi kuwa mtu mwingine tofauti na *Yesu Kristo Mwana* *Wa Mungu aliye hai, ambaye ni Mwokozi* wetu sisi. Isaya katika fungu la 9 anatuambia kuwa *malaika* huyu aliwaokoa, na kuwakomboa, na aliwaongoza watu wa Mungu katika siku zote za kale.


 *Je Malaika wa Bwana anaweza kuwa ndiye malaika mkuu Mikaeli?* 

Zekaria 3:1-2 inasema, “Kisha akanionyesha Yoshua, kuhani mkuu, amesimama mbele ya *malaika wa Bwana* , na Shetani amesimama mkono wake wa kuume ili kushindana naye. *Bwana* akamwambia Shetani, *Bwana na akukemee* Ewe Shetani; naam, *Bwana* , aliyechagua Yerusalemu, na akukemee; je! Hiki si kinga kilichotolewa motoni?”

Hapa tunamwona *malaika wa Bwana akimwambia* shetani kwamba”Bwana na akukemee”, Ukisoma fungu la 3 utaona Yoshua alikuwa amevaa *“mavazi machafu” hii inawakilisha dhambi.* Halafu shetani akaja kwa Yoshua akidai kuwa yuko upande wake, na *malaika wa Bwana* hivyo hivyo, alikuja kumuondolea Yoshua uovu wake, hivyo akamwambia shetani kwamba *Bwana na akukemee.*


*Je ni wapi tena tunaona jambo kama hili hili?* 

Yuda 1:9 inasema, *“Lakini Mikaeli, malaika mkuu,* aliposhindana na Ibilisi, na kuhojiana naye kwa ajili ya mwili wa Musa, hakuthubutu kumshitaki kwa kumlaumu, bali alisema, Bwana na akukemee.”

Hapa tunaona kama hilo hilo lilitoke wakati wa Musa, na *malaika aliyefanya hivyo ni Mikaeli malaika mkuu;* *kwa hakika “malaika wa Bwana” ndiye “Mikaeli”.* Kumbuka shetani pale bado hajatupwa chini alikuwa na nafasi ya tatu mbinguni kwa ukuu, na alipoasi nafasi yake ikachukuliwa na “Gabrieli” ambaye alikuwa mdogo kwake; pia shetani hakunyanganywa nguvu zake alizokuwanazo mwanzo, hivyo malaika ni wadogo kwake, na Mungu alimtuma *Yesu Mwenyewe ambaye alimuumba shetani* kwenda kupambana naye. Kwa *hakika Malaika Mkuu Mikaeli ni Yesu Mwenyewe.* 


Angali jinsi Paulo anavyolitumia neno hilo kwa *Yesu.* 

1 Wathesalonike 4:16 “Kwa sababu *Bwana mwenyewe* atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, *na sauti ya malaika mkuu,* na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza.”

Hapa Yesu atakuja na *“sauti ya malaika mkuu”* kuwafufua wafu. *Na katika Biblia nzima jina “malaika mkuu” limetumika kwa “Mikaeli” peke yake (Yuda 1:9). Na Yohana 5:26-29 inatuambia kuwa wafu wataisikia “sauti ya Mwana wa Mungu”* nao watafufuka. Hivyo *sauti ya malaika mkuu* itakayofufua wafu, *ndiyo sauti ya Mwana wa Mungu, na Mikaeli malaika mkuu ni Yesu Kristo Mwenyewe.* 

Musa alikufa katika mlima alioagizwa na *Yehova* , na Yuda 1:9 inatuambia shetani na *malaika mkuu Mikaeli* walikuwa wakishindania mwili wake, hivyo tunajua kuwa *Musa alifufuliwa na malaika mkuu Mikaeli na akapelekwa mbinguni!*


Na ni kwanini Paulo katika 1 The 4:16 anasema *“sauti ya malaika mkuu” itafufua wafu siku ya mwisho?* Na tunajua hakuna mwingine awezaye kufufua wafu tofauti na *Yesu Kristo Mwana wa Mungu* , 

 *Hivyo Mikaeli ni Yesu Kristo Mwenyewe.* 


Pia angalia kwamba, *malaika Mikaeli* baada ya matukio yote kuisha siku ya mwisho atasimama kuja duniani kuwafufua na kuwaokoa watu wake.

Danieli 12:1,2 inasema, “ *Wakati huo Mikaeli atasimama, jemadari mkuu,* asimamaye upande wa wana wa watu wako;…na wakati huo watu wako wataokolewa; kila mmoja atakayeonekana ameandikwa katika kitabu kile. Tena, wengi wa hao walalao katika mavumbi ya nchi wataamka, wengine wapate uzima wa milele, wengine aibu na kudharauliwa milele.”

Yohana 5:28,29 “Msistaajabie maneno hayo; *kwa maana saa yaja, ambayo watu wote waliomo makaburini wataisikia sauti yake.* Nao watatoka; wale waliofanya mema kwa ufufuo wa uzima, na wale waliotenda mabaya kwa ufufuo wa hukumu.”

Zingatia kwamba, Paulo katika 2 The. 2:16 anafundisha kwamba, *Yesu atakuja na “sauti ya malaika mkuu” kufufua wafu,* halafu Danieli anafundisha katika 12:1,2 kwamba, *“Mikaeli malaika mkuu” ndiye atakayefufua wafu,* *na kuwahukumu, na kuwaokoa watu.* Na Je, umeona Yohana 5:28,29 inasema kuwa *“sauti ya Yesu Mwana wa Mungu” ndiyo itafufua wafu, na kuwahukumu?* Haiwezi kuelezeka wazi zaidi ya hivi, kama mtu ana njaa na ukweli wa Maandiko ambao ni “mstari juu ya mstari, na kanuni juu ya kanuni”, au Mkristo yeyote mwaminifu kwa hakika hawezi kukataa ushahidi wazi kiasi hiki.


 MUNGU; ambaye hutumwa na BABA yake, pia alitumwa kuja kuokoa ulimwengu. Ukweli huu hauwezi kupokelewa na madhehebu ya wanautatu, kwa sababu hawataki kuacha mafundisho ya Kupinga-Kristo ya kanisa Katoliki ambayo hayapo kwenye Biblia. Na kwa kuthibitisha zaidi kwamba Yesu *ni malaika mkuu Mikaeli,* ngoja tuangalie ukweli zaidi ambao hauwezi kupingika.


Zingatia Danieli 12:1 inamwita Mikaeli kama *“Jemedari Mkuu” (Great Prince), na katika Ufunuo 12:7 “Mikaeli na Malaika* zake anapigana na shetani na malaika zake”. Shetani ni mkuu wa malaika zake na malaika zake humwabudu yeye na kutii amri zake; na malaika zake ni jeshi lake, vivyo hivyo *Mikaeli ni mkuu wa malaika zake, na malaika zake ni jeshi lake, nao humwabudu yeye na kutii amri zake (Ebr 1:6-7), na hivyo Yesu ni Jemedari au Amili Mkuu wa jeshi (malaika) la BWANA;*

 zingatia jinsi jeshi la malaika zake wanavyopigana na shetani katika Ufunuo 12:7, halafu angalia Yoshua anavyoonyesha ukweli usiopingika uliopo kati ya *Yesu na Mikaeli.* 

Yoshua 5:13-15 inasema, “Ikawa hapo Yoshua alipokuwa karibu na mji wa Yeriko, akainua macho yake na kuangalia, na tazama, *mtu mume akasimama kumkabili mbele yake,* naye alikuwa na upanga wazi mkononi mwake; Yoshua akamwendea, na kumwambia, Je! Wewe u upande wetu, au upande wa adui zetu? Akasema, La, Lakini nimekuja sasa, nili amiri wa *jeshi la BWANA.* Yoshua akapomoka kiusouso hata chini, naye akasujudu, akamwuliza, *Bwana wangu* aniambia nini mimi mtumishi wake? *Huyo amiri wa jeshi la Bwana* akamwambia Yoshua, Vua viatu vyako miguuni mwako; kwa kuwa mahali hapo usimamapo ni patakatifu. Yoshua akafanya vivyo.”

 *Je umeshika hapo?* 


*Huyu Jemedari au Amiri wa jeshi la BWANA* katika Danieli 12:1 ni *Mikaeli,* na hapa Yoshua anapomoka kiusouso ili kumwabudu lakini Yeye hamzuii, bali anaipokea ibaada ya Yoshua kana kwamba anaistahili kabisa. Na *kulingana na Maandiko hakuna mtu mwingine Yeyote tunayeruhusiwa kumwabudu tofauti na Mungu Mwenyewe na Mwanawe Yesu Kristo, Hivyo Amiri huyo kwa hakika ni Yesu Kristo Mwenyewe.* 


Na Je umeona jinsi ambavyo “Amiri” huyo hata anamwambia Yoshua kuwa mahali aliposimama ni patakatifu, na kwamba avue viatu kama vile *“malaika wa Bwana”* alivyomwambia Musa katika kutoka 3:2-5? Ukweli uko wazi sana, *malaika mkuu Mikaeli ndiye Yesu; tatizo watu wamepofushwa na fundisho la utatu, ndio maana wengine wanaweza kukataa ushahidi makini ambao Biblia inafunua wazi.* 

 *Kwa sababu huyu “malaika wa Bwana”, “Amiri wa jeshi la Yehova” na “Jemedari Mkuu” Mikaeli Mwenyewe anapokea ibaada,* hivyo hawezi kuwa malaika wa kawaida, bali *ni Yesu Kristo Mwenyewe Mwana wa Mungu.*


*Angalia jinsi malaika aliyeumbwa hawezi kukubali kupokea ibaada.* 

Ufunuo 19:10 “Nami nikaanguka mbele ya miguu yake, ili nimsujudie; *akaniambia, Angalia, usifanye hivi; mimi ni mjoli wako na wa ndugu zako walio na ushuhuda wa Yesu.* *Msujudie Mungu.” (Angalia pia 22:8,9)* 


 *Pia zingatia kwamba Mikaeli huitwa “Mkuu”(Prence),* *Na Je unajua kuwa Yesu Kristo ndiye “Mkuu”? Danieli 12:1 inasema, “Wakati huo Mikaeli* *atasimama, jemadari mkuu (the great Prince), asimamaye upande wa wana wa watu wako;…”* 

 *Danieli 10:13* “Lakini mkuu wa ufalme wa Uajemi alinipinga siku ishirini na moja; bali, tazama, huyo *Mikaeli,* mmoja wa hao wakuu wa mbele, akaja kunisaidia;”

Kumbuka: Danieli 10:13 *imetafsriwa vibaya kwa kusema Mikaeli ni “mmoja wa wakuu wa mbele”, neno “mmoja” linatokana na neno la kiebrania “echad” ambalo linamaanisha pia “-a kwanza”, hivyo likitafsriwa vizuri litamaanisha malaika mkuu Mikaeli ni “Mkuu wa kwanza wa wakuu” (Chief Prince of the princes).

Danieli 10:21 “Lakini nitakuambia yaliyoandikwa katika maandiko ya kweli; wala hapana anisaidiaye juu ya hao ila huyo *Mikaeli, mkuu wenu (your Prince).”* 


 *Je Yesu Kristo ndiye Mkuu huyo ambaye ni Mikaeli?* Kumbuka neno “mkuu” la kiebrania lilolotumika kwa Yesu na kwa Mikaeli ni שָׂר‎ (sar) ambalo kwa uhalisi linamaanisha *“mwana mfalme”,* kwa kiingereza limetafsiriwa kama *“prince”,* neno *sar* linamaanisha “Mkuu ambaye ni *mwana wa Mfalme”,* au kwa uhalisi *“mwana wa mfalme ambaye ni mtawala”.*


 *Kama malaika mkuu Mikaeli ni* *“Mwana wa Mfalme”* mbinguni, hawezi kuwa *mtu* yeyote ila *Yesu Mwenyewe* . Na Je unajua kuwa Yesu ndiye “Mwana Mfalme” au “Mkuu” huko mbinguni? Angalia mafungu yafuatayo ambayo yanamwita Yesu “Mkuu”(Prince) kama vile Mikaeli alivyo.

Danieli 9:25 “Basi ujue na kufahamu, ya kuwa tangu kuwekwa amri ya kutengeneza na kuujenga upya Yerusalemu hata zamani zake masihi aliye mkuu (prince);…”

Danieli 8:25 “…naye atasimama kushindana naye aliye *Mkuu wa wakuu; (Prince of princes)* lakini atavunjika, bila kazi ya mikono.”

Isaya 9:6 *“Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, Tumepewa mtoto mwanamume; Na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake; Naye ataitwa jina lake, Mshauri wa ajabu, Mungu mwenye nguvu, Baba wa milele, Mfalme(sar) wa amani.”* 


Matendo 3:14 “mkamwua yule *Mkuu wa uzima (Prince of life),* ambaye Mungu amemfufua katika wafu; na sisi tu mashahidi wake.”


Matendo 5:31 “Mtu huyo Mungu amemtukuza kwa mkono wake wa kuume, awe *Mkuu na Mwokozi (Prence and Seviour)* , awape Waisraeli toba na msamaha wa dhambi.”


 *Ufunuo 1:5 “…Yesu Kristo, shahidi aliye mwaminifu,* *mzaliwa wa kwanza wa waliokufa, na mkuu wa wafalme (Prince of kings) wa dunia…”* 


 *Hivyo, Yesu ndiye Mkuu huyo malaika mkuu ambaye ni Mikaeli,* haiwezi kuelezewa wazi zaidi ya hapa, kwa hiyo tunaona kuwa Yesu alikuwepo tangu zamani katika Agano la kale kama “malaika wa Bwana”, na jina la Bwana lilikuwa ndani yake; *Yeye alikuwa Mwana wa Mungu tangu zamani kabla dunia haijaubwa.* Hii inathibitisha kuwa fundisho la utatu ni uongo; kwa maana linasema kwamba Yesu ni Mungu yuleyule mmoja, ambaye alishuka kutoka mbinguni *akachukua asili ya ubinaadamu kwa kuzaliwa kule Bethlehemu kama Yesu,* ndipo kuwepo kwa Yesu kukaanza rasmi, lakini Biblia haisemi vinginevyo; *hivyo tuna uhuru wa kuchagua, aidha kuamini inachokisema Biblia  wala Yesu.*

Friday, 6 September 2019

Co-peration firm


                                        
                         KARIBU KISIMA CHA BARAKA                                     
                                                                     

Jifunze mambo mbalimbali kupitia Kisima cha baraka cooperation firm . ni umoja unaokupa fursa kubwa ya kubadirishana mawazo na wengine duniani ili kuleta ufahamu sahihi na chanya  katika mambo tofauti tofauti kimaadili kwa maendeleo bora. Fundisha Mambo ya kiroho na kimwili kwa kuzingatia maadili mema,jifunze,tangaza  pia biashara yako nk.
                      Blog 
  Andika kisima cha baraka
                               YouTube    
https://www.youtube.com/channel/UC3ZaFWsTDp2mMWUGiemC4mwUC3ZaFWsTDp2mMWUGiemC4mw. 
                     Whatapp 
https://chat.whatsapp.com/EFaLiohw0LhL1931A3pKGQEFaLiohw0LhL1931A3pKGQEFaLiohw0LhL1931A3pKGQEFaLiohw0LhL1931A3pKGQEFaLio
     Kupitia group hili utaunganishwa na group la biashara




Friday, 10 November 2017

INGIZA NYIMBO ZAKO ZA GOSPEL YOU TUBE BURE KABISA


                                

                                                      FURAHIA OFAAA!!!
             
                                        
                                              



Tuna kujuza Kuwa ikiwa unahitaji njimbo zako zionekaze mtandaoni ,basi tutafutekwanamba 0757250806.  Utawekewa nyimbo zako you tube buuuree kabisa barikiwa, mtaarifu na mwenzako




MWONGOZO WA KUWAJUA MALAIKA WATENDAO KAZI NA MUNGU


  1.   MWONGOZO WA KUWAJUA MALAIKA WATENDAO   KAZI NA MUNGU MBINGUNI NA DUNIANI NA NAMNA WANAVYO TENDA KAZI.
Najua umesha soma vitabu vingi au kuangalia mahubiri mbali mbali yanayo zungumzia kuwajua mapepo au majini na majina yao, sasa leo naomba tujifunze japo kwa ufupi juu ya malaika   ili tujue namna wanavyo fanya kazi kama wajumbe wa baraza la mbinguni kwani ufahamu huu utatufanya tuwe karibu na Mungu kama wengine wanavyo tumia mapepo au wanavyo kuwa karibu na majini.   karibu twende pamoja

 MFANO WA MUONEKANO WA MALAIKA
                             


                                                       
                       MALAIKA NINANI?

Neno la kiingereza "angel" linatokana na neno la kigiriki "angelos" lenye maana ya "Mjumbe" katika Agano la Kale, pia kwa Kiebrania neno "malaika" ni "malak" pia lina maana ya "mjumbe". Nabii malaki alipata jina lake kutoka neno hili. Yeye mwenywe alikuwa mjumbe na alitabiri kuhusu kuja kwa mjumbe wa agano ambaye ni Yesu Kristo (Malaki 3:1) Ingawaje neno malaika katika Biblia, maana yake ni mjumbe, karibu mara nyingi hutumika kwa viumbe wa mbinguni, pengine hutumika kwa wajumbe ambao ni wanadamu. Pia ni viumbe wenye uweza mkuu sana (2 Petro 2: 11)

Kwa Mujibu wa katekisimu katoliki Malaika ni roho tupu walioumbwa na Mungu, ili wamtukuze milele, wamlinde kila mtu na kumtumikia Bwana Yesu katika kutuokoa. “Angalieni, msidharau mmojawapo wa wadogo hawa, kwa maana nawaambia ya kwamba malaika zao mbinguni sikuzote huutazama uso wa Baba yangu aliye mbinguni” (Math18:10).

Hawa ni viumbe (Roho) au wajumbe walioumbwa na Mungu kwa ajili ya kufanya kazi ya Mungu kazi ya kuwatumikia wanadamu na kumtukuza Mungu mbunguni. Kwa ufupi wao wapo kwaajili ya kumtumikia Mungu,  Neno “malaika” humaanisha “Mjumbe.” Wa habari za Mungu kwa mwanadamu malaika wapo wa aina mbalimbali na vitengo tofauti hili linathibitishwa pale biblia inapo sema kuwa kuna malaika mkuu (Angels: God’s Messengers)  ( Danieli 12; 7 ), (Yuda 1;9 ), kwahivi ikiwa kuna malaika mkuu basi wapo na wengine wenye vitengo vinavyofuata au tofauti na mkuu.

Katika Agano la kale malaika wa Mungu anajulikana (sio kutokana na umbo lake) kwa habari njema anayo leta; mara nyingi anaonekana kama mtu. Maranyingi  si rahisi kubainisha  tofauti kati ya Mungu na huyo mleta habari njema  wake( Kutoka 3;2-6) kwa nje ubainisho kati yake na mtu unaelezwa kwa majina ya kiebrania  “Serafi” ambao ni viumbe wa mbinguni wanaozunguka kiti cha enzi na “Makerubi” ambao wanaonekana kama walinzi wa mahali patakatifu na bustani ya Edeni.

                            


                      SIFA ZA MALAIKA   

v Malaika wana tabia au uwezo wa kujibadirisha kwa mfano wa kitu chochote kulingana na mazingira mfano;  anaweza kuwa jiwe au kuwa kama Binadamu ,  Mti, Nyumba n.k, kwa mfano; wale malaika walio mtokea Ibrahimu. (Ebrania 13:2)
v Malaika wanaweza kuasi: (Yuda 1:6)(Ezekieli 28:17,)( Isaya 14:12-15.)
v Malaika wanazo nguvu nyingi. ( 2 Petro 2:11)

KUNA MALAIKA WA NAMNA AU AINA AU NGAZI TOFAUTI TOFAUTI KAMA IFUATAVYO

Kuna malaika wa aina nyingi tofauti tofauti na idadi yao haijatajwa waziwazi hii ni kudhihirisha kwamba ni jeshi kubwa sana linalo jumuisha vitengo tofauti tofauti vya malaika, ndiyo maana tutajifunza japo kwa uchache ili tuwe na mwanga tu utakao tuongoza kufahamu zaidi (Ufunuo 5;11)hapa  katika kitabu hiki Biblia ina sema Yohana aliona malaika wengi sana elfu kumi mara elfu kumi na  elfu mala elfu  ni ni kuonesha kwamba walikuwa wengi hata hakumbuki idadi au haijui idadi yao alio waona (Luka 2:13,) (Danieli 7;10), (Waebrania 12:22.)

1.    Malaika mwenye nguvu na mwenye mamlaka zaidi ni Mikaeli (malaika wa vita) au Yesu Kristo, yule malaika mkuu. (1 The 4:16)”Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na Parapanda ya Mungu; naowalio kufa katika kristo watafufuliwa kwanza”. Pia soma  (Yuda1; 9)
-         Mikaeli ambaye ni malaika mkuu anawaongoza malaika wote watakatifu,  na jina lake linamaanisha "Nani  kama Mungu?"au ‘ambaye ni kama Mungu,  (Danieli 11:1, 12: 1, 1 Wathesalonike 4:16; Yuda 1: 9; Ufunuo 12: 710). Unapo soma maeneo mbalimbali kwa mfano (Lk 10:18) yanaonesha kuwa na uthibitisho wa kwamba wenda Bwana Yesu akawa ndiye malaika mikaeli , Sasa swali; katika usomaji  wako wa maandiko, nani ambaye ni kama Mungu halafu tena ni kama binadamu  zaidi ya Yesu na je jina Bwana ni la nani zaidi ya Yesu?

v  (Kwa mujibu wa vitabu mbalimbali vya kiroho), “JINA LA MUNGU” lilikuwa ndani ya malaika wake, na ndio maana tunaona huyo malaika wa Bwana, anaitwa Bwana, mara Mungu kwa kuchanganya changanya, malaika huyu wa Bwana ni Yesu Kristo Mwenyewe ambaye alirithi jina lililotukuka kupita la malaika (angalia Waebrania 1:1-4), na jina hilo ni “Mungu” (Ebr 1:8,9). Jina linamaanisha pia asili, hivyo kwa kuwa jina la Mungu lilikuwa ndani yake yule malaika; hii inamaana yule malaika naye alikuwa na asili ya Uungu, kitu pekee kinachothibitisha kuwa yule malaika ni Yesu Kristo mwenyewe aliyezaliwa zamani za kale na Baba, na kwa kuwa ni mwana wa Mungu, ana asili na sifa za kiuungu na ana haki ya kutumia jina la Baba yake.
v Zekaria 3:1-2 inasema, “Kisha akanionyesha Yoshua, kuhani mkuu, amesimama mbele ya malaika wa Bwana, na Shetani amesimama mkono wake wa kuume ili kushindana naye. Bwana akamwambia Shetani, Bwana na akukemee Ewe Shetani; naam, Bwana, aliyechagua Yerusalemu, na akukemee; je! Hiki si kinga kilichotolewa motoni?”
v  Hapa tunamwona malaika wa Bwana akimwambia shetani kwamba”Bwana na akukemee”, Ukisoma fungu la 3 utaona Yoshua alikuwa amevaa “mavazi machafu” hii inawakilisha dhambi. Halafu shetani akaja kwa Yoshua akidai kuwa yuko upande wake, na malaika wa Bwana hivyo hivyo, alikuja kumuondolea Yoshua uovu wake, hivyo akamwambia shetani kwamba Bwana na akukemee. Je ni wapi tena tunaona jambo kama hili hili?
v  Yuda 1:9 inasema, “Lakini Mikaeli, malaika mkuu, aliposhindana na Ibilisi, na kuhojiana naye kwa ajili ya mwili wa Musa, hakuthubutu kumshitaki kwa kumlaumu, bali alisema, Bwana na akukemee.”
v  Hapa tunaona kama hilo hilo lilitoke wakati wa Musa, na malaika aliyefanya hivyo ni Mikaeli malaika mkuu; kwa hakika “malaika wa Bwana” ndiye “Mikaeli”.
v  Danieli 12:1,2 inasema, “Wakati huo Mikaeli atasimama, jemadari mkuu, asimamaye upande wa wana wa watu wako;…na wakati huo watu wako wataokolewa; kila mmoja atakayeonekana ameandikwa katika kitabu kile. Tena, wengi wa hao walalao katika mavumbi ya nchi wataamka, wengine wapate uzima wa milele, wengine aibu na kudharauliwa milele.”
v  Zingatia Danieli 12:1, inamwita Mikaeli kama “Jemedari Mkuu”, na katika Ufunuo 12:7 “Mikaeli na Malaika zake anapigana na shetani na malaika zake”. Shetani ni mkuu wa malaika zake na malaika zake humwabudu yeye na kutii amri zake; na malaika zake ni jeshi lake, vivyo hivyo Mikaeli ni mkuu wa malaika zake, na malaika zake ni jeshi lake, nao hutii amri zake (Ebrania 1:6-7
. Ukiona mambo hujayapata kama inavyotakiwa maana yake yupo azuiaye.Yupo saizi ya ibilisi ambaye anaitwa Malaika Mikaeli. Shetani alikuwa malaika lakini alimwasi Mungu na Mikaeli ndiye aliyemshughulikia.
Ukiona mambo kwenye maisha yako yameshindikana usifikiri Mungu hajakusikia maombi yako na amekuacha, kuna kizuizi cha mkuu wa anga mahali ambaye amekuzuia na huyo lazima ashughulikiwe na yale majibu yako yaje kwako kwa jina la Yesu.  
                                
2.    Maserafi,  makerubi,
3.    Rafaeli ( Malaika wa Uponyaji),pia kuna
4.    Gabrieli (Malaika wa taarifa) hawa ni baadhi tu , Gabrieli ni mmoja wa wajumbe wakuu wa Mungu, jina lake linamaanisha "shujaa wa Mungu," au Mungu ni nguvu yangu , na alipewa ujumbe muhimu kama vile ujumbe aliopewa Danieli (Danieli 8:16;9:21), aliopewa Zekaria (Luka 1: 18 19), na Maria (Luka 1: 2638). (Luka 2:9-14 )
Hawa ni baadhi tu.

       JE MALAIKA WALIKUWAPO TANGU LINI
           
Malaika waliumbwa zamani kabla ya dunia kuumbwa, ( Mwanzo 1:1-) Viumbe vyote vya kiroho viliumbwa wakati huu kabla ya mwanzo, hakuna aliyekuwa akiishi. Mungu aliwapa uzima kwanza kisha, wakashuhudia uumbaji mwingine. Mungu alipo iumba dunia malaika walipaaza sauti zao na kushangilia (Ayubu 38:4-7), na kwa njia ya kristo Yesu vitu vingine vikaumbwa (Wakolosai 1:13-17) nao hawaoi wala kuzaa (Marko 12;25).          

Pia viumbe vyote vya kiroho vinamwabudu Mungu. Mungu ni mkuu kuliko mapepo na malaika wote. Aliishi kabla yao na aliwaumba. Watu wengi kanisani mwetu wana mawazo ya juu sana kuhusu malaika na viumbe vya kiroho; wanaongelea malaika na mapepo kana kwamba hao ndio Mungu.( (Nehemia 9:6) (Malaika na viumbe vya kiroho sio Mungu bali vinamwabudu Mungu.)
    
                          MAKERUBI.

Makerubi wana husianishwa na kiti cha enzi cha Mungu ,Yaani Mungu huketi juu yao. Mungu huketi juu ya Makerubi (Zaburi 80:1) (Zaburi 99:1) (Ezekieli 10:1, 2.). "makerubi,"  ni viumbe hai ambao hulinda utakatifu wa Mungu kutoka kwa uchafu wowote wa dhambi (Mwanzo 3:24; Kutoka 25:18, 20)
Pia ni aina ya Malaika wanao beba uwepo wa Bwana, ni malaika wangazi ya juu mbele ya Bwana, (Ezekieli 28;13-18) pia yeye huonekana kwa sura za wanyama zaidi ,(Ezekieli 10;1-22 )na hasa kuanzia mstari wa 10;10 -17 maandiko yana mwita kuwa ni kerubi afunikaye (Ezekieli 28;13-18 ).
Ngazi hii ya kerubi ndiyo ambayo hata shetani alikuwa hapa katika ngazi hii ya Malaika (Ufunuo 12;7,) Ndiposa katika kitabu  hiki cha ufunuo 12 tunaona kuwa Mikaeli kama malaika mkuu akiwa na malaika wengine walio chini yake wakishirikiana katika vita.

Makerubi ndio wa kwanza kutajwa katika Biblia katika (Mwanzo 3:24, )"Basi akamfukuza huyo mtu, akaweka Makerubi, upande wa mashariki wa bustani y Edeni, na upanga wa moto uliogeuka huko na huko, kuilinda njia ya mti wa uzima." Na kama tulivyo tangulia kusema ya kuwa Kabla ya shetani kufanya  uasi wake, shetani alikuwa kerubi soma (Ezekieli 28:12-15).Na baada ya kuasi akageukana kuwa malaika mwasi, Na hata sanduku la agano pamoja na makala zake zilizomo zilikuwa na uwakirishi wa makerubi . (Kutoka 25:17-22), (kutoka 26:1-31),(kutoka36:8; 1),( Wafalme 6:23-35); (wafalme 7:29-36; 8:6-7), (1 Mambo ya  Nyakati 28:18; 2),( Mambo ya Nyakati 3:7-14; 2),( Mambo ya Nyakati 3:10-13; 5:7-8), (Waebrania 9:5)
(Ufunuo 4:6-9) pia inaonekana kuelezea juu ya makerubi. Makerubi hutumikia kwa kusudi la kutukuza utakatifu na nguvu za Mungu. Hii ni mojawapo ya jukumu lao kuu kama tunavyojifunza katika Biblia. Mbali na kuimba sifa za Mungu, wao.

Sura ya 1 na 10 ya kitabu cha Ezekieli huelezea "wale viumbe hai wanne" (Ezekieli 1:5) kuwa viumbe hawa ni sawa na makerubi (Ezekiel 10). Kila mmoja alikuwa na nyuso nne -ule wa mtu, simba, ng'ombe, na tai (Ezekieli 1:10;) pia 10:14) , na kila mmoja alikuwa na mabawa manne. Katika muonekano wao, makerubi "walikuwa na sura ya mwanadamu" (Ezekiel 1:5). Makerubi hawa walitumia mbili ya mbawa zao kwa kuruka na zingine mbili kwa ajili ya kufunika miili yao (Ezekieli 1:6, 11, 23). Na ndiyo maana wanaitwa Kerubi afunikaye, pia chini ya mabawa yao makerubi walionekana kuwa na umbo lenye mfano wa mkono wa mwanadamu (Ezekieli 1:8; 10:7-8, 21).

Hivyo tunaweza kusema Kiti cha Enzi cha Mungu kinazungukwa na wanyama wanne wenye vichwa tofauti. Hawa ni Simba, Ndama, Tai na Mwanadamu, wanatambulikana kama Makerubi na wana mabawa sita wanakizunguka Kiti cha Enzi cha Mungu (Ufunuo 4:6-9). Wameumbika katika viungo mchanganyiko, katika Ezekieli wakiwa walinzi wa Yehova wa Israeli na wanaonekana wenye mabawa manne katika viwiliwili vyao vya juu. Hapa hawajatajwa kuwa na mabawa mawili katika miguu yao kama wale Makerubi wanaokizunguka Kiti cha Enzi cha Mungu, au wale wa moto katika Agano la Kale. Idadi ya hao Makerubi kuwa wanne inatokana na Uumbaji.
                                   MASERAFI
                                           
Maserafi ni viumbe, malaika wanao husishwa na maono ya nabii Isaya juu ya Mungu wake katika hekalu wakati Mungu alimwita kwa huduma yake ya unabii (Isaya 6:1-7). Sasa ukisoma katika.  ( Isaya 6:2-4 ), Maandiko yanasema  " Juu yake walisimama maserafi; kila mmoja alikuwa na mabawa sita; kwa mawili alifunika uso wake, na kwa mawili alifunika miguu yake, na kwa maawili aliruka. Wakati, kila mmoja na mwenzake, wakisema, Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu, ni Bwana Mungu wa majeshi; Dunia yote imejaa utukufu wake. Na misingi ya vizingiti ikatikisika kwa sababu ya sauti yake aliyelia, nayo nyumba ikajaa moshi".

Pia hawa ni viumbe wanao mwabudu Mungu Maserafi ;( Isaya 6:1-3)

Viumbe hawa pia waliwahi kujihusisha na utakaso kwa ajili ya nabii Isaya wakati yeye alianza huduma yake ya kinabii. Mmoja aliweka makaa ya mawe ya moto juu ya mdomo wa Isaya "Tazama hili limekugusa midomo yako, na uovu wako umeondolewa, na dhambi yako imefunikwa" (Isaya 6:7).   maserafi nao ni watiifu sana kwa Mungu kama walivyo mmalaika wengine kama vile makerubi, maserafi hasa walijishugulisha katika kumwabudu Mungu.

Maserafi wana mabawa sita;
 (Isaya 6:2,6). Wana nguvu uwezo wa kuondoa makosa yaletayo dhambi na kuwaandaa manabii kwa kuwatakasa (Isaya. 6:7). Kuwa na mabawa sita inadhihirisha ukuu na uwezo wao katika utendaji wao wa kazi mbalimbali.
Kwa hiyo hawa maserafi ni “moto wa mbinguni”
  (Kum. 8:15),( Isa. 14:29; 30:6). Mungu aliwatuma ili waweze kuwaadhibu watu waliotenda dhambi. KWAHIVI TUNA WEZA KUSEMA WANAWAKILISHWA KWA NJIA YA MOTO.

Pia kuna malaika wengine wakuu wanatajwa mfano Gabrieli, mikaeli, Urieli malaika mkuu wa dunia na watu wakali) na Raphaeli, Ragueli (ambaye analipiza kisasi juu ya
dunia na mwangaza) na Saragaeli. Hawa wanapatikana katika kitabu cha Henoko
(Luka1;26-38),(Luka1;11-20),(Danieli10;13)pia(Daniel12;1 )
(Ufunuo12;7-8)
 ,
Hawa maserafi wana tambulikana kama makerubi wanao kizunguka Kiti cha Enzi cha Mungu kama tunavyoona hapo juu ( Hii ni kwa ufupi ). Barikiwa na Roho mtakatifu atufundishe zaidi kwani sisi wanadamu tunajua kwa sehemu.

UTHIBITISHO KWAMBA MALAIKA WANA WEZA KUWA KATI YETU.

Katika Maandiko, tunaona matukio mengi ambayo malaika walikuwa sehemu muhimu ya mpango wa Mungu. Mstari mmoja unaonyesha uwezekano wa malaika kutembea miongoni mwetu hii leo: "Msisahau kuwafadhili wageni; maana kwa njia hii wengine
wamewakaribisha malaika pasipo kujua" (Waebrania 13: 2). Kumbukumbu dhahiri ni kwa Ibrahimu, ambaye malaika wake alimtokea kama wanaume (Mwanzo 18). Aya hii inaweza
au isiweze kuthibitisha kwamba malaika kwa kweli hutembea kati  yetu bila kujua.

Kuna mifano kadhaa ya maandiko ya kukutana na malaika, kwa hiyo tunajua kwamba Mungu anaweza kutumia malaika kutekeleza mambo fulani. Jambo tusilolijua kwa uhakika ni mara ngapi malaika wanajiruhusu kuonekana na watu. Malaika anaweza kuwafundisha watu (Mwanzo 16: 9), kuwasaidia watu (Danieli 6:22), kutoa ujumbe kwa watu (Luka 1:35), kuonekana katika maono na ndoto (Danieli 10: 13), kulinda watu (Kutoka 23:20), na kusaidia kufanya
mipango ya Mungu.(Got questions ).
 NI JINSI GANI MALAIKA WANAVYOTUHUDUMIA?
    
Kwa mwamini, kule kufahamu kwamba malaika wapo kwa faida yake hii ni msaada wa kutosha. Hii ni sawa na mtu anavyo weza kumwamini daktari anapomfanyia upasuaji, hatakama amepigwa  sindano ya ganzi lakini bado anamuamini daktari, huyu ni mwanadamu si zaidi sana malaika wanao fanya kazi ya Mungu?.

Kwa kifupi ni kwamba, kweli malaika wanaishi na wapo kwa ajili ya kutusaidia kama tunamcha Mungu. Ukweli hautegemei yale tunayoyaona. Tatizo la wanadamu tunapenda kuviamini zaidi vitu vinavyo onekana  ambavyo ni vya muda tu, tunasahau kuwa  visivyo onekana ni vya milele ((2Wakorintho 4:18).

Wakati jeshi la mbinguni wanapotumwa kuwakusanya wateule pamoja kwa ajili ya hukumu Yesu atakaporudi, wateule wataweza kukutana na kuwaona malaika kwa mara ya kwanza mwaliko huenda ukawa hivi, ‘Bwana amekuja anawaita!" (Yohana 11:28): "Unifumbue macho yangu, ili niyatazame maajabu yatokayo katika Sheria yako". (Zaburi 119:18).
     
Biblia inasema pia Atakuagizia malaika zake wakulinde katika njia zako zote (Zaburi 91;11) Kumbe wako viumbe ambao wamewekwa na Mungu kwa shughuli mbalimbali ikiwa ni pamoja na ulinzi wa watu wa Mungu, wakati lile kundi la pili si kundi jema wao wapo kwa ajili ya kudhuru, kushawishi kutenda uovu, kukatisha tamaa na kuwapinga wanadamu wenye asili ya uumbaji wa Mungu kwa sura na mfano wake wakitesa na kuua na kuharibu, haya sio mawazo ya kipuuzi kama wanavyo fikiri wana sayansi ambao hawaamini katika mambo yasiyoweza kupimwa na kuthibitika kwa kuonekana kwa macho.Pia huongoza katika njia sahihi. (Kut 23;20-22)

Tunapaswa kuwa na heshima kwa Mungu wetu na kujua mipaka tuliyo nayo, Mungu amewaumba malaika ili awatumie kwa mapenzi yake na sio wana damu kuwa amrisha wanacho taka hatakama ni cha kiovu bali jambo sahihi ni kumwomba Mungu atuagizie malaika hii, walau itapendeza kwani yeye ndiye ajuaye ni malaika yupi atakaye faa, zaidi sana unaweza tu kuzungu mza na malaika ambaye amesha kwisha kutumwa kwako (Lk 1:26-38) hapa utakuta malaika walitumwa ndipo hao wandamu wakaweza kuzungu mza nao, (Waebrania 1;1314 )“ Je yuko malaika aliyemwambia wakati wowote Uketi mkono wangu wa kuume hata nitakapoweka adui zako chini ya nyayo zako? Je hao wote si roho watumikao wakitumwa kuwahudumu wale watakaourithi wokovu? Ninacho taka kumaanisha ni hiki unapotambua malaika waliotumwa kwaajili yako halafu ukazungumza nao ndiyo unaweza kupata msaada kwa mfano inajulikana kuwa kila mwanadamu anamalaika wake walinzi hivyo unaweza kuzungumza nao, lakini kuwaamuru moja kwa moja bila mapenzi ya Mungu  hainogi sana
                                                      
Ni kweli kwamba huenda mwanadamu akawa ni muhimu zaidi mbele za Mungu kuliko malaika lakini lazima tutambue pia kuwa wenda nafasi ya malaika ikawa tofauti na sisi wanadamu kwa kumjua Mungu au kuwa karibu na Mungu “Angalieni, msidharau mmojawapo wadogo hawa, kwa maana nawaambia ya kwamba malaika zao mbinguni sikuzote huutazama uso wa Baba yangu aliye mbinguni” (Math18:10).hivyo kuwa sikiliza na kuwaheshimu ni vema kwani itatusaidia kumjua zaidi Mungu.

Hakuna matukio katika Maandiko ambapo wanadamu waliweza kutoa amri za malaika, ama kwa jina lao au kwa jina la Yesu. Hakuna vifungu ambapo mtu ana mamlaka juu ya kazi ya
malaika. Tunajua kwamba wao ni viumbe wa cheo cha juu, kwa sababu Yesu amejiweka yeye mwenyewe "kiwango cha chini kuliko malaika" ili azaliwa na kuteseka kama mwanadamu (Waebrania 2: 79; Zaburi 8: 4).

Mafundisho kwamba waumini wana mamlaka juu ya malaika ni uongo. Kanuni zifuatazo za Biblia zinaonyesha kwamba malaika hawatii amri za wanadamu:
• Tazama maneno ya Musa "Tulimlilia MwenyeziMungu, naye akakisikiakilio chetu, akatuletea malaika aliyetuondoa Misri" (Hesabu 20:16). Waisraeli hawakuamuru malaika kuja kwao. Walimwomba Mungu, ambaye chini ya amri yake malaika hufanya kazi. Shadraki, Meshaki, na Abednego walikataa kuinamia sanamu ya Nebukadneza (Danieli 3:1718). Mungu kwa rehema yake "alimtuma malaika wake na kuwaokoa watumishi wake"

AMINI KWAMBA UNALINDWA NA JESHI KUBWA SANA LA MALAIKA.

Elisha aliomba maombi ili Bwana amfungue macho mtumishi wake (2Wafalme 6;1317) mara moja mtumishi wa Elisha alifunguliwa macho yake na aliona jeshi kubwa sana la kiroho (malaika), hata ingawa jeshi la washami lilipozwa na Israel walipata ushindi wa bila mapigano lakini tunapata ufunuo mkubwa wa kuweko kwa kundi kubwa la malaika wanao wahudumia wale wanaourithi wokovu. Ikiwa huduma hii kubwa ya malaika ilikuwa hivi wakati wa Elisha ni muhimu kufahamu kuwa nyakati za agano jipya sisi tuko chini ya agano lililo bora zaidi na roho hawa hutumwa kwaajili ya kutuhudumia Biblia inasema hivi katika (Waebrania 1;1314 )“ Je yuko malaika aliyemwambia wakati wowote uketi mkono wangu wa kuume hata nitakapoweka adui zako chini ya nyayo zako? Je hao wote si roho watumikao wakitumwa kuwahudumu wale watakaourithi wokovu?”

Agano jipya pia linatupa ufunuo fulani kuhusu malaika na huduma zao aidha, Paulo mtume alikuwa akiwafundisha wakristo kule Efeso kuwa na ufahamu kuhusu maswala ya ulimwengu wa kiroho, ( Waefeso 6;10-18), ulimwengu wa kiroho unamajeshi makubwa ya makundi ya malaika ,makundi haya yamegawanyika katika sehemu kuu mbili, malaika wateule yaani wale walioonyesha utii kwa Mungu walipopata nafasi ya kutumia utashi wao na kundi linguine ni la malaika walioasi  kutoka katika kundi la malaika wateule lakini waliamua kwa utashi wao kumfuata shetani na hivyo kuwa pamoja na shetani na kumtumikia yeye na kupewa majina mengi yanayofanana na utendaji wao wa kazi majina waliyopewa ni Mashetani,  majini,  mapepo,  roho chafu, maruhani, na kadhalika, jina linalotumika katika Biblia kuhusu viumbe hao ni Pepo wachafu, hili ndilo tutakalolitumia zaidi katika kitabu hiki au somo hili. Ni jambo la furaha sana kujifunza kuhusu malaika.
                                              
                                  MUHIMU
   
Malaika wapo katika uwepo wa Mungu au wanafanya kazi ndani ya ramani au ulimwengu wa Roho wa Mungu, kwasababu wao pia ni rohowema, kumbuka hapa sizungumzii roho au malaika waasi, kwa maana hiyo wapo malaika wema na wabaya malaika wabaya malaika wabaya nikama vile mashetani wanaofanya kazi za kishetani ndio maana ili  malaika wema watusaidie vizuri tunapaswa kuwa watakatifu, hiki ni kitu kinacho wafanya wafanye makao ndani yetu na kuzungukia Mambo yetu yote kila mmoja na kazi yake .

Wao wana ya tambua matakwa ya Roho mtakatifu hata kabla wewe huja yajua ndio maana kuna wakati mtu anaweza kupata ujumbe fulani kiroho halafu akasema ahsante Roho mtakatifu kwa kunipa ujumbe kumbe kunawakati hatujui kuwa ni kweli Roho mtakatifu anatufundisha  lakini kumbe aliye mpa ujumbe  ni malaika wa upashaji wa habari { Gabrieli } .Ufahamu tunapanua hivi. kuna Mungu Baba, Huyu ni roho,  Kuna Mungu mwana huyu ni Mwili na Roho , Kuna Mungu roho Mtakatifu huyu naye ni Mungu Yule Yule lakini ameonekana kwa sura, kazi au kitengo tofauti , hivyo malaika naye ni roho lakini inategemea anajihusisha kufanya nini hawa wote ni roho unapo wafahamu vizuri kunawakati itakusaidia sana nisawa na wakati unakemea pepo,  sawa ni shetani yule yule lakini usipo tambua ni pepo gani ili umlenge moja kwa moja unaweza ukachukua muda sana kumwondoa  sio kwa sababu hauna nguvu za Mungu bali ni kwa sababu haumjui unaye pambana naye.


KWANINI TUWATUMIE MALAIKA KATIKA MAMBO YETU?

Hapa simaanishi kuwaabudu bali  tunapaswa kuwaheshimu na kuwa karibu nao kwani wameumbwa kwaajili ya kumtumikia Mungu katika maisha  yetu wanadamu.

v  Inaonesha hawa pendezewi na mwanadamu kupotea dhambini ndiyomaana mtenda dhambi mmoja anapotubu na kugeuka kumwelekea Mungu, “malaika hushangilia.” (Luka 15:10)
v  Hufanya kituo mahali palipo patakatifu palipo andaliwa  kwaajili ya utukufu wa Mungu mfano ibada n.k
v  Mungu ana watumia sana kuwaimarisha na kuwalinda watumishi wake wa aminifu hapa duniani. (Waebrania 1:14)
v  Wana uwezo wa kukunyakua kutoka juu, ili utue chini kwa usalama (muulize Yesu alipochukuliwa mpaka juu ya mnara wa hekalu ili ajaribiwe ali ambiwa nini na ibilisi ? ndipo utakapo jua kazi kubwa ya malaika ambayo haya ibilisi anaijua)
v  Malaika anaweza kutuongoza mpakapale tulipo tengenezawa(Kut 23;20-22)

v Malaika wanaweza kuwafunga vinywa maadui ikiwa ni mpango wa Mungu mfano; nabii Danieli alitupwa ndani ya shimo la simba, haku umizwa. Kwa nini?  Kwasababu “Mungu wangu mwenyewe alimtuma malaika wake na kufunga vinywa vya simba.” (Danieli 6:22).
v  Malaika wanaweza kukuchukua katika roho na kukupeleka pahala fulani ili kukuonesha mambofulani au kuna wakati unaweza kupelekwa katika altare ya Yesu yaani katika ulimwengu wa kiroho ili Yesu akutatulie mamboyako,( operation iliyoko katika ulimwengu wa  kiroho) hii unaweza ielewa vizuri ukikutana na watu ambao walikuwa na vimbe katika sehemu fulani za miili yao halafu hospitari wakaambia vipimo havisomi lakini baada ya Malaika wa uponyaji kushughirika wakajikuta vimbe zime yeyuka 










USHUHUDA; Mimi mwenyewe niliwahi fanyiwa upasuaji operation/surgery ya shingo ilikuwa haina uwezo wa kugeuka nyuma kalibu wiki zima, pia  niliponywa macho yalipokuwa yaki uma ghafla utadhani yamewekwa pilipili au vumbi lakini huku nikisikiliza wimbo uitwao (ALTARE KWA BWANA YESU NDIO HAZINA YETU MALAIKA NIPELEKENI YESU UNIOKOE ) nikiwa katika muunganiko wa ki-roho na ndipo nilipo gundua kuwa kumbe malaika wana mchango mkubwa sana maishani mwetu, hii ni kwasababu niliomba na kukemea  sana siku nzima lakini sikupona,   nafikiri kuna wakati unatakiwa upelekwe katika wodi la kiroho ili ufanyiwe uchunguzi na Bwana Yesu  pata wimbo huo utafakari. NB; Huu ushuhuda sijaumaiza nikipande tu kwa ufupi.

v   Unaweza kuepushwa na janga fulani ikiwa ni mapenzi ya Mungu kwa mfano; Lutu na binti zake kwa msaada wa malaika wali okolewa na kupelekwa nje ya mji wa Sodoma na Gomora ulio teketezwa kwa moto kutokana na uovu
v   Kwa sababu hata Ibrahimu aliwatumia ili kuwaomba kupunguzwa kwa adhabu.
v   Malaika anaweza kuleta taarifa  .” (Ufunuo 14:6, 7) mfano;  pale kaburini walio kwenda kulitazama kaburi la Yesu malaika akawatokea na kuwaambia kwanini mnamtafuta aliye hai kati ya waliokufa?   Mariamu alipashwa habari na Malaika wa Bwana kuwa ata pata mimba na kumzaa mtoto wa kifamle
Pia taarifa ya kuwa  Sara mke wa Ibrahimu atazaa mtoto mwakani mida kama hii ni malaika walio mtokea Ibrahimu
Tukianza kujifunza juu ya malaika  Mungu ataendelea kutufundisha.

NB: Kunawakati malaika huwapa watu taarifa halafu wao wanasema ni machale yao sasa sijui machale ndio nini .

v   Pia wana uwezo wa kuondoa matatizo yetu mfano ; pale walipo liondoa jiwe katika kaburi la Yesu ili asitoroke .
v   Wanaweza kututia nguvu tunapo ishiwa nguvu , malaika alimtokea  Yesu na “akamtia nguvu.” (Luka 22:43)
v   Petro kutoka gerezani.  Ilikuwa ni kwa msaada wa malaika (Matendo 12:6-11).
v   Wao hufanya makao kwa wale walio safi kiroho wanao pigania utakatifu au wema au usafi (Zaburi 34:7).
NB: Hata hivyo,  ni lazima tukumbuke kwamba malaika wana mtumikia Mungu wala si wanadamu. (Zaburi 103:20, 21) Wanafuata mwongozo wa Mungu bali si maagizo au mao
ya wanadamu. Hivyo, Mungu ndiye tunaye paswa kumuomba msaada, sio malaika. (Mathayo 26:53).

Pia, Maandiko yanatuambia kwamba sala zetu na ibada yetu inapaswa kuelekezwa kwa Mungu peke yake. (Kutoka 20:3-5; Zaburi 5:1, 2; Mathayo 6:9) Malaika waaminifu hututia moyo tufanye hivyo. (Ufunuo 19:10)

Labda Mungu akikwambia uwatume au kuwaagiza na sio kwa mapenzi yako bali msikilize Mungu hii ni kwasababu usije ukadhani unawatuma kumbe wakawa hawa kuelewi maana hauja angalia mapenzi ya Mungu ninini, tambua kwamba malaika wapo makini sana kumsikiliza zaidi Mungu na huu ndiyo uaminifu walio nao.

   MFANO WA KUOMBA MSAADA WA MALAIKA
       
Ee Mungu mwenye nguvu, nina kuja kwako kwa unyenyekevu kupitia  jina la mwanao Yesu kristo nakuomba uniagizie malaika wa vita/wa uponyaji/taarifa/mlinzi/, ili wanisaidie kupigana na maadui zangu kwa jina la Yesu mwanao nimeomba amina.
                                                
                                                 Au

 Mungu Baba ninakuja mbele zako kwa njia ya kristo mwanao mpendwa,  nina jua unanisikiliza daima,  hivyo ninatamani kupata taarifa au ujumbe juu ya  mgonjwa huyu au tatizo……..  kwakuwa wewe ni Mungu wa siri, nina kusihi Bwana na Muumba wangu uniagizie malaika ili anijurishe namna ya kulitatua tatizo hili, maana nina amini utakapo nipa taarifa utanipa na namna ya kulitatua, Roho mtakatifu niongoze kuelewa ujumbe nitakao letewa,ninapopata ujumbe, adui ashindwa kuuiba kwa jina la Yesu amina. (Sasa wakisha kuja hapo ndio unaweza watumia kuwa uliza maswali au kuwaomba msaada zaidi na wao watajua namna ya kukusaidia lakini haya yote lazima uwe na macho ya rohoni)

Nimekupa muongozo huu kwasababu hawa hawana mamlaka kuliko Mungu bali hufuata maagizo ya Mungu  yaani  wao  humtumikia Mungu ila kwa kuwa mimi na wewe tuna wafahamu na kazi zao, basi tuna mwomba Mungu msaada wao ,ni sawa na mtu anapo hitaji msaada fulani  wa wanajeshi, kumsaidia suala fulani,  ni muhimu kumuona kiongozi mkuu ili awatume kukusaidia  na wakitumwa na mkuu hufanya kazi kwa nguvu zote. Sasa kiongozi mkuu wa jeshi la malaika ni yesu kristo ambaye ndiye malaika mikaeli.

Tunawathamini sana malaika hao waaminifu ambao siku zote hutekeleza maagizo ya Mungu! Huwa tumia kuwa saidia na kuwa linda watumishi wake waaminifu walio duniani hii ina tutia sana nguvu  kwa sababu kuna viumbe wa roho hatari ambao wanaitwa roho waovu wanaotaka kutudhuru

NB: Hawa ni baadhi tu ya malaika wapo wengi sana lakini tukiwa na ufahamu tu, juu ya uwepo wao na kazi zao katika maisha ya mwanadamu,  inaweza kutusaidia. Na kazi hizi zote anaye zifanya ni Mungu yuleyule mmoja kupitia jeshi lake la malaika kila mmoja na kitengo chake.
   
SHETANI  HUJIFANYA  KAMA  MALAIKA WA NURU.

kwa kuwa uwiano wa uovu na giza, na uzuri na mwanga, ni mfano inayofanana yenye nguvu katika historia ya mwanadamu. Katika Biblia, nuru ni mfano wa kiroho wa kweli na asili ya Mungu isiyobadilika (Yakobo 1:17). Hutumiwa mara kwa mara katika Biblia kutusaidia kuelewa kwamba Mungu ni mzuri kabisa na wa kweli (1 Yohana 1: 5). Tunapokuwa "katika nuru," tuko pamoja Naye (1 Petro 2: 9).
                                                                                
           
        FAHAMU ZAIDI KUHUSU MALAIKA

·       Malaika wema kazi yao ni kutuombea, kutumwa na Mungu kwetu, na wanatulinda kama Malaika walinzi. (Ebr, 13:2). Ambapo kila
·       Mwanadamu anaMalaika wake wa kumlinda na kumuongoza Roho na Mwili, ndie Malaika wake mlinzi, (Zab, 91:11, Mt. 18:10).
·       Malaika wote sio sawa, wapo Malaika Wakuu, Malaika wanaomtumikia Mungu Mbinguni kwa mfano Makerubi na Maserafi, na pia wapoMalaika walinzi.
·       Malaika wakuu ni Mikaeli, Gabrieli na Raphaeli (Dn, 10:13, Tobiti 12:15, Lk 1:26).
·       Mashetani kazi yao ni kuteswa Motoni na hutaka kudhuru Roho na Miili ya wanadamuna kutupoteza milele. (1 Petro, 5:8, Yoh, 8:44).      
·       Hapo Mwanzo Mungu aliumba Malaika katika hali ya njema na Heri kubwa. Kisha aliumba mbingu na nchi, na viumbe vyotevinavyoonekana na visivyoonekena. (Kol, 1;16, Mwa, 1;31)
·       Malaika ni viumbe vilivyo Roho tupu na vyenye akili na utashi. (Zab 91:11, Ebr 1:7, Uf, 12:7-9).
·       Malaika wengine walikosa kwa kumkaidi Mungu, wakatupwa motoni na ndio Mashetani ambao Mkubwa wao ni Lusiferi. (Yn, 8:44: Uf12:7-9,).
·       Mungu aliumba Malaika ili Wamtukuze, Wafurahi nae Mbinguni na wawe Matarishi/wajumbe wake kwa Wanadamu. (Tob 12:12, Lk.16:22).








            Imeandaliwa na  E.mkinga
NB;kusharea  kwenye makundi ya mitandao mbalimbali ya kijamii kama vile
                                     WatsApp, Instagram ,Twitter,Facebook
                   KISIMA CHA BARAKA
Kisimachabaraka.blogspot.com